عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، قَالَ: «نَهَى رَسُولُ اللهِ ﷺ عَنْ بَيْعِ الْحَصَاةِ، وَعَنْ بَيْعِ الْغَرَرِ»

Kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye amesema:

1- “Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, amekataza kuuza kwa kutupa kokoto.  2. Na kuuza kwa udanganyifu”

Kwa vile maisha ya watu yameegemea kwenye kununua na kuuza, kiasi ambacho maisha yao hayawezi kunyooka bila biashara, Uislamu umepanga kanuni za biashara, na kuifanya kuuza na kununua asili yake kuwa halali, isipokuwa ikipatikana dalili inayo haramisha biashara hiyo au kupatikana ujinga wa kutoijua bidhaa yenyewe au rushwa au kuingizwa kwake au ikiingiliwa na riba.

1. Miongoni mwa biashara ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu ameziharamisha ni kuuza au kununua kwa kutupa kokoto, ambao ulikuwa ni uuzaji wa kawaida katika zama za kabla ya Uislamu, na una namna nyingi; Ikiwa ni pamoja na kwamba muuzaji anasema: Nimekuuzia ardhi hii kutoka hapa mpaka kokoto litakapoishia, kisha anatupa kokoto, na aina nyingine ni kwamba kuuza au kununua hiyari yaoni kwa muda ambao kokoto halijanguka chini kutoka kwa mkono wa mnunuzi. Aina nyingine ni pamoja na kwamba anatupa kokoto kwenye  kundi la kondoo, na kondoo yeyote atakayepigwa na kokoto hiyo atauzwa kwa bei waliokubaliana, na aina nyingine ni  kushika kokoto na kusema: Kwa kila kokoto nina dirham kwa bidhaa hiyo. Na aina zingine ambazo zote ni miamala ya kibiashara isiyojulikana, tena yenye hatari, na ulaji wa pesa za watu kwa uwongo.
2. Biashara ya ulaghai pia ni haramu, nayo ni kila biashara ambao kinacho uzwa au kununuliwa hakijulikani, au haiwezekani kuikabidhi kwa mnunuzi. Kama vile kuuza samaki baharini, kuuza kijusi cha mnyama tumboni mwa mama yake, na kuuza maziwa kwenye Chuchu. Yote hayo ni udanganyifu ulioharamishwa kwa sababu ya ujinga uliomo. Idadi au ukubwa wa samaki haijulikani, na mtu anaweza kushindwa kumpata huyo samaki, na kijusi cha mnyama tumboni mwa mama yake hatujui ikiwa inatoka hai au imekufa, kamili au haijakamilika, na maziwa kwenye chuchu haijulikani kuwa na afya au kuharibiwa, na uzito wake haujulikani. Uuzaji wa kokoto ni aina ya uuzaji wa udanganyifu, lakini Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, aliubainisha kwa kuutaja kwa sababu ya kutokea mara kwa mara katika zama za kabla ya Uislamu. Pamoja na yote Sharia imeruhusu baadhi ya miamala ambayo kuna uwongo mdogo kwa sababu ya kuwepo haja hiyo. Ni uongo rahisi kama kumuuza kondoo akiwa na mtoto wake tumboni, na kumuuza na maziwa kwenye kiwele chake, na kama mtu kununua maji ya kunywa kwa dirham moja, kwa mfano, yenye mahitaji ya watu tofauti ya maji, mtu anaweza kunywa zaidi ya mtu mmoja. Kwa kuwa udanganyifu ulikuwa rahisi na watu katika mauzo hayo walikuwa na haja, hiyo inaruhusiwa [1]

MAFUNDISHO:

1- Muislamu awe na shauku ya kujua ni nini kinaruhusiwa na ni yapi yaliyo haramu katika biashara; Ili asije akaingia kwenye miamala haramu na kula pesa za watu bila ya haki.

2. iliyoharamishwa inayomtegemea mtu kurusha sarafu kwenye kitu maalum, na akiipiga anashinda, na akiikosa anapata hasara.

3.akikisha kwamba uuzaji na ununuzi wako ni halali kisheria; Kwa hiyo kitu kinajulikana, bei yake inajulikana, na muda wake - ikiwa sio mkono kwa mkono - unajulikana.

4. Biashara kiuhalisia wake ni jambo halali kisharia, isipokuwa uharamu unaweza kuhusiana na kuuza katika moja ya vitu vitatu: la kwanza: uharamu wa bidhaa, kama vile kuuza nyama iliyokufa, nguruwe, Pombe na kadhalika. ya pili: ni udanganyifu kutokana na kutojua kitu katika uuzaji au bei au kutoweza kukitoa, tatu: kuwepo kwa riba katika kuuza. Hakikisha kwamba ununuzi na uuzaji wako hauna mambo haya.

5. Miongoni mwa aina zilizoenea za uuzaji wa ulaghai: ni uuzaji wa bidhaa isiyoonekana, ambayo ni wakati mtu ananunua kitu ambacho hakukiona na hakupata sifa kamili ya bidhaa.

6. Moja ya aina za uuzaji wa ulaghai ni kwamba mtu ananunua kitu kisichojulikana; kama kununua nguo katika nguo nyingi lakini hajui ni ipi ameinunua, basi tu kulingangana kuishika pasina kupangilia chaguzi, yaani utakayo ishika ndio umenunua.

7. Moja ya aina zilizoenea kwa sasa ni kuuza ulaghai wa masanduku ya zawadi yasiyojulikana, ambayo ni wakati mtu ananunua sanduku kwa kiasi maalum, bila kujua kilicho ndani yake.

8. Miongoni mwa aina zilizoenea za uuzaji wa udanganyifu: ni mtoto hununua mfuko wenye zawadi ndani yake, bila kujua ni gani iliyomo ndani yake, na labda hakuna chochote ndani yake, na hiyo ndio inaitwa ni uongo.

9.  Moja ya njia maarufu za uuzaji wa udanganyifu ni kwamba mtu anauza mazao ya ardhi yake kwa miaka mingi ijayo.

10. Mshairi alisema:

Katika watu wapo ambao kawaida yao ni kudhulumu, na anaeneza maneno ya udhuru.

Huthubutu kula haramu na kudai = kuwa ana mzigo mzito wa kufanya hivyo.

Ewe unaye kula haramu hebu tuambie = uhalali wa kula haramu unaupata kitabu gani? Je, hukujua kwamba Mungu anajua kilichotokea? = na atahukumu kati ya waja siku ya kiyama.


Marejeo

1. Ufafanuzi wa Al-Nawawi katika kitabu cha sahihi Muslim (10/156)

Miradi ya Hadithi