عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: (سَبْعَةٌ يُظِلُّهُمُ اللهُ فِي ظِلِّهِ يَوْمَ لَا ظِلَّ إلَّا ظِلُّهُ: الْإِمَامُ الْعَادِلُ، وَشَابٌّ نَشَأَ بِعِبَادَةِ اللهِ عز وجل، وَرَجُلٌ قَلْبُهُ مُعَلَّقٌ فِي الْمَسَاجِدِ، وَرَجُلَانِ تَحَابَّا فِي اللهِ؛ اجْتَمَعَا عَلَيْهِ، وَتَفَرَّقَا عَلَيْهِ، وَرَجُلٌ دَعَتْهُ امْرَأَةٌ ذَاتُ مَنْصِبٍ وَجَمَالٍ، فَقَالَ: إِنِّي أَخَافُ اللهَ، وَرَجُلٌ تَصَدَّقَ بِصَدَقَةٍ، فَأَخْفَاهَا حَتَّى لَا تَعْلَمَ يَمِينُهُ مَا تُنْفِقُ شِمَالُهُ، وَرَجُلٌ ذَكَرَ اللهَ خَالِيًا فَفَاضَتْ عَيْنَاهُ.

Kwa kutoka kwa Abu Hurairah Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kutoka kwa Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam amesema: 1- “Watu aina saba Mwenyezi Mungu atawatia kwenye kivuli chake siku ambayo hakuna kivuli ila chake. 2- Imamu Muadilifu 3- Kijana aliyekulia katika ibada ya Mwenyezi Mungu. 4- Mtu ambaye moyo wake umefungamana na misikiti. 5- Watu wawili waliopendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. wakakusanyika kwa ajili yake na kutawanyika kwa ajili yake. 6- Mwanaume aliyekaribishwa na mwanamke mwenye cheo na mrembo, akasema: Mimi namuogopa Mwenyezi Mungu. 7- Mtu aliyetoa sadaka na akaificha mpaka mkono wake wa kushoto usijue mkono wake wa kulia unatoa nini. 8- Na mtu aliye mtaja Mwenyezi Mungu kwa siri, mpaka akalia”.


Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi mtukufu:

“Mkizidhihirisha sadaka ni vizuri; na mkizificha mkawapa mafakiri kwa siri basi hivyo ni kheri kwenu, na yatakuondoleeni baadhi ya maovu yenu. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda”

[Al-Baqara: 271]. 

Na amesema Mwenyezi mtukufu:

“Na Wanapo Sikia yaliyo teremshwa kwa Mtume utaona macho yao yanachururika machozi kwa sababu ya Haki waliyo itambua. Wanasema: Mola wetu Mlezi! Tumeamini. Basi tuandike pamoja na wanao shuhudia”.

[Al-Ma’ida: 83]

Na akasema Mwenyezi Mungu mtukufu:

“wao walikuwa ni vijana walio muamini Mola wao Mlezi. Na Sisi tukawazidisha uwongofu” .

[Al-Kahf: 13]

Na akasema Mwenyezi mtukufu:

  “Katika Nyumba ambazo Mwenyezi Mungu ameamrisha zitukuzwe, na humo litajwe jina lake, wanamtakasa humo asubuhi na jioni (36) Watu ambao biashara wala kuuza hakuwashughulishi na kumdhukuru Mwenyezi Mungu, na kusimamisha Sala, na kutoa Zaka. Wanaikhofu Siku ambayo nyoyo na macho yatageuka” . 

[An-Nur: 36-37]

Na akasema Mwenyezi Mungu mtukufu:

“Na ama yule anaye ogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi, na akajizuilia nafsi yake na matamanio (40) Basi huyo, Pepo itakuwa ndiyo makaazi yake!” .

[Al-Nazi’at: 40, 41]


Miradi ya Hadithi