عن عمرِو بنِ العاصِ، أنه سَمِعَ رسولَ الله ﷺ يقول: «إذا حكَم الحاكمُ فاجتهدَ، ثم أصاب، فله أجرانِ، وإذا حكم فاجتَهدَ، ثم أخطأ، فله أجرٌ» متفق عليه.
عن عمرِو بنِ العاصِ، أنه سَمِعَ رسولَ الله ﷺ يقول: «إذا حكَم الحاكمُ فاجتهدَ، ثم أصاب، فله أجرانِ، وإذا حكم فاجتَهدَ، ثم أخطأ، فله أجرٌ» متفق عليه.
kutoka kwa Amru Ibun Al-a’swi (r.a), hakika yeye alimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani ziwe juu yake akisema:
1. “Atakapo hukumu hakimu na akajitahidi, kisha akapatia, basi anamalipo mara mbili.
2. Na atakapo hukumu na akajitahidi, kisha akakosea, basi anamalipo mara moja”
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu
" Na linapo wafikia jambo lolote lilio khusu amani au la kitisho wao hulitangaza. Na lau kuwa wangeli lipeleka kwa Mtume na kwa wenye mamlaka kati yao, wale wanao chunguza wangeli lijua ".
{An-Nisaa : 83}
" Wagonjwa, na wasio pata cha kutumia, maadamu wanamsafia niya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hapana njia ya kuwalaumu wanao fanya wema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu”.
{At-Tawba: 91}
" Na Daud na Suleiman walipo kata hukumu katika kadhiya ya konde walipo lisha humo mbuzi wa watu usiku. Na Sisi tulikuwa wenye kushuhudia hukumu yao hiyo". 78 Halikadhalika Mwenyezi Mungu mtukufu amesema: "Tukamfahamisha Suleiman. Na kila mmoja wao tulimpa hukumu na ilimu. Na tuliifanya milima na ndege kuwa pamoja na Daud imnyenyekee na imtakase Mwenyezi Mungu. Na Sisi ndio tulio fanya hayo ".
{Al-Anbiyaa 78 - 79}