عن جَابِر بن عبد الله رضي الله عنهما قال: سَمِعْتُ النَّبِيَّ ﷺ يَقُولُ: «بَيْنَ الرَّجُلِ وَبَيْنَ الشِّرْكِ وَالْكُفْرِ تَرْكُ الصَّلَاةِ»

kutoka kwa Jabir bin Abdillah, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, amesema:

“Nimemsikia Mtume Rehema na Amani zimshukie akisema: “Baina ya mtu na ushirikina na ukafiri ni kuacha Swalah” .

Swala ni nguzo ya pili katika nguzo za Uislamu baada ya shahada mbili, nayo ni nguzo ya Uislamu ambayo juu yake uislamu umejengwa.

Amesema Mtume (saw) :

“Kichwa cha mambo –yote- ni Uislamu, na nguzo yake ni Swala, na kilele chake ni jihadi” [1]

 na swala ni kitendo  kinachopendwa zaidi na Mwenyezi Mungu

imesimuliwa Kutoka kwa Abdullah bin Masoud, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, amesema:

Nilimuuliza Mtume (saw) : Ni amali gani anayoipenda zaidi Mwenyezi Mungu? Akasema: “ni kuswali swala katika wakati wake” .[2]


Ndio maana sala ilikuwa alama ya kutofautisha Waislamu. kwani mnafiki inakuwa nzito kwake,

wala haitekelezi ila kama alivyosema Mwenyezi Mungu:

{Hakika wanaafiki wanamhadaa Mwenyezi Mungu, naye anawahadaa, na wanaposimama kuswali husimama wakiwa wavivu}.

[An-Nisaa: 142]


Na kafiri hukanusha uwajibu wake na kuiacha moja kwa moja, na ndio maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akaahidi adhabu kali kwa mwenye kuacha swala, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu.

"Kila nafsi itafungika (Motoni) kwa (amali mbovu) ilizozichuma 39. isipokuwa watu wa kuliani (watu wa kheri) 40. (Hao watakuwa) katika Mabustani, wakiulizana 41 . Juu ya watu wabaya ( wawaambie): 42. "Ni kipi kilichokupelekeni Motoni? 43· Watasema: "Hatukuwa miongoni mwa waliokuwa wakisali ". 

[Al-Muddathir: 38-43]

Na Mwenyezi Mungu alisema kuhusu moto huo wa saqari:

“Nitakuja mtia kwenye Moto wa Saqar: “Na nini kitakujuulisha ni nini huo Moto wa Saqar?27  .Haubakishi wala hausazi. 28.Unababua ngozi iwe nyeusi. 29.Juu yake wapo kumi na tisa. 30."

[Al-Muddathir: 26-30]


Katika Hadithi hii, Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) ametueleza juu ya hukumu ya kupuuza Swalah, na kubainisha kuwa ni kitengenishi baina ya Muislamu na kafiri. “Baina ya mtu na ushirikina na ukafiri ni kuacha Swala ”.  Na hii inafanana na kauli yake aliposema “Ahadi iliyo baina yetu na wao ni Swala, basi mwenye kuiacha amekufuru.”[3]  Na Umar akasema: “Hakuna nafasi katika Uislamu kwa mtu anayepuuza Swala) [4]. Na Abdullah bin Shaqiq, Mwenyezi Mungu amrehemu, alikuwa akisema: “Maswahaba wa Muhammad (saw), hawakuona matendo yoyote kuwa ukafiri kama  kuacha swala”. [5]

MAFUNDISHO

1. wanawazuoni wameafikiana kwa kauli moja kwamba mwenye kuacha Swalah kwa kukanusha wajibu wake basi huyo ni kafiri na ameritadi, na wamekhitalifiana kuhusu mwenye kuiacha kwa uvivu na uzembe. Kuna waliosema kuwa ni: kafiri, na wengine wakasema: huyo ni fasiqi-muovui alinganiwe kutubia, la sivyo atauawa, na ikasemwa kuwa: ni fasiqi asiuawe. Na Mwislamu wa kweli anayemjua Mola wake Mtukufu na kumuamini Mtume Wake, (saw), hawi katika nafasi ambayo wanazuoni wamehitilafiana baina ya kumkufurisha na ufasiq, bali atafanya haraka kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuwa karibu nae kwa kutenda matendo ya juu zaidi baada ya kutekeleza wajibu.


2. Omar Ibn Al-Khattab alipochomwa mkuki ambao ilikuwa sababu ya kifo chake, na maswahaba walimuingiza nyumbani kwake, wakajaribu kumuamsha kutoka katika kuzimia kwake ikashindikana, wakasema: Swala pekee ndiyo itamuamsha, wakaita: Swala! Ewe Amirul-Muuminin! Akasema: “Ndio, na hakuna sehemu katika Uislamu kwa mwenye kupuuza Swala.” Akaswali huku damu ikichuruzika kutoka kwenye Jeraha Lake. Je! Maswahaba walikuwa na hamu ya kuswali kwa kadiri gani? [6]


3.

Imesimuliwa kutoka kwa Abdillsh bin A`mru bin al aswii, Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kutoka kwa Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) kwamba siku moja alitaja swala na kusema:

" mwenye kuhifadhi swala atakuwa na nuru na hoja – utetezi- na kuokoka siku ya kiamah, na asiyehifadhi swala hatakuwa na nuru wala hoja – utetezi- wala kuokoka, na siku ya kiamah atakuwa pamoja na Qaruun na Fir`Aun na Haaman na Ubai Bin Khalaf.)  [7]"


Ibn al-Qayyim, Mwenyezi Mungu amrehemu, amesema: “katika hadithi hii Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) amewataja watu hawa wanne, kwa sababu ni vingozi wakuu wa makafiri. Na hapa kuna nukta muhimu, nayo ni kwamba mwenye kuacha kuhifadhi swala, ima anashughulishwa na mali, au ufalme, au uongozi, au biashara, hivyo basi atakueshughulishwa na mali yake na akaacha kuswali basi siku ya kiama atakuwa pamoja na Firauni, na atakaeshughulishwa na uongozi na utumishi akaacha kuswali basi atakuwa pamoja na Haman, na atakueshughulishwa na biashara yake akaacha kuswali basi atakuwa pamoja na Ubay bin Khalaf” [8]


4. Vipi mtu anaacha Swala hali ya kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ameifanya ni kafara ya dhambi na maovu ya mja?!

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani ziwe juu yake):

“Je, mmeona lau kuna mto katika mlango wa mmoja wenu, akawa akioga ndani yake kila siku mara tano je atabakiwa na uchafu wowote?” maswahaba Wakasema: "Haitabaki chochote katika uchafu wake." Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) Akasema: huo ndio mfano wa Swalah tano, Mwenyezi Mungu hufuta dhambi kupita swalah  .[9]"


5. Ibn Masoud, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, amesema kuhusiana na swala ya jamaa: “na hakika Mwenye kuacha swala tulikuwa tukimuona kuwa ni mnafiki wa wazi, na hakika mtu alikuwa akiletwa kwa kukokotwa/ kubebwa na watu wawili kisha anasimimishwa kwenye safu- ili aswali jamaa-. ”[10]

6. Mshairi alisema:
uwito wa sala juu ya minara = katika majira ya alfajiri ya asubuhi na usiku utulivu
ni uwito unaoleta uhai kwa ulimwenguni=,kwa wakazi wa vijijini na mijini
Na ni mwito kutoka mbinguni kwenda duniani = kwa walio juu ya ardhi na ndani
Na ni mkutano baina ya Malaika na imaani = na Waumini bila ya idhini
Na ni sababu ya kuelekea katika kufaulu, na kwa kheri =  kisha na haki,  na uwongofu, na wema.


7. mwingine alisema:
mja mwema  huisahau dunia yake kwa kuidharau = na kuona wazi uhalisia  wa nafsi yake 
mbavu za waja wema huachana na vitanda vyao, = na kumaliza  usiku wao wakiwa wamesimama kuswali na kusujudu.
Katika usiku wa kiza huiendea swala, wakichochewa na= shauku kwa mwenye nguvu na vilema.
Wanasoma Aya za Mwenyezi Mungu katika mihrab yake =  hadi  alfajiri inakaribia kuingia
mpaka adhana inapoadhiniwa  = huelekea kwa Mwenyezi Mungu mola wao.
Je umewahi kuona raha inayokuwepo wakati umesimama= mbele ya mola wako kwa unyenyekevu na heshima?!
Na uliwahi kuona waja wema wakiwa katika safu moja kwa unyeyekavu, = na wanavyotoa salamu?!

المراجع

  1. mepokewa na Al-Tirmidhiy (2616) na Al-Nasa’i (11330).
  2. Imepokewa na Al-Bukhari (527) na Muslim (85).
  3. Imepokewa na Al-Tirmidhiy (2621), Al-Nasa’i (463) na Ibn Majah (1079).
  4. Imesimuliwa na Malik katika Al-Muwatta (1/39) na Al-Daraqutni (1750).
  5. Imepokewa na Al-Tirmidhiy (2622).
  6. Imesimuliwa na Malik katika Al-Muwatta (1/39) na Al-Daraqutni (1750).
  7. Imepokewa na Ahmad (6576), na Shuaib Al-Arna`ut amesema: sanad yake ya upokezaji ni hasan.
  8. “Swala na Hukumu za mwenye kuiacha” cha Ibn Al-Qayyim (uk. 51).
  9. Imepokewa na Al-Bukhari (528) na Muslim (667).
  10. Imepokewa na Muslim (654).


Miradi ya Hadithi