عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ «مَنْ كَانَتْ لَهُ مَظْلِمَةٌ لِأَخِيهِ مِنْ عِرْضِهِ أَوْ شَيْءٍ، فَلْيَتَحَلَّلْهُ مِنْهُ اليَوْمَ، قَبْلَ أَنْ لاَ يَكُونَ دِينَارٌ وَلاَ دِرْهَمٌ، إِنْ كَانَ لَهُ عَمَلٌ صَالِحٌ، أُخِذَ مِنْهُ بِقَدْرِ مَظْلِمَتِهِ، وَإِنْ لَمْ تَكُنْ لَهُ حَسَنَاتٌ، أُخِذَ مِنْ سَيِّئَاتِ صَاحِبِهِ، فَحُمِلَ عَلَيْهِ».

Kutoka kwa Abu Hurayra, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimshukie.

1- “Atakayekuwa na dhulma kwa ndugu yake, heshima yake au kitu chochote kile, basi na amrudishie hayo leo kabla ya siku ambayo haitakubaliwa dinari wala dirham. 

2- Akiwa na kheri itachukuliwa kutoka kwake kwa kiasi cha dhulma yake, na ikiwa hana amali njema itachukuliwa baadhi ya maovu ya aliyeifanyiwa dhulma na kubebeshwa”.

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Na iogopeni Siku ambayo mtu hatomfaa mtu kwa lolote, wala hayatakubaliwa kwake maombezi, wala hakitapokewa kikomboleo kwake; wala hawatanusuriwa” .

[Al-Baqara: 48]

Na akasema Mwenyezi Mungu aliyetukuka:

“Wala msiliane mali zenu kwa baat'ili na kuzipeleka kwa mahakimu ili mpate kula sehemu ya mali ya watu kwa dhambi, na hali mnajua”.

[Al-Baqara: 188]

Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayo yafanya madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatapo kodoka macho yao”.

[Ibrahim: 42]

Miradi ya Hadithi