عَنْ عَدِيِّ بْنِ حَاتِمٍ رضى الله عنه، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ «مَا مِنْكُمْ أَحَدٌ إِلَّا سَيُكَلِّمُهُ رَبُّهُ لَيْسَ بَيْنَهُ وَبَيْنَهُ تُرْجُمَانٌ، فَيَنْظُرُ أَيْمَنَ مِنْهُ فَلا يَرَى إِلَّا مَا قَدَّمَ مِنْ عَمَلِهِ، وَيَنْظُرُ أَشْأَمَ مِنْهُ فَلا يَرَى إِلَّا مَا قَدَّمَ، وَيَنْظُرُ بَيْنَ يَدَيْهِ فَلا يَرَى إِلَّا النَّارَ تِلْقَاءَ وَجْهِهِ، فَاتَّقُوا النَّارَ وَلَوْ بِشِقِّ تَمْرَةٍ، فَمَنْ لَمْ يَجِدْ، فَبِكَلِمَةٍ طَيِّبَةٍ».

Kutoka Kwa Adiy Ibn Hatim Mwenyezi Mungu awe radhi naye amesema:

Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehma na Amani ziwe juu yake amesema:"Hakuna yeyote kati yenu isipokuwa atazungumza na Mola wake, bila ya kuwepo mkalimani kati yao.Mwanadamu ataangalia upande wake wa kulia, hataona chochote isipokuwa matendo yake, na ataangalia upande wake wa kushoto, hataona chochote isipokuwa matendo yake, na atatizama mbele yake na hataona kitu isipokuwa moto.Jihadharini na moto, hata kwa kukitoa sadaka kipande cha tende.Basi asiyeipata atoe sadaka hata kwa neno jema”

  1. AnaelezeaMtume Rehma na Amani zimshukie kwamba hakuna yeyote isipokuwa atasimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi, na kuwajibishwa kwa yale aliyoyafanya, atasema naye bila ya mpatanishi wala mkalimani, bali kila mtu atakwenda kwa mola wake pasina mwombezi wa kumuombea wala kumtetea. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

    “Nanyi mlitujia wapweke kama tulivyo kuumbeni mara ya kwanza. Na mkayaacha nyuma yenu yote tuliyo kupeni, na wala hatuwaoni hao waombezi wenu, ambao mlidai kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu kwenu. Yamekatika mahusiano yenu, na yamekupoteeni mliyo kuwa mkidai.

    [Al-An'am: 94]. 

  2. Mja akisimama mbele ya Mola wake, hapati msaidizi wala mwombezi isipokuwa vitendo vyake. Atatafuta mtu wa kumuokoa kutokana na adhabu na kuhesabiwa; kwa sababu amesema Mtume rehma na Amani zimshukie:  “Yeyote atakaye ingia katika majadala wa kuhesabiwa ataangamia.”[1] Atatazama kuliani kwake na kushotoni kwake hataona chochote isipokuwa matendo yake, kisha anatazama mbele yake hataona isipokuwa moto. Sababu yake ni kwamba moto uko kwenye njia yake, na hawezi kuukwepa. Kwakuwa Ni lazima apite kwenye Sirat [2].

  3. Na ikiwa hii ndiyo hali ya mja Siku ya Qiyaamah, basi inafaa zaidi watu wachukue tahadhari kutokana na Moto ili kuepukana nao, hivyo atakuwa mwema na mbora zaidi, na mwanadamu anapaswa kuwa na shauku ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu nyakati zote, na kwamba asidharau chochote katika ibada. Katika matendo madogo ni Kutoa sadaka anachoweza, hata kama hiyo ni nusu ya tende.

  4. Na ikiwa huna chochote cha kutoa katika sadaka, basi neno jema linakutosheleza katika kumridhisha Mwenyezi Mungu, huenda likawa ni sababu ya kukuokoa kutokana na Moto.

Mafunzo

  1. Kumbuka kwamba umesimama mbele ya Mwenyezi Mungu peke yako, bila ya familia yako au marafiki pamoja nawe, na hauambatani na nasaba, fedha, au cheo. Basi jiandaeni mahali hapo:

    “Na kwa wanao ogopa kusimamishwa mbele ya Mola wao Mlezi watapata Bustani mbili”

    [Al-Rahman: 46].

  2. Usidharau matendo yoyote; iwe ni matendo mazuri au mabaya; Kwani milima mikubwa zaidi iliundwa kutokana na mlundikano wa changarawe na chembe za mchanga. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

    “Siku hiyo watu watatoka kwa mfarakano wakaonyweshwe vitendo vyao (6) Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona (7) Na anaye tenda chembe ya uovu atauona”

    [Al-Zalzalah: 6- 8].

  3. Moja ya matendo makubwa yanayomweka mtu mbali na Moto ni sadaka, ndio maana Mtume Rehema na Amani zimshukie akaamrisha katika Hadithi, na ndio maana Mola Mtukufu akasema:

    “Na toeni katika tulicho kupeni kabla hayajamfikia mmoja wenu mauti, tena hapo akasema: Mola wangu Mlezi! Huniakhirishi muda kidogo nipate kutoa sadaka, na niwe katika watu wema”.

    [Al Munafiqun: 10].;;

  4. Usichelewe kumpa masikini glasi ya maji, au kumtukuza Mwenyezi Mungu, au kusoma hata Aya, na usiseme: Ninajitayarisha ili nifanye zaidi ya hili, kwani maafa hutokea: alikuja ombaomba kwenye mlango wa Aisha, Mungu amuwie radhi, akamwambia kijakazi wake: “Mlishe.” Akaenda kijakazi, kisha akarudi, na akamwambia Aisha: “Sijapata chochote cha kumlisha.” Akasema: “Rudi ukamtafutie chochote,” basi akarudi yule kijakazi na Akapata tende akaileta Aisha akasema. : "Mpe hiyo tende, kwani ndani yake mna uzito wa atomu, ikiwa itakubaliwa" [3]

  5. Je, ni wingi ulioje wa matendo mema yanayilingana na kipande cha tende au zaidi yake, kama vile kuwafurahisha wazazi na jamaa kwa mazungumzo au kuwahudumia, ikiwemo kumbebea kikongwe mizigo yake au kumsaidia mtu dhaifu, kumvisha nguo masikini, na kuwajali wajane au yatima, Amesema Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam: “Usidharau kitu chochote cha kheri, hata kukutana na ndugu yako kwa uso wa furaha.” [4].

  6. Ulimi unaweza kuwa sababu ya kumpeleka mja kwenye pepo ya milele, au unampeleka kwenye moto wa Jahannamu, mafikio ya mtu yanategemea ulimi wake, Ulimi unaweza kuwa sababu ya kuokoka kwake au kuangamia kwake.

  7. Keti na familia yako na wanafunzi, na mtafakari juu ya matendo mema ambayo mnaweza kufanya bila shida, basi mhamasishane kila mmoja juu ya kuyatenda.

  8. Mshairi amesema:

Wekeza mema katika ulimwengu wako na ujitahidi = na usijali mabaya na wivu

Fanya vizuri kwa ajili ya siku ambayo watu wote wanaingoja = ndani yake kuna hukumu ya Mwenyezi Mungu mmoja.

Matendo yako ndio yanakubainishia ni makazi gani utafikia = bustani za mbinguni au moto wa kaburini.

Marejeo

  1. Al-Bukhari (4939) na Muslim (2876).
  2. Fath al-Bari, Sharh Sahih al-Bukhari, cha Ibn Hajar (11/404).
  3. Al-Bayhaqi katika “shua`bul Imani” (3190).
  4. Muslim (2626).


Miradi ya Hadithi