عن سفيانَ بنِ عبد الله الثقفيِّ قال: قلتُ: يا رسولَ الله، قل لي في الإسلام قولًا لا أسأل عنه أحدًا بعدكَ - وفي حديث أبي أسامة: غيرَك – قال: «قل: آمنتُ بالله، فاستقم».
عن سفيانَ بنِ عبد الله الثقفيِّ قال: قلتُ: يا رسولَ الله، قل لي في الإسلام قولًا لا أسأل عنه أحدًا بعدكَ - وفي حديث أبي أسامة: غيرَك – قال: «قل: آمنتُ بالله، فاستقم».
Kutoka kwa Sufyan bin Abdullah Al Thaqafi, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, amesema:
1- Nilisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu niambie kitu katika Uislamu ambacho sitamuuliza yeyote baada yako - na katika Hadithi ya Abu Usama: asiyekuwa wewe.
2- Akasema Mtume: “Sema: Nimemuamini Mwenyezi Mungu, kisha kuwa na msimamo”.
Mwenyezi Mungu aliyetukuka amesema:
“Sema: Hakika mimi ni mtu kama nyinyi; inafunuliwa kwangu ya kwamba Mola wenu ni Mola Mmoja tu. Basi nyookeni sawa kumwendea Yeye, na mumtake msamaha, na ole wao wanao mshirikisha” .
[Fussilat: 6]
Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
“Hakika walio sema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Kisha wakanyooka sawa, hao huwateremkia Malaika wakawaambia: Msiogope, wala msihuzunike; nanyi furahini kwa Pepo mliyo kuwa mkiahidiwa (30) Sisi ni vipenzi vyenu katika maisha ya dunia na katika Akhera, na humo mtapata kinacho tamaniwa na nafsi zenu, na humo mtapata mtakavyo vitaka”.
[Fussilat: 30, 31]