عَنْ عُبَادَةَ بْنِ الصَّامِتِ قَالَ: بَايَعْتُ رَسُولَ اللَّهِ ﷺ فِي رَهْطٍ، فَقَالَ: «أُبَايِعُكُمْ عَلَى أَنْ لا تُشْرِكُوا بِاللَّهِ شَيْئًا، وَلا تَسْرِقُوا، وَلا تَزْنُوا، وَلا تَقْتُلُوا أَوْلاَدَكُمْ، وَلا تَأْتُوا بِبُهْتَانٍ تَفْتَرُونَهُ بَيْنَ أَيْدِيكُمْ وَأَرْجُلِكُمْ، وَلا تَعْصُونِي فِي مَعْرُوفٍ، فَمَنْ وَفَى مِنْكُمْ فَأَجْرُهُ عَلَى اللَّهِ، وَمَنْ أَصَابَ مِنْ ذَلِكَ شَيْئًا فَأُخِذَ بِهِ فِي الدُّنْيَا، فَهُوَ كَفَّارَةٌ لَهُ وَطَهُورٌ، وَمَنْ سَتَرَهُ اللَّهُ فَذَلِكَ إِلَى اللَّهِ؛ إِنْ شَاءَ عَذَّبَهُ، وَإِنْ شَاءَ غَفَرَ لَهُ».

Kutoka kwa Ubaada bin As-Samit, Mwenyezi Mungu awe radhi naye amesema:

1- Niliweka kiapo cha utii kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimshukie, nikiwa katika kundi, na akasema: “Naweka kiapo cha utii kwenu kwa sharti kwamba msimshirikishe Mwenyezi Mungu na kitu chochote, msiibe, msizini, msiwaue watoto wenu. Wala msije na uwongo mnao uzua baina ya mikono yenu na miguu yenu, wala msiniasi kwa wema. 2- Na atakaye tekeleza hayo miongoni mwenu, basi ujira wake uko kwa Mwenyezi Mungu, na likimpata lolote katika hayo basi nitamuhukumu hapahapa duniani. Kufanya hivyo ndio kafara yake na inamtakasa. Na yeyote ambaye Mwenyezi Mungu atamfichia siri, basi hukumu yake ni kwa Mwenyezi Mungu. Akitaka atamuadhibu, na akipenda atamsamehe”  

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mtukufu:

“Sema: Njooni nikusomeeni aliyo kuharimishieni Mola wenu Mlezi. Nayo ni kuwa, msimshirikishe Yeye na chochote. Na wazazi wenu wafanyieni wema. Wala msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya umasikini. Sisi tunakuruzukuni nyinyi na wao. Wala msikaribie mambo machafu, yanayo onekana, na yanayo fichikana. Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharimisha kuiuwa, ila ikiwa kwa haki. Hayo amekuusieni ili myatie akilini” .

[Al-An’am: 151]

Miradi ya Hadithi