عَنْ أَبِي ذَرٍّ، عَن النَّبِيِّ ، فِيمَا رَوَى عَن اللهِ تَبَارَكَ وَتَعَالَى أَنَّهُ قَالَ: «يَا عِبَادِي، إِنِّي حَرَّمْتُ الظُّلْمَ عَلَى نَفْسِي، وَجَعَلْتُهُ بَيْنَكُمْ مُحَرَّمًا؛ فَلا تَظَالَمُوا. يَا عِبَادِي، كُلُّكُمْ ضَالٌّ إِلَّا مَنْ هَدَيْتُهُ؛ فَاسْتَهْدُونِي أَهْدِكُمْ. يَا عِبَادِي، كُلُّكُمْ جَائِعٌ إِلَّا مَنْ أَطْعَمْتُهُ؛ فَاسْتَطْعِمُونِي أُطْعِمْكُمْ.يَا عِبَادِي، كُلُّكُمْ عَارٍ إِلَّا مَنْ كَسَوْتُهُ؛ فَاسْتَكْسُونِي أَكْسُكُمْ. يَا عِبَادِي، إِنَّكُمْ تُخْطِئُونَ بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ، وَأَنَا أَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعًا؛ فَاسْتَغْفِرُونِي أَغْفِرْ لَكُمْ. يَا عِبَادِي، إِنَّكُمْ لَنْ تَبْلُغُوا ضَرِّي فَتَضُرُّونِي، وَلَنْ تَبْلُغُوا نَفْعِي فَتَنْفَعُونِي. يَا عِبَادِي، لَوْ أَنَّ أَوَّلَكُمْ وَآخِرَكُمْ، وَإِنْسَكُمْ وَجِنَّكُمْ، كَانُوا عَلَى أَتْقَى قَلْبِ رَجُلٍ وَاحِدٍ مِنْكُمْ، مَا زَادَ ذَلِكَ فِي مُلْكِي شَيْئًا.يَا عِبَادِي، لَوْ أَنَّ أَوَّلَكُمْ وَآخِرَكُمْ، وَإِنْسَكُمْ وَجِنَّكُمْ، كَانُوا عَلَى أَفْجَرِ قَلْبِ رَجُلٍ وَاحِدٍ، مَا نَقَصَ ذَلِكَ مِنْ مُلْكِي شَيْئًا. يَا عِبَادِي، لَوْ أَنَّ أَوَّلَكُمْ وَآخِرَكُمْ، وَإِنْسَكُمْ وَجِنَّكُمْ، قَامُوا فِي صَعِيدٍ وَاحِدٍ فَسَأَلُونِي، فَأَعْطَيْتُ كُلَّ إِنْسَانٍ مَسْأَلَتَهُ، مَا نَقَصَ ذَلِكَ مِمَّا عِنْدِي إِلَّا كَمَا يَنْقُصُ المِخْيَطُ إِذَا أُدْخِلَ البَحْرَ. يَا عِبَادِي، إِنَّمَا هِيَ أَعْمَالُكُمْ أُحْصِيهَا لَكُمْ، ثُمَّ أُوَفِّيكُمْ إِيَّاهَا، فَمَنْ وَجَدَ خَيْرًا فَلْيَحْمَدِ اللهَ، وَمَنْ وَجَدَ غَيْرَ ذَلِكَ فَلا يَلُومَنَّ إِلَّا نَفْسَهُ».

Kutoka kwa Abuu Dharri, kutoka kwa Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake), aliyo yapokea kutoka kwa mola wake Mtukufu, hakika yeye amesema:

 “Enyi waja wangu, hakika mimi nimejiharamishia dhuluma, na nikaifanya kuwa haramu baina yenu, basi msidhulumiane.Enyi waja wangu, nyote mmepotea, ila niliye muongoza, basi niombeni uongofu, nami nitawaongoza.Enyi waja wangu, nyote mnanjaa ila niliye mpatia chakula, basi niombeni chakula, nami nitawapatieni.Enyi waja wangu, nyote mko uchi, ila niliye mvisha, basi niombeni mavazi nami nitawapatieni.Enyi waja wangu, hakika nyinyi mnakosea usiku na mchana, na mimi ninasamehe madhambi yote, basi niombeni msamaha nami nitawasamehe.Enyi waja wangu, hakika nyinyi hamuwezi kufanya juhudi za kunidhuru, mkanidhuru, na hamuwezi kufanya juhudi za kuninufaisha, mkaninufaisha.Enyi waja wangu, lau kuanzia wa mwanzo mpaka wa mwisho kati yenu, majini na watu, wakiwa ni kama moyo wa mtu mmoja aliye mcha Mwenyezi Mungu kati yenu, hilo haliongezi katika ufalme wangu chochote.Enyi waja wangu, lau kuanzia wa mwanzo mpaka wa mwisho kati yenu, majini na watu, wakiwa ni kama moyo wa mtu mmoja aliye muasi Mwenyezi Mungu kati yenu, hilo halipunguzi katika ufalme wangu chochote.Enyi waja wangu, lau kuanzia wa mwanzo mpaka wa mwisho kati yenu, majini na watu, wakisimama katika uwanja mmoja, wakaniomba, nikampa kila mmjo alicho kiomba, hilo halipunguzi chochote kwa nilivyo navyo, ila ni kama kiasi cha sindano inapo ingizwa baharini. Enyi waja wangu, hayo ni matendo yenu ninayadhibiti, kisha nitawalipa. Atakae pata kheri, basi amshukuru Mwenyezi Mungu, na atakae pata kinyue asimlaumu yeyote zaidi yake mwenyewe”

Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) anasimulia kutoka kwa Mola wake Mtukufu Hadithu qudusiyyu. Hadithu qudusiyyu, ni maneno ya Mwenyezi Mungu, amabayo si Qur`ani, yaani matamshi ni ya Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) na maana ni ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. kinyume na Qur`ani amabayo ni ya Mwenyezi Mungu, maneno na maana.

  1. Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaita waja wake kwa huruma: enyi waja wangu. Na anawaeleza kwamba amejiharamishia dhulumu japo kuwa yeye ni Muweza wa kila kitu, amesema Mtukufu:

    ““Hakika Mwenyezi Mungu hadhulumu hata uzito wa chembe moja”

    (An-Nisa: 40)

    Mwenyezi mungu ndiye mwenye ufalme na ndiye Muumba na mwenye amri, pamoja na hayo yote amekataa kudhulumu. Huu ni utangulizi wa kubainisha kwamba amewaharamishia watu dhuluma na kuwazuia wasidhulmiane.

Na Dhuluma maana yake; ni kuacha haki kwa kuweka kitu mahala pasipo stahiki. Na Mwenyezi Mungu ameharamisha ushirikina na kuufanya kuwa dhuluma kubwa. Kila dhuluma baina ya waja, katika nafsi, mali na heshima ni haramu hata kama ni kidogo sana. Mwenyezi amemuonya mdhulimaji:

“Wala usidhani kuwa Mwenyezi Mungu hana khabari na wanayoyafanya madhalimu.”

[Ibrahim: 42]

na akaamrisha uadilifu hata kwa maadui:

““Enyi mlio amini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu, Fanyeni uadilifu kwani kufanya Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu”

[Al- Maaidah: 8].

2.   Kisha Mwenyezi Mungu akawaita tena waja, na kuwaeleza kwamba viumbe wote wako katika upotevu, ila ambaye atamuonyesha haki na kumjalia aifuate; kwasababu wamezaliwa wakiwa hawajui chochote. Na mwanadamu kwa uwezo wake mdogo hawezi kujua kwa mtizamo wake ukweli wa kila jambo. Watu wametofaitiana wakatengeneza makundi, mambo yasiyo kuwa wazi yakakithiri, matamanio ya nafsi yakaenea. Mambo hayaendi kiakili, kwani kuna wenye akili wengi wameteleza. Na muongofu ni aliye ongozwa na Mwenyezi Mungu na kuwa imara katika haki, na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akaamrisha waja wamuombe uongofu.[1]

Uongofu haukomei kwenye kujaliwa kuwa mwislam, bali unajumuisha kujua hukumu na sheria zake, eidha kunyenyekea kwa kutekeleza aliyo yafundisha Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake), kwa sababu hii, Mwenyezi Mungu akawaamrisha waja wake waumini, wawe wanaomba katika Sala kwa kusema:

"Utuongoze kwenye njia iliyonyooka”

[Al-Fatihah: 6][2]. 


3.   Kisha tena Mwenyezi Mungu akawaita waja wake na kuwaeleza kwamba, viumbe wote wana njaa ila aliye mpatia chakula. Inatakiwa wamuombe yeye chakula; kwa sababu akitaka, anaharibu vyakula vyote ardhini, au anawafanya watu kuwa mafukara, au anawanyima chakula kwa kupitia maradhi au kuwekwa kizuizini au vyovyote vile. Hivyo basi mwanadamu hali chochote ila kwa fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu.

4.   Kisha tena Mwenyezi Mungu akawaita waja wake, na kuwambia kwamba viumbe wote wako uchi, hawana nguo ila aliye mvisha. Hivyo basi wanatkiwa wamuombe mavizi, kwani akitaka anawanyima. Chakula na mavazi ni mfano tu katika kuzungumzia riziki, viumbe wanahitaji riziki kutoka kwake kama wanavyo hitaji uongofu.:

““Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti.”

[Al-Dhariyat: 58].

5.   Kisha tena Mwenyezi Mungu akawaita waja wake na kuwakumbusha mapungufu yao ya kila siku ya kukosea usiku na mchana, na kwamba yeye anasamehe madhambi yote, kwa vyovyote yakatavyo kuwa mengi au makubwa, hivyo wanatakiwa wamuombe msamaha:

“Sema: Enyi waja wangu walio jidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu”

[Al-Zumar: 53]

 Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) ameeleza kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ananyosha mkono usiku ili aliye kosea mchana atubie, na ananyoosha mkono mchana ili aliye kosea usiku atubie mpaka juwa linachomoza”[3].6.   Kisha tena Mwenyezi Mungu akawaita waja wake na kuwaeleza kwamba wao si chochote mbele yake, hawamdhuru kwa ukafiri wala vita au chochote kile, kwani hawana uwezo huo na wao ni sehemu katika ufalme wake, na wala hawawezi kumnufaisha si kwa Imani wala msaada au chochote kile, kwa sababu yeye amejitosheleza. Kisha akataja mbele yake mifano ya kuonyesha jinsi alivyo jitosheleza.7.   Kisha tena Mwenyezi Mungu akarudia kuwaita waja wake na akawambia kwamba, utiifu wa waja haumnufaishi, lau ingelikuwa imani ya watu na majini, ni kama Imani ya Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake), hilo lisingelimzidishia lolote katika ufalme wake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Na anaye fanya juhudi basi bila ya shaka anafanya juhudi kwa ajili ya nafsi yake. Hakika Mwenyezi Mungu si mhitaji wa walimwengu”

[Al-Ankabut: 6]. 

8.   Kisha tena Mwenyezi Mungu akarudia kuwaita waja wake na akawambia kwamba, maasi yao hayamdhuru, lau kufuru  na maasi yao ingelikuwa kama kufuru ya Ibilisi, hilo lisingelimpunguzia chochote katika ufalme wake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Wala wasikuhuzunishe wale wanao kimbilia ukafirini. Hakika hao hawamdhuru kitu Mwenyezi Mungu. Bali Mwenyezi Mungu anataka asiwawekee chochote cha kuwafaa katika Akhera, na watapata adhabu kubwa (176) Hakika wale walio nunua ukafiri kwa Imani hawatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu, na wataadhibiwa adhabu chungu”

[Al Imran: 176, 177]. 


9.   Kisha Mwenyezi Mungu anasifia fadhila na neema zake ambazo haziesabiki wala kudhibitiwa, kwamba viumbe wote toka kuumbwa mbingu na Ardhi mpaka siku ya Kiyama, wakisimama katika eneo moja, kila mmoja  akamuomba anacho kitaka katika riziki na neema, na Mwenyezi Mungu akampa anacho kiomba, hilo haliathiri ufalme wake hata kidogo. Akatoa mfano wa sindano inapo wekwa baharini, je inapunguza chochote katika maji ya bahari?. Hivyo ndivyo zilivyo fadhila za Mwenyezi Mungu, hazina mwisho.

10.   Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akaeleza kwamba hatima ya mwanadamu inategemea matendo yake, kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu anaandika matendo yetu yote, kisha atatulipa. Atakaye pata kheri, amshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kumuongoza kuwa na Imani na kumjalia kutenda mema, na atakaye pata kinyume, basi ni mavuno ya matendo yake mwenyewe, yeye ndiye wa kulaumiwa, asimlaumu yeyote zaidi yeke mwenyewe.

Mafunzo

  1. Jihadhari na dhuluma, kwani ndiyo dhambi mbaya sana, zingatia maana yake ili usidumbukie ndani yake. Miongoni mwa dhuluma ni ushirikina, ambao ni kumuwekea Mwenyezi Mungu Mtukufu mwenza katika mambo ambayo haifa kuelekezewa zaidi yake yeye, hata kama ni shirki ndogo kwa kujionyesha mbele ya viumbe katika sala au elimu au vinginevyo. Miongoni mwa dhuluma, ni kudhulumu haki za waja, hata kama ni kwa kuwakata mishahara bila haki, au pakingi ya gari, au maneno ya mzaha. miongoni mwa dhuluma mbaya ni mtu kujidhulumu mwenyewe kwani anajiingiza motoni kwa starehe inayo isha.

  2. Tafakari kila unachotaka kukifanya, na daima kumbuka kumuomba Mola wako uongofu na riziki; hivyo viko katika mkono wa Mwenyezi Mungu pekee, naye anapenda kusikia mja anamuomba.

  3. Usizembee kumuomba Mwenyezi Mungu haja zako za Akhera, sisi tunamuhitajia Mwenyezi Mungu kila wakati, tuko uchi, tuna njaa, tumepotea ila kwa fadhila zake.

  4. Mwenyezi Mungu ametuumba ili tumtii, na akatuwekea usiku na mchana ili tumuabudu, pamoja na hayo yote, ni mara ngapi tunateleza na kutenda madhambi mchana au katika sitara ya usiku?!. Tuzibe mapungufu hayo kwa kufanya ibada na kumuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu msamaha daima, hasa asubuhi na jioni.

  5. Unapo fanya jambo jema, usiligeuze kuwa ni masimango, na wala usidhani kwamba ni lazima kujibiwa dua au kunyanyuliwa kwa sababu ya hilo jema, Mwenyezi Munge amerizika na wewe ndio muhitaji.

  6. Usihuzunike wala kuvunjika moyo unapoona maasi au kufuru, hilo halimdhuru Mwenyezi Mungu kwa lolote, kama Mola wako akitaka hawaezi kuyafanya. Tekeleza unayo amrishwa, kama ibada na nasaha, na wala usihuzunike.

  7. Usijione kwamba umeisha omba sana dua, na wala usidhani kwamba Mwenyezi Mungu anaona kwamba ameelemewa kutoa, amesema Mwenyezi Mungu:

    ““Vinamwomba Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi. Kila siku Yeye yumo katika mambo”

    [Al-Rahman: 29]

    . Na akasema Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake): “Mkono wa Mwenyezi Mungu umejaa, hauishiwi kwa kutoa, anatoa usiku na mchana; mnaona je alivyo vitoa toka kuumba mbingu na Ardhi? Kwa hakika havijaisha vilivyopo kuliani kwake”[4]

  8. Kutoa mifano ni katika njia zenye matunda mazuri katika kufundisha na kuathiri, tizama picha hii inavyo kita na kueleweka: (nikama kiasi cha sindano inapo ingizwa baharini.” jitahidi kubainisha na kusogeza kinacho lengwa kwa kutoa mifano ya karibu inayo onekana.[5]

  9. Amesema mshairi:Kwa hakika ninaapa, dhuluma ni mbaya***lakini mdhulumaji ndiye mbaya.Kesho siku ya malipo tunaenda kwa Mwenyezi Mungu***nambele yake watakutana walio kuwa na ugomvi

  10. Amesema Mshairi mwingine:Usimuombe mwanadamu akutatulie tatizo*** muombe ambae milango yake haifungwi.Mwenyezi Mungu anachukia usipo muomba***na mwanadamu akiombwa anachukia.

Marejeo

  1. Tazama: “Al-Mufhim lamaa 'ashkil min talkhis muslimin" cha Al-Qurtubi (6/552-553).
  2. Tazama: “Jami’ al-Ulum wa al-Hakam” cha Ibn Rajab al-Hanbali (2/40).
  3. Muslim (2759), kutoka kwa Abu Musa al-Ash’ari.
  4. Al-Bukhari (7419) na Muslim (993).
  5. Tazama: “Sharh Riyadh as-Salihin” cha Ibn Uthaymiyn (2/433).


Miradi ya Hadithi