- Abdullah bin Masood anatuelezea hadithi ambayo baadhi ya vipengele vyake ni mambo ya siri ambayo hakuna anaye jua uhalisia wake ila Mwenyezi Mungu Mtukufu, ndio maana akasema: (na yeye ndiye mkweli anae kubalika) sawa sawa katika mambo ya wazi au siri. Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) anaelezea hali za kijusi na hatua za kuumbika kwake katika tumbo la mama. Anakuwa ni tone la maji, maji ya uzazi ya baba na yai la mama, na eneo la kuumbiwa ni katika kizazi cha mama, kisha anakuwa pande la damu lililo ganda, linaitwa a’laqah, yaani kinacho ganda au kuning’inia, na limeitwa hivyo kwa sababu huwa linaganda katika kuta za kizazi, kisha linakuwa pande la nyama, ni kipande cha nyama kidogo kiasi ambacho inawezekana kukitafuna mdomoni.
2. Baada ya kuwa pande la nyama, Mwenyezi mungu anamuamrisha malaika msimamizi wa vizazi, yaani viumbe pindi wanapokuwa tumboni kwa mama, aandike mambo yake yote, anaandika riziki yake, kifo chake, matendo yake na atakuwa mwema au muovu. Lakini pia huwa anandika mambo zaidi ya hayo, kama vile, atakuwa jinsia ya kike au kiume,[1] tabia zake na maumbile yake[2]. Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) aliyataja hayo mambo manne kwa sababu mengine yanaingia ndani yake , na kwa kuzingatia umuhimu wake. Haya anayo yaandika malaika si aliyo yaandika Mwenyezi Mungu katika Lauhul mahfuudh (palipo andikwa mambo yote yanayotokea), haya anayo yaandika malaika, kuna uwezekano wa kufutwa au kurekebishwa au kubadilishwa kwa sababu alizo ziweka Mwenyezi Mungu, kama dua na matendo mema, tofauti na aliyo yathibitisha Mwenyezi Mungu katika Lauhul mahfuudh, hayo haiwezekani kuyabadilisha wala kuyarekebisha.
‘‘ Mwenyezi Mungu hufuta na huthibitisha ayatakayo. Na asili ya hukumu zote iko kwake.
3. Hapo ndipo Mwenyezi Mungu anapulizia kijusi roho na kinakuwa hai kwa uwezo wake Mtukufu. Kupulizia roho ni katika mambo ya ghaibu ambayo anayajua Mwenyezi Mungu pekee, na amelificha viumbe wake wasilijue,
amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
“ Na wanakuuliza khabari za Roho. Sema: Roho ni katika mambo ya Mola wangu Mlezi. Nanyi hamkupewa katika ilimu ila kidogo tu."
, Bali sisi wajibu wetu ni kuamini kwa yakini alicho kielezea
Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake)
‘‘kutoka kwa Mola wake kwamba “ Hakika amri yake anapo taka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na kikawa. ” .
Hayo yote hutokea pindi pande la nyama linapo kuwa kikamilifu na tutengeneza umbile la binadamu,
amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
“5. Enyi watu! Ikiwa nyinyi mna shaka ya kufufuliwa basi kwa hakika Sisi tulikuumbeni kutokana na udongo, kisha kutokana na manii, kisha kutokana na kipande cha damu ilio gandana, kisha kutokana na kipande cha nyama chenye umbo na kisicho kuwa na umbo",
Pande la nyama lililo jiweka katika Umbile, ni lililo umbika kikamilifu, katika sura ya binadamu, na pande la nyama ambalo halijajiweka katika umbile, ni ambalo alijaumbika kikamilifu katika sura ya binadamu, hili huwa linapolomoka, inakuwa ni mimba liyotoka[4].
4. Kisha Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) akaeleza kwamba, kinacho zingatiwa katika matendo ni mwisho wake, na yote yaliyo tangulia yanabaki katika elimu ya Mwenyezi Mungu na jinsi alivyo andika ubaya au uzuri kwa mja. Huenda mtu akatenda matendo ya watu wa Motoni kwa muda Mrefu mpaka kifo chake kinapo karibia, Mwenyezi Mungu anamuafikisha, anatubia na anamsamehe na kuhitimisha uhai wake kwa matendo mema na kuingia Peponi, kwa sababu Mwenyezi Mungu alisha andika katika Lauhul mahfuudh (palipo andikwa mambo yote yanayotokea), na katika tumbo la mama yake alipo muagiza malaika, kwamba atakuwa mwema.
5. Na kinyume chake, mtu anaweza kutenda matendo ya watu wa Peponi kwa muda mrefu, mpaka anakaribia kuingia Peponi kwa kukaribia kifo chake, lakini anatanguliwa na aliyo yaandika Mwenyezi Mungu kwamba atakuwa muovu, anatenda matendo ya watu wa Motoni na anakufa katika hali hiyo na kuwa katika watu wa Motoni. Hii haimanishi kwamba muumini anaweza kupotea baada ya kuongoka bila sababu kutoka kwake mwenyewe. Hayo yote ni kwa hekima na uadilifu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa mfano, mtu anaye muabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu bila elimu, kwa jinsi anavyo jisikia, akipatwa na kheri anashukuru, ikiwa kinyume anakufuru, kama alivyo sema
“Na katika watu wapo wanao muabudu Mwenyezi Mungu kwa ukingoni. Ikimfikia kheri hutulia kwayo, na ukimfikia msukosuko hugeuza uso wake. Amekhasiri dunia na Akhera; hiyo ndiyo khasara iliyo wazi."
Na mfano ni mnafiki, katika hadithi: “Mtu anaweza kutenda matendo ya watu wa Peponi – katika macho ya watu – hali ya kuwa ni mtu wa Motoni, na mtu anaweza kutenda matendo ya watu wa Motoni – katika macho ya watu – hali ya kuwa ni mtu wa Peponi”[5]. Na mwisho wa uhai kama huu, kwa mtu ambaye kwa muonekano ni mwema, ni katika matukio adimu sana yasiyo onekana mara kwa mara, na hekima yeke ni kuonesha kwamba, katika matendo kinacho zingatiwa ni mwisho wake, na mwanadamu kamwe asijidangaye kwa wingi wa ibada na matendo yake mazuri. Hii ni miongoni mwa huruma za Mwenyezi Mungu, kwani watu kutubia na kuacha maovu inatokea kwa wingi sana, ama kubadilika na kuwa waovu ni nadra, ingelikuwa ni kinyume, watu wangelipata Mtihani mkubwa sana[6].
Mara nyingi inavyo julikana ni kwamba watu wema huwafikishwa kutenda mema, na waovu hutenda mauvu, kama ilivyo bainishwa katika hadithi kwamba Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) anasema: “hakuna yeyote kati yenu wala yeyote ambeye amepuliziwa uhai, ila huandikwa nafasi yake Peponi na nafasi yake Motoni, japo imeadikiwa kuwa ni mwema au muovu”, bwana mmoja akasema: eh Mtume wa Mwenyezi Mungu, si tuache kutenda mema na tusubiri matokeo kama ilivyo andikwa? Atakae kuwa ni mwema, ataingia katika wema, na atakae kuwa ni muovu, ataingia katika waovu,
Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) akasema:
“wema watawekewa wepesi kufanya mema, na waovu watawekewa wepesi kufanya maovu” kisha akasoma: “Na akaliwafiki lilio jema, ”
MAFUNDISHO
- Amesema Ibn masood, katika kuelezea sifa ya Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake): “mkweli anae kubalika”, hii ni kuonesha jinsi alivyo muamini, kumkubali na kutekeleza aliyo kuja nayo kikamilifu hata kama akielezea mambo ambayo yako kinyume kiakilia, au juu ya uwezo wa aikili kuyakubali au kuyakanusha katika mambo ya ghaibu. Na ndio maana maswahaba ni watu bora baada ya manabii, na kiigizo cha waumini katika kumuamni Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) na kufuata mafundisho yake.
2.Ameeleza Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) hatua za ukuaji wa kijusi katika tumbo la mama kabla ya teknolojia ya kitabibu na vifaa vya kisasa vilivyo thibitisha ukweli wa maneno ya Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake). Jambo hili ni katika mambo yenye kumzidishia muumini Imani, pindi anapo ona Sayansi inathibitisha kilicho elezewa takika Qur`ani na mafundisho ya Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) na wala hakuna mgongano wowote.
3.Tizama uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kubadisha kijusi katika hatua tofauti tofauti, na katika kupanga mipango kwa njia nzuri yenye kustaajabisha. Mfano wa mambo kama haya yanepelekea kumtukuza Mwenyezi Mungu zaidi na kujisalimisha kweke.
4.Lau mwanadamu angezingatia na kujua hekima ya kuumbwa mwanadamu hatua kwa hatua, na hali ya kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ana uwezo wa kukiambia kitu: kuwa na kikawa jinsi atakavyo. Hii ni kuilea nafsi iwe na utulivu na umakini, na isiwe na papara katika mambo na kutaka matokeo ya haraka, kama inavyo tuonesha mahusiano makubwa aliyo yaweka Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani ziwe juu yake) baina ya kufanya sababu na kupata matokeo yake kwa kuzingatia utaratibu wa kilimwengu.
5.Ukipatwa na jambo katika kazi yako, au riziki yako, au ukatamani upate jambo ambalo hauna, usihangaike kulaumu Qadar yaani mipango ya Mwenyezi Mungu, au kujuta na kuishusha nafsi, bali ridhia alicho kuandikia Mwenyezi Mungu Mtukufu, na utambue kwamba ameliandika ukiwa katika tumbo la mama, na kabla ya kuingia katika tumbo la mama Hakuna zaidi ya kujisalimisha kwake na kufanya anayo yaridhia.
6.Haifai kwa mwanadamu kumuhukumu yeyote kuwa ni mtu wa Peponi au Motoni, kwa sababu hilo ni la Mwenyezi Mungu pekee, na yeye ndiye ameandika matendo yote ya waja, muovu anaweza akawa mwema, na mwema anaweza akawa muovu.
7.Haifai kwa mwanadamu kubweteka na matendo yake na kuacha jitihada, kwa sababu kinacho zingatiwa katika matendo ni mwisho wake. Sufian Athauriy - Mwenyezi Mungu amrehemu – alikuwa analia akisema: “naogopea isije ikawa katika lauhul mahafudh yaani palipo andikwa mambo yote yanayotokea, imeandikwa kwamba mimi ni muovu”, na alikuwa akisema: “naogopea kupokonywa Imani kabla ya kifo changu”[8].
8.Inatakiwa kwa mwislaam adumu katika kumuomba Mwenyezi Mungu amdumishe katika kumtii, na wala asimpoteze na akateleza. Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) alikuwa akikithrisha kusema: “Eh mwenye kubadisha nyoyo, nakuomba uudumishe moyo wangu katika dini yako”[9]
9.Ameeleza Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) kwamba, kuna mtu alisema: “ninaapa, Mwenyezi Mungu hatamsamehe fulani” na Mwenzi Mungu akasema: “ni nani anaapa juu yangu kwamba sitamsamehe fulani?! Kwa hakika nimesamehe na nimekufutia mema yako”[10].
10.Amesema Ally bin Abuu Twaalib: “jiepusheni kuwaiga watu, kwa sababu, mtu anaweza kutenda matendo ya watu wa Peponi kisha anabadilika, - kwa jinsi Mwenyezi Mungu anavyo juwa uhalisia wake – anatenda matendo ya watu wa Motoni, ana kufa akiwa katika watu wa Motoni, na mtu anaweza kutenda matendo ya watu wa Motoni kisha anabadilika - kwa jinsi Mwenyezi Mungu anavyo juwa uhalisia wake – anatenda matendo ya watu wa Peponi, anakufa na akiwa katika watu wa Peponi. Ikiwa hamna budi zaidi ya kumuiga, basi muige ambao walio kwisha tangulia mbele ya haki na wala si walio hai[11].
11.Amesema mshairi:
katikaa ulimwengu Mwenyezi Mungu ana dalili zinazo thibitsha uwepo wake***huenda ndogo kabisa ndiyo aliyo ifanya iwe sababu ya wewe kuongoka.
Huenda dalili za uwepo wake zilizopo katika nafsi***ni maajabu makubwa lau jicho lako likizama kwa mazingatio.
Na ulimwengu umejaa siri***kama jicho lako likitizama kwa kutaka undani wake.
Kiulize kijusi kinacho ishi peke yake***bila msimamizi wala chakula, ni nani ana kusimamia?
Marejeo
- Al-Bukhari (3333) na Muslim (2646)
- .Ishaq bin Rahwayh katika “Musnad” yake (2/344), na al-Ajri katika “Shari’ah” (365). Al-Haythami aliisahihisha katika “Majma’ Al-Zawa’id na Manbi Al-Fawa’id” (7/193)
- .Tazama: "sherh ya arobaini al-Nawawi" cha Ibn Rajab (uk. 45), "Fath al-Bari" cha Ibn Hajar (11/485)
- .Tazama: “Al-Mufhim lamaa 'ashakil min talkhis kitab muslimin” cha Al-Qurtubi (6/651)
- .Al-Bukhari (2898) na Muslim (112) kutoka katika Hadithi ya Sahel bin Saad Al-Saadi, M/Mungu amuwiye radhi
- .Ufafanuzi wa Arobaini Al-Nawawi cha Ibn Daqiq Al-Eid (uk. 39)
- .Al-Bukhari (1362) na Muslim (2647)
- .Ufafanuzi wa Arobaini Al-Nawawi cha Ibn Rajab (uk. 47)
- .Al-Tirmidhiy (2140), Ibn Majah (3834), kwa kutoka kwa Anas bin Malik, Al-Tirmidhiy amesema: Ni Hadithi nzuri.
- Muslim (2621), kutoka kwa Jundub bin Abdullah
- “i`ilam almuqiiin an rabi a`la amina"” na Ibn al-Qayyim (2/135).