عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهَا زَوْجِ النَّبِيِّ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ ﷺ كَانَ عِنْدَهَا، وَأَنَّهَا سَمِعَتْ صَوْتَ رَجُلٍ يَسْتَأْذِنُ فِي بَيْتِ حَفْصَةَ، قَالَتْ: فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، هَذَا رَجُلٌ يَسْتَأْذِنُ فِي بَيْتِكَ، فَقَالَ النَّبِيُّ ﷺ: «أُرَاهُ فُلاَنًا»، لِعَمِّ حَفْصَةَ مِنَ الرَّضَاعَةِ، قَالَتْ عَائِشَةُ: لَوْ كَانَ فُلانٌ حَيًّا - لِعَمِّهَا مِنَ الرَّضَاعَةِ - دَخَلَ عَلَيَّ؟ فَقَالَ: «نَعَمْ؛ الرَّضَاعَةُ تُحَرِّمُ مَا تُحَرِّمُ الوِلادَةُ» 

Kutoka kwa Aisha, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, mke wa Mtume, rehma na amani zimshukie:

1-    Kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu alayhi wa sallam alikuwa kwa Aisha, na Aisha akasikia sauti ya mtu akibisha hodi katika nyumba ya Hafsa, : Akasema: Huyu mtu anabisha hodi nyumbani kwako, basi Mtume rehma na amani zimshukie akasema: “Ninamuona ni mtu Fulani ” kwa ami yake Hafsa kwa kunyonya sehemu moja. 2. Aisha akasema: unasemaje lau fulani angekuwa hai - ami yake kwa kunyonya – akaja nyumbani kwangu? Naye akasema: Ndiyo. Kunyonyesha kunayaharamisha yote yaliyoharamishwa kutokana na nasaba na kuzaa”


Miradi ya Hadithi