عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الخُدْرِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ ﷺ لِأَصْحَابِهِ: «أَيَعْجِزُ أَحَدُكُمْ أَنْ يَقْرَأَ ثُلُثَ القُرْآنِ فِي لَيْلَةٍ؟» فَشَقَّ ذَلِكَ عَلَيْهِمْ وَقَالُوا: أَيُّنَا يُطِيقُ ذَلِكَ يَا رَسُولَ اللهِ؟ فَقَالَ: «اللهُ الوَاحِدُ الصَّمَدُ ثُلُثُ القُرْآنِ».

Kutoka kwa Abu Said Al-Khudri, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema: Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, aliwaambia maswahaba zake:

1- Je, mmoja wenu anashindwa kusoma theluthi ya Qur-aan katika usiku mmoja? 

2- ikawa ngumu kwao, wakasema: Ni nani anaweza kufanya hivyo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? 

3- Akasema: “Qul Huwa Allah ahd, Allah Alssamad (yaani suratul ikhlaas yenye maana ya) Mwenyezi Mungu ni Mmoja, Mwenyezi Mungu ndio Mkusudiwa.) ni theluthi ya Qur’ani. 

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu: 

 Ishara yoyote tunayo ifuta au tunayo isahaulisha tunailetea iliyo bora kuliko hiyo, au iliyo mfano wake.

[Al-Baqarah: 106]

Amesema Mwenyezi Mungu: 

1. Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee.  2. Mwenyezi Mungu Mkusudiwa.  3. Hakuzaa wala hakuzaliwa  4. Wala hana anaye fanana naye hata mmoja. 

Miradi ya Hadithi