عَنْ أبِي هُريرةَ رضي الله عنه ، أنَّ رسولَ اللهِ ﷺ قَالَ: «مَنْ دَعَا إلى هُدًى، كان لهُ مِنَ الأَجْرِ مِثْلُ أجورِ مَنْ تَبِعهُ، لا يَنقُصُ ذلك مِنْ أجُورِهم شيئًا، ومَنْ دَعَا إِلَى ضَلالَةٍ، كان عليه مِنَ الإثمِ مثلُ آثامِ مَنْ تَبِعهُ، لا يَنْقُصُ ذلك مِنْ آثامِهم شَيئًا»

Kutoka kwa Abu Huraira, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, hakika Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam amesema:

1- “Mwenye kulingania kwenye uwongofu atapata ujira kama ujira wa wale wanaomfuata bila ya kuwapunguzia ujira wao hata kidogo. 2- Na anayelingania upotevu atapata dhambi sawa na dhambi za wale wanaomfuata bila ya kuwazuilia dhambi zao hata kidogo”  

1-   Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam anahimiza juu ya kulingania kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kueneza hukumu za dini baina ya watu, na anawahimiza kufanya hivyo kwa kutaja malipo na fadhila za Walinganiaji. Atakayelingania katika sura zozote za kheri - iwe ni ibada kubwa au ndogo - atapata malipo sawa na wale wanaomfuata na kumuiga, bila ya malipo yao kupungua hata kidogo.

Na wito huo sio kusema tu, lakini pia inajumuisha matendo. Muislamu akifanya kitu katika Sunnah na wengine wakaifuata, atapata malipo ya kitendo chake na malipo sawa na wale wanaoifuata.

 2_ Na Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, anatahadharisha dhidi ya kuwapoteza watu na kuwapotosha, anayelingania ukafiri na ushirikina au uzushi na uongo au uasi, sawasawa wito wake ni wa maneno au kitendo, ana dhambi ya upotevu wake na sawa na dhambi ya wale wanaomfuata katika upotofu wake, na dhambi hii inayompata haipungui kutoka katika dhambi ya mfuasi hata kidogo, kwani kila mmoja wao ana mzigo wake uliokamilika.

Mwenyezi Mungu anasema:

“Ili wabebe mizigo yao kwa ukamilifu Siku ya Kiyama, na sehemu ya mizigo ya wale wanao wapoteza bila ya kujua. Angalia, ni maovu mno hayo wanayo yabeba”

[An-Nahl: 25]

, Na akasema Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam: “Haitauliwa nafsi kwa dhulma, lakini mtoto wa kwanza wa Adam ana dhamana ya damu yake, kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kuasisi jambo la kuua[1]”

Hadithi hii inathibitishwa na kauli yake Mtume, amani iwe juu yake: “Mwenye kutambulisha tabia njema katika Uislamu, basi atapata malipo yake, na pia malipo ya wale walioifuata baada yake, bila ya kupunguziwa malipo yao hata kidogo. Na anaye ingiza katika Uislamu mfano mbaya basi anabeba mzigo wake na mzigo wa walio tenda baada yake bila ya kuwapunguzia mizigo[2]”

Mafunzo

1-   Ukitaka kuzidisha amali zako, waite watu kwa Mwenyezi Mungu; Unapata ujira kama ujira wa wale wanaokufuata.

2-   Walinganiaji kwa Mwenyezi Mungu ni miongoni mwa watu wa sadaka inayoendelea kuongezeka hata baada ya kufa kwao na haikomi, basi jitahidi matendo yako mema yawe ni yenye kuendelea na uyasitishe maovu yako.

3-   Chukua hatua ya kuhuisha Sunnah ambazo Waislamu wengi walizipuuza. Kwa kuzihuisha, utapata radhi za Mwenyezi Mungu, na mapenzi ya Mtume Wake, Rehema na Amani zimshukie, na malipo ya wanaozifuata.

4-   Kueneza elimu ya Kiislamu ni njia mojawapo muhimu ya kuwaita watu kwa Mwenyezi Mungu. Kupitia humo, watu wanajua hukumu za dini yao, hivyo wanatii amri na wanajiepusha na makatazo.

5-   Jihadharini na matendo maovu yanayoendelea, kwani watu wangapi wamekufa na Malaika waliopewa dhamana ya kuandika bado wanaandika maovu yao! Waliwaita watu kwenye upotofu, ushirikina, uzushi na dhambi, na wengine wakawafuata.

6-   Mtu mwenye furaha ni yule atakaye kuwa kiongozi katika wema, na mtu duni na dhalili ni aliye kiongozi wa Motoni, kama alivyo sema

Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Na tukawafanya viongozi waitao Motoni”

[Al-Qasas: 41]

Marejeo

  1. Imepokewa na Al-Bukhari (3335) na Muslim (1677).
  2. Imepokewa na Muslim (1017).


Miradi ya Hadithi