عَنْ أبِي هُريرةَ رضي الله عنه ، أنَّ رسولَ اللهِ ﷺ قَالَ: «مَنْ دَعَا إلى هُدًى، كان لهُ مِنَ الأَجْرِ مِثْلُ أجورِ مَنْ تَبِعهُ، لا يَنقُصُ ذلك مِنْ أجُورِهم شيئًا، ومَنْ دَعَا إِلَى ضَلالَةٍ، كان عليه مِنَ الإثمِ مثلُ آثامِ مَنْ تَبِعهُ، لا يَنْقُصُ ذلك مِنْ آثامِهم شَيئًا»

Kutoka kwa Abu Huraira, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, hakika Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam amesema:

1- “Mwenye kulingania kwenye uwongofu atapata ujira kama ujira wa wale wanaomfuata bila ya kuwapunguzia ujira wao hata kidogo. 2- Na anayelingania upotevu atapata dhambi sawa na dhambi za wale wanaomfuata bila ya kuwazuilia dhambi zao hata kidogo”  

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Mwenyezi Mungu amesema:

 “Ili wabebe mizigo yao kwa ukamilifu Siku ya Kiyama, na sehemu ya mizigo ya wale wanao wapoteza bila ya kujua. Angalia, ni maovu mno hayo wanayo yabeba”

[An-Nahl: 25]

Na akasema Mwenyezi Mungu mtukufu:

 “Na walio kufuru waliwaambia waumini : Fuateni njia yetu, nasi tutayabeba makosa yenu. Wala wao hawatabeba katika makosa yao chochote kile. Hakika hao ni waongo (12) Na hapana shaka wataibeba mizigo yao na mizigo mingine pamoja na mizigo yao. Na kwa yakini wataulizwa Siku ya Kiyama juu ya waliyo kuwa wakiyazua” .

[Al-Ankabut: 12, 13]

Amesema Allah mtukufu   :

“Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema, na akasema: Hakika mimi ni katika Waislamu” .

[Fussilat: 33]

Miradi ya Hadithi