عَنْ عَائِشَةَ رضي الله عنها، قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللهِ :«عَشْرٌ مِنَ الْفِطْرَةِقَصُّ الشَّارِبِ، وَإِعْفَاءُ اللِّحْيَةِ، وَالسِّوَاكُ، وَاسْتِنْشَاقُ الْمَاءِ، وَقَصُّ الْأَظْفَارِ، وَغَسْلُ الْبَرَاجِمِ، وَنَتْفُ الْإِبِطِ، وَحَلْقُ الْعَانَةِ، وَانْتِقَاصُ الْمَاءِ». قَالَ مُصْعَبٌ: وَنَسِيتُ الْعَاشِرَةَ إِلَّا أَنْ تَكُونَ الْمَضْمَضَةَ

Kutoka kwa Aisha, (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani ziwe juu yake) amesema:

1- “Mambo kumi ni ya kimaumbile” 

 2- Kukata masharubu, 

 3- kuacha ndevu zikue, 

 4- Kupiga mswaki, 

 5- Kupandisha maji puani, 

 6- Kukata kucha, 

 7- Kuosha nafasi za vidole. 

 8- kunyofoa nywele za kwapa, 

 9- Kunyoa sehemu za siri 

 10- Kustanji”. 

 11- Musab akasema: Nimesahau la kumi ila nahisi ni kusukutua kinywa .

1. Uislamu unahusika na mambo yote ya nje na ndani ya mwanadamu, ndiyo maana umebainisha muonekana wa Muislamu. Katika Hadith hii, Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake) anaeleza kuhusu baadhi ya mambo ya kimaumbile, ni mambo ya Sunnah ambayo Mwenyezi Mungu amewaumbia waja na kuyaweka kuwa ni sheria, mambo hayo yakitekelezwa, uzuri wa mwili na maumbile kamili ambayo mwanadamu ameumbiwa hupatikana, wenye akili timamu wanalishuhudia hilo. Ila kuna baadhi ya mambo ya kimaumbile yanaweza kupotoshwa na kutolewa katika asili yake,

kama alivyo sema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani ziwe juu yake):

“"Kila mtoto huzaliwa akiwa na asili ya maumbile (yaani mwislaam), wazazi wake wanamfanya kuwa Myahudi, au Mkristo, au majusi. ” [1]


Si kwamba, mambo ya kimaumbile ni haya kumi tu, ambayo amebainisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani ziwe juu yake) katika Hadithi hii, bali, yametajwa katika Hadith nyingine, na wala hatukukusudia kuyataja yote hapa. 


2. La kwanza katika mambo hayo ni: kukata masharubu; ni nywele zinazokua juu ya mdomo wa juu. Imeamrishwa zikatwe kwa sababu zikibaki, zinasababisha kero kwa kile kinacho toka puani, na kuingia kwenye maji wakati wa kunywa, na zinaweza kuwa na vijidudu hatari . [2]
Kukata masharubu ni Sunnah, na inatakiwa katika kuyakata, kujitahidi mpaka mdomo uonekane, na wala sio kuyanyoa. 


3. Ya pili: kuacha ndevu zikue; Nazo ni nywele zinazoota kwenye kidevu na mashavu ya mwanaume. Kinacho kusudiwa katika kuacha ndevu ni kuziacha ziwe nyingi zisiguswe kwa kunyolewa au kupunguzwa. 
Kuziacha ndevu zikue, ni wajibu kwa kila Muislamu, imethibiti katika Hadithi kadhaa zikibainisha hilo: "ziacheni, timizeni kwa kuziacha, ziachieni, ziacheni, ziacheni ziwe nyingi." Kwa hizi Hadithi zote, inaashiria kwambani amri ya kuacha ndevu zikuwe, na wala zsiguswe kwa kukata, kunyoa au kung'oa. 


4. Ya tatu: Kutumia mswaki; Ni kijiti kinachotengenezwa kwa mti wa Arak hutumika kusafisha na kutakasa meno na kinywa, na kuondoa harufu mbaya. 
Kutumia mswaki ni sheria na inapendeza kila wakati, inasisitizwa zaidi wakati wa Swala, na unapo amka kutoka usingizini, harufu ya kinywa inapobadilika na meno yanapoonekana kuwa ya njano;

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani ziwe juu yake):

“mswaki ni kitakasa kinywa, unaridhiwa na  Mola mlezi. ” [3]


5. Nne: Kupandisha maji puani; ni mtu kutia maji puani kisha ayatoe; ili kuondoa maudhi na uchafu uliomo ndani yake. 


6. La tano kati ya mambo hayo: ni kukata kucha, inatakiwa mtu akate kucha ndefu; ili kuzuia uchafu na vijidudu hatari kukusanyika ndani yake. 


7. Ya sita: kuosha fundo za vidole na nafasi zake zote, kwa sababu ni sehemu ambayo mara nyingi huwa zinaficha matope, najisi na vijidudu. Inaingia katika hukumu hii, sehemu zenye mikunjo katika mwili, inatakiwa pasafishwe na kuondoa uchafu uliopo. 


8. Ya saba: kuondoa nywele zinazoota chini ya kwapa; kwa sababu zipo mahali ambapo jasho na uchafu hukusanyika, na kusababisha harufu mbaya. 
Sunnah ni kuondoa nywele hizo kwa njia yoyote ile, iwe kwa kunyoa au kung’oa, kwa sababu lengo ni kuziondoa, na tayari litakuwa limetimia, japo kuwa kung’oa ni bora na vizuri sana kwa mwenye kuweza . [4]


9. Jambo la nane katika mambo ya kimaumbile: ni kunyoa nywele ambazo zinazokuwa sehemu za siri za mwanaume na mwanamke, kuota kwa nywele hizo ni ishara ya balehe. Uondoaji huu unaitwa isithdaad; kwa sababu hutumika chuma - ambacho ni wembe - kuzinyoa. 


10. Jambo la tisa katika mambo ya kimaumbile: ni kutumia  maji kwa ajili ya kujisafisha baada ya kujisaidia. 
Wanazuoni wengine wakasema mtu anyunyizie maji kwenye sehemu zake za siri  au nguo baada ya kutawadha; ili kuondoa wasiwasi kwamba huenda kuna  matone ya mkojo yaliangukia nguo zake . [5]


11. Mmoja wa wapokezi wa Hadithi alisahau sifa ya kumi, akasema, kwa asilimia nyingi itakuwa ni kusukutua; yaani, ni mtu kuzungusha maji kinywani mwake kisha ayateme. 

12. Wanazuoni wengine wakasema, bali sifa ya kumi ni tohara, ushahidi ni kwamba imetajwa katika Hadith iliyopokelewa kutoka na Abu Hurairah

Kutoka kwa Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake): amesema:

“Mambo ya kimaumbile ni matano au matano ni katika mambo ya kimaumile: tohara, kunyoa sehemu za siri, kung'oa nywele za kwapa, kukata kucha, kukata masharubu” . [6]


13. Tohara kwa wanaume ni lazima; nako ni kukata ngozi inayofunika kichwa cha sehemu za siri za mwanaume mpaka chote kiwe wazi; kwa sababu gozi hiyo humeza mkojo na kusababisha uchafu. 


14. Ama kwa wanawake, tohara ni heshima na ni Sunnah. Inafanywa kwa kukata sehemu ndogo kabisa ya ngozi kwenye sehemu ya juu ya uke . [7]


15. Kimsingi, kukata masharubu, kukata kucha, kung'oa nywele za kwapa na kunyoa sehemu za siri, inapaswa viondoshwe haraka mara tu vinapo refuka, ikiwa ni ngumu basi, haipendezi kuviacha hadi siku arobaini zipite. Anas bin Malik (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema: “tuliwekewa muda wa kukata masharubu, kukata kucha, kung'oa nywele za kwapa na kunyoa sehemu za siri, visiachwe zaidi ya usiku arobaini” . [8]

MAFUNDISHO

1- Uislamu umezingatia usafi wa mwanadamu, kwa nje na ndani, na umehakikisha kuwa mtu awe katika hali nzuri

amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao tubu na huwapenda wanao jisafisha”

[Al-Baqarah: 222]

eidha Uislam umefanya “kujitoharisha kuwa sehemu ya imani ”[9], hivyo basi Muislamu hana budi kuuweka mwili na muonekane wake safi, kama anvyo jitahidi kuzingatia usafi wa imani yake na moyo wake. 

1- Mwenyezi Mungu Mtukufu ameweka sharti kwamba mja wake akitaka kusali, awe katika tohara kamili, mwenye nguo na mwili safi, tayari kwa kusimama mbele zake akiwa safi ndani ya kiwiliwili chake kwa toba, na nje kwa usafi na kujipamba, ndo maana mwenye kutawadha husema: “Ewe Mola nijaalie niwe miongoni mwa wanaotubia, na nijaalie niwe miongoni mwa wanaojitakasa.” 

1- Inapendeza kwa mtu kufuata mafundisho ya Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake), kwa kukata sharubu zake, na inapendeza kuanza na upande wa kulia. 

1- Hairuhusiwi mtu kukata au kunyoa ndevu zake, bali kinacho ruhusiwa ni kurekebisha ambazo zimevurugika, ili ziwe na muonekano mzuri. 

1. Haipendezi kwa mtu kuwa na baadhi ya sifa zilizotajwa na wanavyuoni kuhusiana na ndevu; kama vile kuzipaka rangi nyeusi kwa wasio kuwa katika jihadi (vitani), kuzipaka rangi ya manjano ili ionekane kuwa una Zuhdi (umeiacha Dunia na kuifuata Akhera), kuzitia weupe ili kuhadaa uonekane kuwa ni mzee mwenye hekima na maarifa, kunyoa, kung'oa mvi, kuweka mtindo kwa ajili ya kuwavutia wanawake na kuziacha zimevurugika ili kuonyesha kuwa una Zuhdi na kutojijali . [10]


2. Inapendeza mtu kutumia mswaki kusafisha kinywa chake na kukitia manukato ili kuondoa harufu mbaya. Ili kutimiza hilo, inaruhusiwa kutumia mswaki wa brashi, dawa ya meno, na vinginevyo ambayo vitatimiza lengo. 


3. Ni Sunna kutumia mswaki kabla ya kila swala kwa kufuata yale aliyosema Mtume, (Rehema na amani ziwe juu yake):

“Lau nisingeliona kuwa ni uzito kwa Ummah wangu -au kwa watu-, ningeliwaamrisha kutumia mswaki kabla ya kila Swala. ” [11]

1- Si vibaya kutumia mswaki wakati wowote, bali kwa aliyefunga inapendeza kuutumia, kutoka kwa Amer bin Rabi’ah, (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema: “Nimemuona Mtume, (Rehema na amani ziwe juu yake) kwa idadi zisizo hesabika, akipiga mswaki hali ya kuwa amefunga ” [12]

1- Kupandisha maji puani ni miongoni mwa vitendo vinavyosafisha pua, na ndio maana Mtume (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amemuamrisha mwenye kutawadha, akasema: "pandisha maji puani kwenda juu, isipokuwa kama umefunga.  " [13]

1- Muislamu awe na pupa ya kupunguza na kukata kucha, kama inavyopaswa pia kujikagua uchafu unaoingia ndani yake kuzisafisha. 

1- Inaingia katika hukumu ya kuosha vifundo na nafasi za vidole, kila sehemu inayoweza kukusanya uchafu; kama masikio, mikunjamano ya mwili na kila sehemu ambayo jasho au udongo au chochote mfano wake vinaweza jikusanya . [14]

1- Inapendeza kwa mtu kunyoa nywele zake za sehemu ya siri mara kwa mara, kusafisha maeneo yote ambayo yanaota nywele na kusafisha maeneo ya  mapaja yake, na kuhakikisha kwamba maji yameingia kwenye ngozi vyema, kwa sababu maeneo hayo nivyepesi kupata magonjwa na maambukizi. 

1. Bila shaka kutumia maji kusafisha mahali baada ya kujisaidia ni bora kuliko kutumia vitu tofauti na maji wakati kuna maji. Kwani kutumia maji uchafu uondolewa kabisa, na athari zake hutakaswa, na harufu yake mbaya hutolewa kutoka mahali pa najisi.


2. (11) udanganyifu na kujiona visimzuie Muislamu kutokubali haki au kusema ukweli; kwani Msimulizi wa Hadith hii alipotia shaka kuwa amesahau sifa yoyote kati ya hizo, alisema wazi; hivyo Basi kuweka wazi kosa, au kusahau na kutojua ni bora kuliko kumzulia uongo Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake, amani iwe juu yake.


3. (11) kusukutua kinywa ni miongoni mwa Sunnah za maumbile ambazo Muislamu anatakiwa kuzipupia na kudumu nazo. Ili apate radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu na malipo ya kumfuata Mtume Wake, na ili akamilishe twahara kamili.


5. Mshairi alisema:
Ulizaliwa na asili yako ambayo = ni imani na kusadikisha uwepo wa Muumba 
Na umetahiniwa kwa kupewa mamlaka ya kuchagua= na mbele yako  kuna njia mbili ziko wazi.
Basi ukifanya kila ulitakalo, tambua kuwa  uko chini ya uangalizi = kwani wewe huwezi kufichikana mbele ya Mwenyezi Mungu Hakimu.

Marejeo

  1. Imesimuliwa na Al-Bukhari (1385) na Muslim (2658), kwa kutoka kwa Abu Hurayrah (ra)
  2. “Sharh Riyadh as-Salihin” cha Ibn Uthaymiyn (5/230).
  3. Imesimuliwa na Al-Nasa’i (5), na Al-Bukhari alitoa maoni ya msistizo kabla ya hadith (1934).
  4. Sherh  Al-Nawawi alaa Muslim” (3/149).
  5. Sherh  Al-Nawawi alaa Muslim”   (3/150)
  6. Imepokewa na Al-Bukhari (5889) na Muslim (257).
  7. “Sharh Riyadh as-Salihin” cha Ibn Uthaymiyn (5/229).
  8. Imepokewa na Muslim (258).
  9. Imepokewa na Muslim (223).
  10. Sherh  Al-Nawawi alaa Muslim (3/149, 150).
  11. Imepokewa na Al-Bukhari (887) na Muslim (252).
  12. Imepokewa na Al-Tirmidhiy (725), na amesema Hadithi nzuri, na Al-Bukhari akatoa maoni kwa kusisitiza Hadithi (1934).
  13. Imepokewa na Abu Daawuud (142), Al-Tirmidhiy (788), Al-Nasa’i (114), na Ibn Majah (448).
  14. Tazama: “sherh  Al-Nawawi alaa Muslim” (3/150).



Miradi ya Hadithi