عن عبد الله بنِ عمرَ رضي الله عنهما قال: أخَذَ رَسولُ اللهِ ﷺ بمَنْكِبِي، فَقالَ: «كُنْ في الدُّنْيا كَأنَّكَ غَرِيبٌ، أوْ عابِرُ سَبِيلٍ»، وكانَ ابنُ عُمَرَ يقولُ: «إذا أمْسَيْتَ فلا تَنْتَظِرِ الصَّباحَ، وإذا أصْبَحْتَ فلا تَنْتَظِرِ المَساءَ، وخُذْ مِن صِحَّتِكَ لِمَرَضِكَ، ومِنْ حَياتِكَ لِمَوْتِكَ».

Kutoka kwa Abdullah bin Umar, Allah amuwiye radhi, ambaye amesema:

1- Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alinishika bega na kusema: “Kuwa katika dunia hii kama kwamba wewe ni mgeni. 

2- Au mpita njia, 

3- Ibn Umar alikuwa akisema: “Ikifika jioni, usisubiri asubuhi, na ukiamka asubuhi, usisubiri jioni. 

4- Chukua kutoka kwenye afya yako yatakayo kunufaisha utakapo ugua, 

5- Na Chukua kutoka kwenye uhai wako yatakayo kufaa wakati wa kufa kwako”

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mola mlezi na Mtukufu:

“Na jitengezeeni zawadi. Na hakika bora ya zawadi ni uchamngu.”

[Al-Baqarah: 197]

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Na yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi, iliyo wekwa tayari kwa wachamngu”

[Al Imran: 133]

Mwenyezi Mungu anasema:

“Waache wale, na wastarehe, na iwadanganye tamaa. Watakuja jua”

[Al-Hijr: 3]

Pia Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:

“Mpaka yanapo mfikia mmoja wao mauti, husema: Mola wangu Mlezi! Nirudishe (99) Ili nitende mema sasa katika vile nilivyo viacha. Wapi! Hii ni kauli tu anayo isema ”

[Al- Mu’minun: 99, 100]

Pia Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:

“Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi, na iogopeni siku ambayo mzazi hatamfaa mwana, wala mwana hatamfaa mzazi kwa lolote. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli. Basi yasikudanganyeni maisha ya dunia, wala asikudanganyeni na Mwenyezi Mungu mdanganyifu ”

[Luqman: 33]

Akasema Tena Mola Mlezi:

“Jueni ya kwamba maisha ya dunia ni mchezo, na pumbao, na pambo, na kujifakhirisha baina yenu na kushindana kwa wingi wa mali na watoto. Mfano wake ni kama mvua ambayo huwafurahisha wakulima mimea yake, kisha hunyauka ukayaona yamepiga manjano kisha yakawa mabua. Na akhera kuna adhabu kali na maghfira kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi. Na maisha ya dunia si chochote ila ni starehe ya udanganyifu”

[Al-Hadid: 20]

Miradi ya Hadithi