عَنْ عَدِيِّ بْنِ حَاتِمٍ رضى الله عنه، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ «مَا مِنْكُمْ أَحَدٌ إِلَّا سَيُكَلِّمُهُ رَبُّهُ لَيْسَ بَيْنَهُ وَبَيْنَهُ تُرْجُمَانٌ، فَيَنْظُرُ أَيْمَنَ مِنْهُ فَلا يَرَى إِلَّا مَا قَدَّمَ مِنْ عَمَلِهِ، وَيَنْظُرُ أَشْأَمَ مِنْهُ فَلا يَرَى إِلَّا مَا قَدَّمَ، وَيَنْظُرُ بَيْنَ يَدَيْهِ فَلا يَرَى إِلَّا النَّارَ تِلْقَاءَ وَجْهِهِ، فَاتَّقُوا النَّارَ وَلَوْ بِشِقِّ تَمْرَةٍ، فَمَنْ لَمْ يَجِدْ، فَبِكَلِمَةٍ طَيِّبَةٍ».

Kutoka Kwa Adiy Ibn Hatim Mwenyezi Mungu awe radhi naye amesema:

Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehma na Amani ziwe juu yake amesema:"Hakuna yeyote kati yenu isipokuwa atazungumza na Mola wake, bila ya kuwepo mkalimani kati yao.Mwanadamu ataangalia upande wake wa kulia, hataona chochote isipokuwa matendo yake, na ataangalia upande wake wa kushoto, hataona chochote isipokuwa matendo yake, na atatizama mbele yake na hataona kitu isipokuwa moto.Jihadharini na moto, hata kwa kukitoa sadaka kipande cha tende.Basi asiyeipata atoe sadaka hata kwa neno jema”

Adiy bin Hatim bin Abdullah

Ni: Abu Tarif, Adiy bin Hatim bin Abdullah bin Saad Al-Ta'i Mwenyezi Mungu awe radhi naye. Baba yake Hatem alijulikana na kuwa maarufu kwa ukarimu wake, Adiy alikuwa Mkristo, akaja kwa Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, na kuziona sifa zake, kisha akasilimu mwaka wa 9 au 10 Hijiria. Na alipofariki Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehma na amani ziwe juu yake) alikuja kwa Abu Bakr al-Siddiq Mwenyezi Mungu awe radhi naye wakati wa kuritadi akiwa na zaka za watu wake, na akashikamana na Uislamu na hakuritadi. na watu wake walithibiti pamoja naye, alishuhudia ufunguzi wa mji wa Iraq. Alifariki katika mji wa Kufa mwaka wa 67 Hijiria, akiwa na umri wa miaka mia moja na ishirini [1].

Marejeo

  1. Unaweza kurejea historia yake katika kitabu: “Maarifaat al-Sahaba” cha Abu Nu’aym (4/1846), “"Al istie`ab Fi Maarifat Al'as-habi”” cha Ibn Abd al-Bar (4/1770), “Asad al-Ghaba” cha Ibn Al-Atheer (3/357), “"Al'iisabat Fi Tamayuz Alswahabati"” cha Ibn Hajar Al-Asqalani (4/267).


Miradi ya Hadithi