عَنْ تَمِيمٍ الدَّارِيِّ رضى الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ قَالَ: «الدِّينُ النَّصِيحَةُ»، قُلْنَا: لِمَنْ؟ قَالَ: «لِلَّهِ، وَلِكِتَابِهِ،وَلِرَسُولِهِ،وَلِأَئِمَّةِ الْمُسْلِمِينَ، وَعَامَّتِهِمْ»


Kutoka kwa Tamim al-Dari (Radhi za Mwenyezi ziwe juu yakr) kwamba Mtume (Rehma na Amani zimshukie) amesema:1."Dini ni kunasihiana" 2.  Tukasema:

Kwa ajili ya nani? 3.Akasema: “Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu,4.Na kwa kitabu chake. 5.Na kwa Mtume wake. 6.Kwa viongozi wa Waislamu. 7. Na watu wote”.

  1. Amesema Mtume (Rehema na Amani zimshukie) kuwa Dini ni kupeana nasaha, na nasaha ni neno la ujumla linaloashiria kuwa mtu afanye bidii kuwafanyia wema wengine, Kwani kunasihi ni kama kuilinda Asali kutokana na uchafu.[1]Mtume (Rehma amani ziwe juu yake) akaifanya dini yote katika kupeana nasaha kwa sababu ya kuonesha utukufu wa jambo la kupeana nasaha, ingawa kuna mambo mengi katika dini lakini nasaha imepewa kipaumbele katika utukufu, kama Waarabu wanavyosema: Mali ni Ngamia.[2]

2.  Maswahaba wakauliza: Nasaha hii inatakiwa kwa ajili ya nani? Mtume (Rehma na amani ziwe Juu Yake) akawajibu kwa kuwabainishia kwa kusema:

3.  Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, maana ya “Nasaha” kwa Mwenyezi Mungu ni kumsafishia na kumtakasia Ibada yake kama inavyohitajika katika imani na matendo.

4.  Nasaha Kwa Kitabu Chake kitukufu, inayojumuisha utakaso wa kimatendo: ikiwemo kukiheshimu, kukifuata, na kukipenda.

5.  Nasaha kwa Mtume Wake, (Rehema na amani ziwe juu yake), inayojumuisha utakaso wa kimatendo: ikiwemo kumheshimu, kumfuata, na kumpenda.

Miongoni mwa nasaha kwa Mtume (Rehma na amani ziwe Juu Yake) ni kuyaeleza hayo katika familia na ndugu na jamaa. 

6.  Ama maimamu wa Waislamu ni Viongozi na Wanazuoni, nasaha kwao ni kujitahidi kufanya yale aliyowaamrisha Mwenyezi Mungu kwa upande wao, ikiwa ni pamoja na kuwatii katika wema, na kuwasaidia kutenda mema, na kuswali nyuma yao, na kupigania dini pamoja nao, na kutowafanyia uadui na maasi, na Kutowafuata wanapoteleza na kukosea. na kuwatetea kwa misingi ya haki.[3]

7.  Ama nasaha kwa Waislamu wote ni kuwanasihi katika kufanya juhudi kwa kufanya yale aliyowaamrisha Mwenyezi Mungu ili kuyafikia maslahi ya dini na dunia yao.Na hii ndio maana pana zaidi, na kwa ajili hiyo Mtume (Rehma na Amani zimshukie), akaweka kiapo cha utii kwa maswahaba zake juu ya kunasihi, na hiyo ni katika hadith Kutoka kwa Jarir bin Abdullah Al-Bajali amesema: “Niliweka kiapo cha utii kwa Mtume (Rehma amani ziwe juu yake), juu ya kusikiliza na kutii, na hayo Mtume alinitamkisha kiasi nilichoweza, ikiwemo kumnasihi muislam.[4]”Uhalisia wa nasaha uko kwa mtu mwenyewe, Kwani hulipwa kwa kufanya hivyyo, na Mwenyezi Mungu Mtukufu hana haja ya kuomba Ushauri kwa yeyote[5]. 

Mafunzo

  1. Tamim alikuwa si muislamu, akasilimu mwishoni mwa uhai wa Mtume (Rehma na Amani zimshukie) na akapigania dini pamoja naye, na akawa mfanya ibada mzuri sana, mwenye kusimama kuswali swala za usiku, na msomaji wa Qur’ani. Hapo tunajifunza kuwa Ikiwa iliwezekana kwa mtu ambaye alikuwa si muislamu, kufanya hayo yote basi wewe usikate tamaa au kumkatia tamaa ndugu yako, bali endelea kufanya bidii katika kujifunza na kufanyia kazi elimu yako. 

  2. Kuyabeba majukumu, na kuyatekeleza kwa bidii  na nia njema, ni katika nasaha, kwa kutimiza wajibu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Kitabu chake, na Mtume wake, na Viongozi wa Waislamu na watu wote.

  3. Je, umewahi kutoa jihudi zako za dhati kwa ajili ya Mwenyezi mungu? Jihesabu mwenyewe na kumbuka haki zake juu yako, ikiwa ni pamoja na kumuamini, kutomshirikisha na chochote, kumtii, kuitikia wito wa swala na mambo mengine, na kuwa na nia thabiti katika aliyoyaamrisha na kukataza, na kumpenda zaidi na kumnyenyekea. 

  4. Je, umewahi kutoa jihudi zako za dhati kwa ajili ya kitabu cha Mwenyezi Mungu? Jihesabu mwenyewe na kumbuka haki zake juu yako, ikiwemo: kukiamini, kukisoma mara kwa mara, kutafakari maana yake, kuwalingania watu ili kukiamini na kukisoma, na kukilinda dhidi ya wanao potosha maneno au maana zake, pia kukiheshimu kwa utakatifu wake, na kisishikwe ila na mtu msafi aliye toharika kutoka na uchafu mkubwa na mdogo na kwamba mtu asikiweke kitabu hicho sehemu isiyofaa[6].

  5. Je, umewahi kutoa jihudi zako za dhati kwa ajili ya Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu? Jihesabu mwenyewe na kumbuka haki zake juu yako, ikiwa ni pamoja na: kumuamini, kumtii katika yale aliyokuja nayo, kuacha kufanya ambayo hakuyafundisha, kuheshimu haki yake, kumuusia, kumuenzi, kumuunga mkono, kumnusuru, kuhuisha mwenendo wake katika kueneza ulinganizi wake, na kukanusha tuhuma katika kila analolisema na kulitamka [7] halikadhalika kuwaheshimu maswahaba zake, na kuwatukuza, na kuwapenda. Kwa sababu maswahaba wa mtu ndio wanaomsaidia na kumuhami.

  6. Je, hujudi ipi umeifanya kwa ajili ya Viongozi wa Waislamu, na Watawala na Wanachuoni, na hukumu yao kwako...? Ikiwa ni pamoja na: kuwatii kwa haki, kuwasaidia kwa masilahi ya dini na dunia, kuwakumbusha pale wanapoghafilika, na kuwaita kwa ajili ya nasaha, na kutowadanganya katika nasaha, au kuwasifia zaidi ya stahiki zao na kuwapongeza katika batili pale wanapo kuwepo[8]. 

  7. Je, umejitolea kwa ajili ya Waislamu wa kawaida? Ikiwa ni pamoja na: kuwaelekeza katika yale yenye maslahi kwao, na kuwasaidia katika mambo ya Dini yao na mambo yao ya kidunia kwa kauli na vitendo, na kuwazindua walioghafilika, na kuwaelimisha wajinga, na kutoa sadaka kwa masikini, na kusitiri madhambi yao, na kuwaondolea madhara, na kuleta manufaa. katika Dini na dunia, na kuwatakia kheri duniani na Akhera, na kuacha kuwaudhi, Na kuwatakia yale anayoitakia nafsi yake[9]. 

  8. Maana moja wapo ya nasaha ni kuwatahadharisha watu juu ya kosa wanalolifanya, ikiwa wanafanya baya watakemewa hatua kwa hatua kwa mujibu wa daraja za kuondoa makosa, na kwa kuzingatia maslahi, hata ikiwa ni kwa njia ya kushitaki kwa watawala, yote haya yamo katika kunasihiana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. na haya ni katika mafundisho ya Mtume (rehema na amani ziwe juu yake), na ni muongozo wa maswahaba zake, Mwenyezi Mungu awawie radhi.Na Katika nasaha ni mtu kunasihiwa kwa siri kwani mtu akinasihiwa mbele ya watu, huchukia. Kwa sababu hiyo, Al-Fudayl bin Iyad amesema: Muumini hustiri na kunasihi, na muovu hutukana na kudhalilisha[10].

  9. Kuwashauri wenye mamlaka na madaraka ni kwa kadiri ya uwezo, mtu akihisi kuwa hawezi kupata madhara yao ikiwa atajitokeza kuwashauri, basi awausie, na ikiwa atajihofia basi inatosha kuchukia tu moyoni mwake, na ikiwa anajua kuwa hawezi kuwashauri, basi asifanye mfano wa matendo yao, Kwani akifuata vitendo vyao atakuwa anawahadaa na kuwazidishia fitina, hata kufikia kukosa dini yake.

  10. Hekima ya mwenye kutoa nasaha kwa watu ni kutoa nasaha kwa njia ya fumbo, isipokuwa kwa wale wasioelewa mafumbo, na lisiwepo sharti la kukubaliwa nasaha hizo, bali mtu anapaswa kutekeleza wajibu wake katika kunasihi. Na endapo anaenasihiwa akifanyia kazi nasaha hizo alizopewa hilo ndio bora zaidi, na kama hatozifanyia kazi basi atapata malipo ya kumnasihi ndugu yake.

  11. Moja ya njia za nasaha: ni kubainisha Hadith sahihi na dhaifu, na kuwafafanulia wasimulizi wa hadith, na ni nani anayefaa kujifunza kwake na asiyefaa – na hiyo inafanyika kwa mwenye ujuzi na elimu hiyo-. Aliulizwa Ahmad bin Hanbal: Mtu anayefunga na kuswali na kujitenga ndio anapendeza kwako, au anaezungumza dhidi ya watu wanaozua katika dini? Akasema Imaam Ahmad: Akisimama na kuswali, na akafanya I’tikafu, matendo hayo ni kwa ajili yake mwenyewe, na ikiwa anazungumza na kubainisha watu wa uzushi, basi hii itakuwa ni kwa masilahi ya Waislamu.[11]  na hii ndiyo bora zaidi. hivyo basi Mlinganiaji na Mwanasheria- Mjuzi - wanapaswa kuzungumzia mambo haya kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu, akihesabu hilo katika kunasihi kwa ajili Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

  12. Jarir bin Abdullah (Mwenyezi Mungu awe radhi naye) alipokuwa akiuza bidhaa anamuonesha mnunuzi dosari za bidhaa hiyo, kisha akamhiyarisha kwa kusema: Ukitaka nunua, na ukipenda ondoka, siku moja akaambiwa: Ukifanya hivo si bidhaa zako hazitoisha? akasema: (Niliweka kiapo cha utii kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu juu ya kutoa nasaha kwa kila Muislamu[12] . Na Ushauri haukomei tu katika kutoa maoni na kuinusuru dini, lakini Ushauri unatakiwa katika mambo yote. Mfanyakazi ananasihiwa katika kazi yake ili kuifanya kwa ukamilifu, na mfanyabiashara ananasihiwa kuwafahamisha watu juu ya kasoro za bidhaa yake, na Daktari anashauriwa kukamilisha kazi yake na kutoa dawa kwa ufanisi hata kama bei iko chini, na mwanafunzi anashauriwa kutafuta Elimu na kuwasaidia ndugu zake katika elimu hiyo kwa manufaa yake na taifa lake na kadhalika.

  13.  Amesema Mshairi:Nipe nasaha kwa uhuru kabisa ninapokuwa peke yangu = wala usininasihi katika mkusanyiko wa watu.Kwaani kumnasihi mtu mbele ya watu ni aina ya lawama ambazo sipendi kuzisikiliza.Ikiwa mtakataa na kupinga maneno yangu = basi msifadhaike pale mtakapovunjiwa heshima.

Marejeo

  1. Tazama: “Alam Al-Hadith” cha Al-Khattabi (1/189), “"Almuealim Bifawayid Muslimin" ” Cha Al-Maziri (1/293).
  2. Tazama: “Kashf al-Mushakil kutoka kwa Hadith ya Sahih mbili” ya Ibn al-Jawzi (4/219), na “Riyad al-Afham fi Sharh Umdat al-Ahkam” cha al-Fakhani (1/346).
  3. Tazama: “Sharh Riyadh as-Salihin” cha Ibn Uthaymiyn (2/393).
  4. Imepokewa na Muslim No.: (56).
  5. Tazama: “Alam Al-Hadith” cha Al-Khattabi (1/191).
  6. Tazama: “Al-Mufhim” cha Al-Qurtubi (1/243), “Sharh Riyadh Al-Salihin” cha Ibn Uthaymiyn (2/388).
  7. “Alam Al-Hadith” (Ufafanuzi wa Sahih Al-Bukhari) cha Al-Khattabi (1/192).
  8. Tazama: “Alam al-Hadith” (Sharh Sahih al-Bukhari) cha al-Khattabi (1/193), ““Almafham Lima 'Ushakil Min Talkhis Kitab Muslimin"” cha al-Qurtubi (1/244).
  9. Tazama: “"'iikmal almuealim bifawayid muslimin"” cha Al-Qadi Iyad (1/307), “Al-Kawakib Al-Darari fi Sharh Sahih Al-Bukhari” cha Al-Karmani (1/218).
  10. Tazama jamie aleulum walhakmi" " cha Ibn Rajab al-Hanbali (1/225).
  11. Majmuu’ al-Fatawa” cha Ibn Taymiyyah (28/231).
  12. Tazama (Ufafanuzi wa Sahih Al-Bukhari cha Ibn Battal (1/131).


Miradi ya Hadithi