36 - MWENYEZI MUNGU PEKEE NDIYE ANAYEJUA GHAIBU

عن عبد الله بنِ عمرَ رضي الله عنهما أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ ﷺ قَالَ:«مَفَاتِحُ الغَيْبِ خَمْسٌ لا يَعْلَمُهَا إِلَّا اللَّهُ:لا يَعْلَمُ مَا فِي غَدٍ إِلَّا اللَّهُ،وَلاَ يَعْلَمُ مَا تَغِيضُ الأَرْحَامُ إِلَّا اللَّهُ،وَلاَ يَعْلَمُ مَتَى يَأْتِي المَطَرُ أَحَدٌ إِلَّا اللَّهُ،وَلا تَدْرِي نَفْسٌ بِأَيِّ أَرْضٍ تَمُوتُ،وَلا يَعْلَمُ مَتَى تَقُومُ السَّاعَةُ إِلَّا اللَّهُ» 

Kutoka kwa Abdullah bin Umar, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani zimshukie) amesema:

1-    “Funguo za ghaibu ni tano anazozijua Mwenyezi Mungu pekee. 2.Mungu pekee ndiye anayejua kitakachotokea kesho. 3.Hakuna ajuaye kubadilisha matumbo ya uzazi isipokuwa Mwenyezi Mungu. 4.Hakuna ajuaye ni lini mvua itakuja ila Mwenyezi Mungu. 5.Na nafsi yoyote haijui itafia katika ardhi gani. 6.Hakuna ajuaye Qiyama itakuja lini ila Mwenyezi Mungu. 


Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Na ziko kwake funguo za ghaibu; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Yeye anajua kilioko nchi kavu na baharini. Na halidondoki jani ila analijua. Wala punje katika giza la ardhi, wala kibichi, wala kikavu ila kimo katika Kitabu kinacho bainisha”

[Al-An'am: 59].

Allah mtukufu pia amesema:

“Wanakuuliza muda wa kiyama itakuwa lini? Sema: Kujua muda wake, ujuzi huo uko kwa Mola Mlezi wangu. Hakuna yeyote aliye dhihirishiwa kutokea kwake isipo kuwa Yeye. Ni nzito katika mbingu na ardhi. Haikujieni ila kwa ghafla tu. Wanakuuliza kama kwamba wewe una pupa ya kuijua. Sema: Ujuzi wake uko kwa Mwenyezi Mungu. Lakini wengi katika watu hawajui” .

[Al-A'raf: 187]

Pia amesema mola mlezi aliye tukuka:

“Sema: Hapana katika mbingu na ardhi ajuaye ya ghaibu isipokuwa Mwenyezi Mungu. Wala wao hawajui lini watafufuliwa (65) Kwani huo ujuzi wao umefikilia kuijua Akhera? Bali wao wamo katika shaka nayo tu, bali wao kwa ujuzi nayo ni vipofu” .

[An-Namli: 65, 66]

Mwenyezi Mungu mlezi pia anasema:

“Hakika kuijua Saa ya Kiyama kuko kwa Mwenyezi Mungu. Na Yeye ndiye anaye iteremsha mvua. Na anavijua viliomo ndani ya matumbo ya uzazi. Na haijui nafsi yoyote itachuma nini kesho. Wala nafsi yoyote haijui itafia nchi gani. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua, Mwenye khabari” .

[Luqman: 34]

Na amesema mwenyezi majina yatukuzwe:

“Na ametukuka Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi na viliomo ndani yake. Na uko kwake ujuzi wa Saa ya Kiyama, na kwake Yeye mtarudishwa”

[Al-Zukhruf: 85].

Na amesema aliye tukuka kwa utukufu wake:

“Yeye ndiye Mwenye kujua ya siri, wala hamdhihirishii yeyote siri yake (26) Isipo kuwa Mtume wake aliye mridhia. Naye huyo humwekea walinzi mbele yake na nyuma yake” .

[Al-Jinn: 26, 27]

Miradi ya Hadithi