36 - MWENYEZI MUNGU PEKEE NDIYE ANAYEJUA GHAIBU

عن عبد الله بنِ عمرَ رضي الله عنهما أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ ﷺ قَالَ:«مَفَاتِحُ الغَيْبِ خَمْسٌ لا يَعْلَمُهَا إِلَّا اللَّهُ:لا يَعْلَمُ مَا فِي غَدٍ إِلَّا اللَّهُ،وَلاَ يَعْلَمُ مَا تَغِيضُ الأَرْحَامُ إِلَّا اللَّهُ،وَلاَ يَعْلَمُ مَتَى يَأْتِي المَطَرُ أَحَدٌ إِلَّا اللَّهُ،وَلا تَدْرِي نَفْسٌ بِأَيِّ أَرْضٍ تَمُوتُ،وَلا يَعْلَمُ مَتَى تَقُومُ السَّاعَةُ إِلَّا اللَّهُ» 

Kutoka kwa Abdullah bin Umar, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani zimshukie) amesema:

1-    “Funguo za ghaibu ni tano anazozijua Mwenyezi Mungu pekee. 2.Mungu pekee ndiye anayejua kitakachotokea kesho. 3.Hakuna ajuaye kubadilisha matumbo ya uzazi isipokuwa Mwenyezi Mungu. 4.Hakuna ajuaye ni lini mvua itakuja ila Mwenyezi Mungu. 5.Na nafsi yoyote haijui itafia katika ardhi gani. 6.Hakuna ajuaye Qiyama itakuja lini ila Mwenyezi Mungu. 


1- Amesema Mtume (Rehma na Amani zimshukie) kuwa Mwenyezi Mungu, Ametakasika na Amehodhi elimu ya mambo ya ghaibu ambayo ni Yeye tu ndiye anayeyajua;

Amesema mola mlezi aliye tukuka:

“Sema: Hapana katika mbingu na ardhi ajuaye ya ghaibu isipo kuwa Mwenyezi Mungu. Wala wao hawajui lini watafufuliwa”

[An-Namli: 65]

Na amesema aliye tukuka kwa utukufu wake:

. “Yeye ndiye Mwenye kujua ya siri, wala hamdhihirishii yeyote siri yake (26) Isipo kuwa Mtume wake aliye mridhia. Naye huyo humwekea walinzi mbele yake na nyuma yake” .

[Al-Jinn: 26, 27]

Na mambo yaliyotajwa katika Hadith sio pekee ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu ameyachagua kwa ajili ya elimu, bali huo ni mfano tu, na sio tu kwa kuyadhibiti hayo tu, au yaweza kuwa haya yaliyo tajwa katika hadithi ni mambo muhimu zaidi ambayo Mwenyezi Mungu ni wa pekee katika kujua. Vinginevyo, katika khabari za Mitume waliotangulia na watu wao ni habari ambazo Mwenyezi Mungu pekee ndiye anajua,

Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema:

“Je, hazikukufikieni khabari za walio kuwa kabla yenu, watu wa Nuhu, na A'di, na Thamud, na wale waliokuja baada yao? Hakuna yeyote anaye wajua isipokuwa Mwenyezi Mungu”

[Ibrahim: 9]

Na aliyoyaficha Mwenyezi Mungu kwa walimwengu wa majini na Malaika na khabari zao, na maajabu ya uumbaji wake katika mbingu na ardhi, na kadhalika. Na Mambo ya ghaibu kuhusiana na uwezekano wa kuyajua mwanadamu yamegawanyika katika sehemu mbili:

- Mojawapo: ni kile ambacho mtu anaweza kukipata na kukijua zaidi kwa kutumia njia na nyezo ambazo Mwenyezi Mungu amempa. Kama kujua nyakati za kuchomoza jua, nyakati za Sala, tarehe za kupatwa kwa jua, na mfano wa hayo, ni katika mambo ambayo Mwenyezi Mungu ameyawekea mfumo maalumu wa kimkakati.

- Na sehemu ambayo ni Mwenyezi Mungu pekee ndiye anayeijua, nayo ni ghaibu kabisa, ambayo inajumuisha mambo haya yaliyotajwa katika Hadith, ambayo yamo ndani ya maneno ya Mwenyezi Mungu:

Mwenyezi Mungu mlezi pia anasema:

“Hakika kuijua Saa ya Kiyama kuko kwa Mwenyezi Mungu. Na Yeye ndiye anaye iteremsha mvua. Na anavijua viliomo ndani ya matumbo ya uzazi. Na haijui nafsi yoyote itachuma nini kesho. Wala nafsi yoyote haijui itafia nchi gani. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua, Mwenye khabari” .

[Luqman: 34]

Mwenyezi Mungu aliyaita mambo haya kuwa ni Funguo kwa kufananisha tu. Kwani Mambo ambayo yamefichwa kwa mtu hayawezi kufikiwa isipokuwa kwa kutumia funguo zinazompeleka huko, sasa Ikiwa funguo zenyewe hazijulikani kwa mwanadamu yeyote, basi vipi kuhusu vile vitu vilivyofichwa?!

2. Jambo la kwanza: ni kile anachochuma mtu katika kesho yake ya karibu na ya mbali, basi mtu hajui ni riziki gani atakayoipata, au ni hatima gani itayomfikia kutokana na makadirio ya kheri na shari, na mtu hajui kesho yake ni wema kiasi gani au mabaya atakayo yatenda.

3. Jambo la pili ni kwamba Yeye, Utukufu ni Wake, anajua yaliyomo tumboni na yanayotokea ndani yake, na anayajua yanayopungua tumboni na ambayo hayajaumbwa, nayo ni kuharibika kwa mimba. Anajua kilichokamilika ndani yake na kukua kwake mpaka wakati wa kuzaliwa kwake, na anajua jinsia ya kijusi, akiwa mwanamume au mwanamke.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Mwenyezi Mungu anajua mimba anayobeba kila mwanamke, na yanayobadilika matumboni na yanayoongezeka, na kila kitu kiko kwake” .

[Al-Raad: 8]

Hii haipingani na kile kilichotokea hivi karibuni katika uwezo wa madaktari kujua jinsia ya mimba katika miezi yake ya mwisho. Haya yanatokana na Mwenyezi Mungu kuidhalilisha elimu na yaliyomo aridhini kwa waja wake; Sayansi ya kisasa haiwezi kugundua hili mpaka baada ya miezi minne kupita, na matokeo yake ni ya kubahatisha, ambayo kuna makosa mengi, na hawawezi kujua idadi ya miezi ya ujauzito katika kila mwanamke, ni saba au tisa. Kadhalika, ikiwa wangeweza kujua jinsia ya kijusi cha mwanamke mmoja, vipi kuhusu matumbo ya wanawake wote wa dunia na yule aliyewafundisha wote kwa wakati mmoja?! Utakatifu ni wake yeye Mwenyezi Mungu.

4. Jambo la tatu: Kujua wakati wa mvua. Hakuna mtu yeyote Duniani ajuaye ni lini mvua itanyesha, ni kiasi gani itanyesha au ni wapi itanyesha.

Na ikiwa wataalamu wa hali ya anga na wapiga nyota wanaweza kutabiri nyakati na maeneo ya mvua, basi hayo ni kutokana na kuona mawingu na anga, na sio kabla yake, na ni hali ambayo haikuwepo katika mataifa tokea zamani. Hata kama ni taifa lililoendelea, na haipingiki kwa watu kukosea Katika utabiri wao.

5. Jambo la nne: Kujua muda na mahali atakapofia mtu, Mwenyezi Mungu amesema:

“Na hakuna nafsi yoyote inayojua itafia katika ardhi gani”.

[Luqman: 34]

Mungu hakumwekea mwanadamu mpaka makhsusi, akiufikia basi atakufa, wala hakuweka sababu ya kujitenga nayo mpaka kufa; Mgonjwa anaponywa, mtu mwenye nguvu anakufa ghafla. Kijana anakumbwa na kifo, mzee anarudishwa kwenye umri wa udhalili sana, na mtu anarudi kwenye maeneo ya hatari, kwa hiyo anazama baharini au anaanguka kutoka mbali zaidi au mfano wahayo lakini anaendelea kuwa hai, na salama salama. Halafu anakuja kufa mtu ambaye katulia nyumbani kwake. 

6.Jambo la tano: Miongoni mwa mambo aliyofahamisha Mtume Rehma na Amani zimshukie katika hadithi ni kujua saa ya Qiyaamah; Hili ni jambo ambalo Mwenyezi Mungu amejichagulia Mwenyewe, na hakuna malaika wa karibu au Nabii aliyewahi kulijua.

Allah mtukufu pia amesema:

“Wanakuuliza muda wa kiyama itakuwa lini? Sema: Kujua muda wake, ujuzi huo uko kwa Mola Mlezi wangu. Hakuna yeyote aliye dhihirishiwa kutokea kwake ila Yeye. Ni nzito katika mbingu na ardhi. Haikujieni ila kwa ghafla tu. Wanakuuliza kama kwamba wewe una pupa ya kuijua. Sema: Ujuzi wake uko kwa Mwenyezi Mungu. Lakini wengi katika watu hawajui” .

[Al-A'raf: 187]

Na Jibril amani iwe juu yake, alimuuliza Mtume Muhammad Swalla Allaahu alayhi wa sallam: Lini kitasimama kiyama? Akasema: "Anayeulizwa juu ya kiyama si mjuzi zaidi kuliko anayeuliza." [1]

MAFUNDISHO

1. Amesema Mtume Rehema na Amani zimshukie baadhi ya mambo ambayo hakuna ajuaye chochote isipokuwa yeye Aliye tukuka. Haifai kwa Muislamu kuamini vinginevyo, au kuwaamini wajinga na makuhani wanaodai kuwa wanalijua hilo.

2. Iwapo Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye anayejua kitakachotokea kesho, basi inakupasa kufanya ibada na wala usilegee na kutegemea yale wanayoyafanya walaghai na waongo, na usiwe na tamaa ya kusikia au kuona kile kinachokusukuma kuacha ibada.

3. Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaficha waja wake elimu ya yatakayotokea siku zijazo. Basi jihadhari usije ukatumia kutaraji kuwa ni kisingizio katika yale uliyoyapuuza miongoni mwa yale ambayo ni wajibu kwako, au ukatenda katika yale yaliyoharamishwa,

basi utakuwa kama makafiri wanapo sema:

“Na washirikina wanasema: Mwenyezi Mungu angeli taka tusingeliabudu chochote badala yake, sisi wala baba zetu, wala tusingeli haramisha chochote bila ya Yeye.” .

[An-Nahl: 35]

4.  Iwapo mja anatamani riziki ya Mwenyezi Mungu, basi na arejee Kwake peke yake, kwani Yeye ndiye mpaji wa riziki.

5. Mwanamke kwenda kwa daktari kumwambia jinsia ya mtoto akiwa bado yuko tumboni na kadhalika hakusababishi madhara au katazo; Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu amewapa wataalamu ujuzi huo na kuwadhalilishia, na ujuzi wao unakomea katika kuyajua hayo baada ya kukamilika ukuaji wa kijusi katika tumbo la mama yake. Ama Kabla ya hapo, haiwezekani kujua uhalisia.

6. Ikiwa mvua ndio sababu ya riziki, hakuna awezaye kuidhibiti na hakuna ajuaye itanyesha lini, wala kiasi chake, wala mahali pake isipokuwa Mwenyezi Mungu. Basi fahamu kwamba riziki yako itakuwa kama alivyoipangilia Mwenyezi Mungu peke yake, endelea kuMuabudu  Yeye na umtegemee Yeye, na jitahidi kutafuta Aliyokuandikia.

7. Mwenyezi Mungu aliwaficha waja wake wakati na mahali pa kufa kwao; Kwani kama mtu angejua kwamba siku fulani atakufa, dunia ingeharibika na ardhi haitakaliwa na mtu, na mtu angeendelea kulia na kusubiri kifo chake hadi kimfikie. Kwa hiyo aliyaficha hayo ili tuwe na motisha ya kufanya kazi na kujenga upya ardhi. Haya yanatokana na hikima yake, ametakasika, ambaye hafanyi lolote isipokuwa kwa hekima inayojulikana kwa wanaoijua na hata isipojulikana.

8. Mwenyezi Mungu amewaficha waja wake tarehe ya Kiyama ili wawe katika kuitazamia daima, na wajiandae maishani mwao kwa matendo mema, na wapiganie muda wao uliobaki maishani mwao kwa kufanya ibada, ni kama alivyouficha usiku wa cheo na saa ya kujibiwa siku ya Ijumaa kwa hekima hiyo.

9. Kuamini mambo haya ya ghaibu na kusimama juu ya yale ambayo Ufunuo umetuambia ni utulivu wa akili na, na kueneza mipangokazi, na kuzidisha kushikamana na Mwenyezi Mungu na kumwamini.

10. Amesema Mshairi: Ewe mwenye kuwapa nafuu watu baada ya kukata tamaa = warehemu waja ambao wamenyoosha mikono kukuomba. Umewazoesha kuwapa riziki bila sababu = isipokuwa wanakuomba kwa kutaraji mazuri Umeahidi kutoa fadhila kwa furaha na karaha = kwa ukarimu na upole ikiwa watakuwa waadilifu.


Marejeo

  1.  Imepokewa na Al-Bukhari (50) na Muslim (9), kwa kutoka kwa Abu Hurairah

Miradi ya Hadithi