عَنْ أُمِّ عَطِيَّةَ رضي الله عنها، أَنَّ رَسُولَ اللهِ  قَالَ: «لَا تُحِدُّ امْرَأَةٌ عَلَى مَيِّتٍ فَوْقَ ثَلَاثٍ، إِلَّا عَلَى زَوْجٍ، أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْرًا، وَلَا تَلْبَسُ ثَوْبًا مَصْبُوغًا، إِلَّا ثَوْبَ عَصْبٍ، وَلَا تَكْتَحِلُ، وَلَا تَمَسُّ طِيبًا، إِلَّا إِذَا طَهُرَتْ، نُبْذَةً مِنْ قُسْطٍ أَوْ أَظْفَارٍ»


Kutoka kwa Ummu Atiyah, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kwamba Mtume

wa Mwenyezi Mungu rehema na amani zimshukie, amesema: 1. “Mwanamke hakai matanga kwa kufa yoyote zaidi ya siku tatu, isipokuwa kwa kufiwa na mume atakaa miezi minne na masiku kumi.  2.Wala havai nguo iliyo tiwa rangirangi isipokuwa nguo pana ya moja kwa moja, na wala asipakae wanja, na wala asiguse manukato na marashi isipokuwa akiwa safi baada ya hedhi. Atumie kiasi kidogo cha marashi na manukato au kucha”


Ummu Atiyah Al-Ansari, Mungu

Ummu Atiyah Al-Ansari, Mungu amuwiye radhi, Sahaba mkubwa, ambaye alijulikana kwa lakabu yake, na jina lake: Nusaiba binti Kaab, na ikasemwa: Nusaiba binti Al-Harith Alikuwa akienda sana na Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehma na Amani zimfikie akiwauguza wagonjwa na kuwatibu majeruhi, na Yeye ndiye aliyemuosha, Zainab, binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehma na Amani ziwe juu yake. [1]

Marejeo

1. Tazama tafsiri yake katika: “Al-Isti’ab” (4/1947), “Asad Al-Ghaba” (7/356), “Al-Isbah” (8/437).

Miradi ya Hadithi