عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، قَالَ: «نَهَى رَسُولُ اللهِ ﷺ عَنْ بَيْعِ الْحَصَاةِ، وَعَنْ بَيْعِ الْغَرَرِ»

Kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye amesema:

1- “Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, amekataza kuuza kwa kutupa kokoto.  2. Na kuuza kwa udanganyifu”

Muhtasari wa Maana

Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam amekataza baadhi ya biashara ambayo inahusisha ulaghai au ujinga wa mmoja wa wahusika katika uuzaji bidhaa na bei, na hii ni pamoja na kwamba mnunuzi anarusha kokoto, na ikianguka juu ya kitu, lazima anunue, na miongoni mwao ni mauzo ambayo ndani yake kuna ujinga unaoharibu mkataba, kama kununua kitu kisichojulikana kwenye mfuko usiojulikana ni kitu gani kilichomo ndani yake.

Miradi ya Hadithi