عن جَابِر بن عبد الله رضي الله عنهما قال: سَمِعْتُ النَّبِيَّ ﷺ يَقُولُ: «بَيْنَ الرَّجُلِ وَبَيْنَ الشِّرْكِ وَالْكُفْرِ تَرْكُ الصَّلَاةِ»

kutoka kwa Jabir bin Abdillah, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, amesema:

“Nimemsikia Mtume Rehema na Amani zimshukie akisema: “Baina ya mtu na ushirikina na ukafiri ni kuacha Swalah” .

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu

238." Zilindeni Sala, na khasa Sala ya katikati, na simameni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu nanyi ni wenye kuqunuti (kunyenyekea). "

[Al-Baqarah: 238]

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu

"Kila nafsi itafungika (Motoni) kwa (amali mbovu) ilizozichuma 39. ~sipokuwa watu wa kuliani (watu wa kheri) 40. (Hao watakuwa) katika Mabustani, wakiulizana 41 . Juu ya watu wabaya ( wawaambie): 42. "Ni kipi kilichokupelekeni Motoni? 43· Watasema: "Hatukuwa miongoni mwa waliokuwa wakisali "

[Al-Muddathir: 38-43]

Miradi ya Hadithi