عَنْ أبِي هُريرةَ رضي الله عنه ، أنَّ رسولَ اللهِ ﷺ قَالَ: «مَنْ دَعَا إلى هُدًى، كان لهُ مِنَ الأَجْرِ مِثْلُ أجورِ مَنْ تَبِعهُ، لا يَنقُصُ ذلك مِنْ أجُورِهم شيئًا، ومَنْ دَعَا إِلَى ضَلالَةٍ، كان عليه مِنَ الإثمِ مثلُ آثامِ مَنْ تَبِعهُ، لا يَنْقُصُ ذلك مِنْ آثامِهم شَيئًا»

Kutoka kwa Abu Huraira, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, hakika Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam amesema:

1- “Mwenye kulingania kwenye uwongofu atapata ujira kama ujira wa wale wanaomfuata bila ya kuwapunguzia ujira wao hata kidogo. 2- Na anayelingania upotevu atapata dhambi sawa na dhambi za wale wanaomfuata bila ya kuwazuilia dhambi zao hata kidogo”  

Muhtasari wa Maana

Walinganiaji kwa Mwenyezi Mungu wana malipo makubwa zaidi miongoni mwa watu. Kwakuwa Wanapokea ujira wao kikamilifu na kama ujira wa wale waliowafuata kwenye wito wao. Watetezi wa ufisadi na upotofu ndio watu wabaya zaidi. Wanabeba mizigo yao na mizigo ya wale wanaowafuata.

Miradi ya Hadithi