عن عبدِ الله بنِ مُعاويةَ رضي الله عنه ، قال: قال النبيُّ :«ثلاثٌ مَن فعَلهنَّ فقد طَعِمَ طَعْمَ الإيمانِ:مَن عبَدَ اللهَ وحدَه، وأنه لا إلهَ إلا اللهُ،وأعطى زكاةَ ماله طيِّبةً بها نفْسُهُ، رافدةً عليه كلَّ عام،ولا يُعطي الهَرِمةَ، ولا الدَّرِنةَ، ولا المريضةَ، ولا الشَّرَطَ اللئيمةَ؛ولكنْ مِن وسَطِ أموالكم؛ فإنَّ اللهَ لم يَسألْكم خيرَه، ولم يأمُرْكم بشرِّه»

Kutoka kwa Abdullah bin Muawiyah Mwenyezi Mungu awe radhi naye amesema: Mtume, rehma na Amani zimshukie, amesema:

“Mambo matatu atakaye yafanya ameonja ladha ya imani. Mwenye kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na kwamba hapana mungu mwingine ila yeye Mwenyezi Mungu. Akatoa zaka ya mali yake kwa niya njema kutoka moyoni mwake, haliyakuwa nafsi yake inamuamuru kufanya hivyo kila mwaka. Hatoi mnyama aliyezeeka, wala mwenye ugonjwa wa ngozi, wala mgonjwa, wala dhaifu; Lakini toeni za kati na kati katika mali zenu; Mwenyezi Mungu hakukuombeni vilivyo bora zaidi, wala hakukuamrisheni mtoe vibaya.”

Muhtasari wa Maana

Mtume Rehma na Amani ziwe juu yake anafahamisha mambo yanayodhihirisha imani ya mja ambayo ni tawhidi, kutoa zaka kwa uhuru na raha, kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, na kuchagua zaka katika mali yake, ili asitoe zaka katika wanyama wagonjwa, wazee, au wenye kasoro

Miradi ya Hadithi