عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الخُدْرِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ ﷺ لِأَصْحَابِهِ: «أَيَعْجِزُ أَحَدُكُمْ أَنْ يَقْرَأَ ثُلُثَ القُرْآنِ فِي لَيْلَةٍ؟» فَشَقَّ ذَلِكَ عَلَيْهِمْ وَقَالُوا: أَيُّنَا يُطِيقُ ذَلِكَ يَا رَسُولَ اللهِ؟ فَقَالَ: «اللهُ الوَاحِدُ الصَّمَدُ ثُلُثُ القُرْآنِ».

Kutoka kwa Abu Said Al-Khudri, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema: Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, aliwaambia maswahaba zake:

1- Je, mmoja wenu anashindwa kusoma theluthi ya Qur-aan katika usiku mmoja? 

2- ikawa ngumu kwao, wakasema: Ni nani anaweza kufanya hivyo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? 

3- Akasema: “Qul Huwa Allah ahd, Allah Alssamad (yaani suratul ikhlaas yenye maana ya) Mwenyezi Mungu ni Mmoja, Mwenyezi Mungu ndio Mkusudiwa.) ni theluthi ya Qur’ani. 

Saad bin Malik bin Sinan Al-Ansari Al-Khazraji Al-Madani

Jina lake ni Abu Saeed, Saad bin Malik bin Sinan Al-Ansari Al-Khazraji Al-Madani, Al-Khudri, alishiriki katika vita ya handaki na vilivyokuja baada yake, na alitaka kushiriki vita vya uhdi Mtume akamkata-lia kwa sababu ya umri wake mdogo, na alishiriki Pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake vita kumi na mbili, na alishiriki pia katika kiapo cha utii chini ya mti, na alisimulia hadith nyingi, na aliwahi kuwa mufti kwa muda, alifariki mwaka wa 74 hijiri

Miradi ya Hadithi