عن أبي هريرة : أنَّ رَجُلًا قالَ للنبيِّ ﷺ: أوْصِنِي، قَالَ: «لَا تَغْضَبْ»، فَرَدَّدَ مِرَارًا، قَالَ: «لَا تَغْضَبْ».
عن أبي هريرة : أنَّ رَجُلًا قالَ للنبيِّ ﷺ: أوْصِنِي، قَالَ: «لَا تَغْضَبْ»، فَرَدَّدَ مِرَارًا، قَالَ: «لَا تَغْضَبْ».
Kutoka kwa Abu Hurairah Mwenyezi Mungu awe radhi naye amesema:
1- Mtu mmoja alimwambia Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam: “Ninasihi.
2- Akasema Mtume: “Usikasirike”
3- Mtume alirudia mara kadhaa akisema: “Usikasirike”
1- Alikuja mtu kwa Mtume rehma na Amani zimshukie akitaka wosia wa kina uliokusanya aina za kheri na sababu za kufaulu ili azihifadhi na kuzifanyia kazi.
2- Mtume rehma na Amani zimshukie akamnasihi asikasirike, kwani ghadhabu ni ufunguo wa maovu yote, na kujikinga nayo ni njia ya kheri.Baadhi ya wanavyuoni walieleza hata tabia njema kwa kuacha hasira; Hasira humsukuma mtu kuua, kupiga, kutukana, na kusema maneno machafu, sawa na vile inavyomfanya mtu aape viapo vikali, na mara nyingi humsukuma kumtaliki mke wake au kuachana na jamaa zake. Bali hasira inaweza kupelekea mtu kutumbukia katika ukafiri na ushirikina, Mwenyezi Mungu atulinde nayo.
3- Yule mtu akarudia swali ili Mtume Rehma na amani zimshukie amwongezee jambo jengine ambalo litamnufaisha duniani na akhera. Hakuongeza Mtume rehma na Amani zimshukie kauli nyengine tofauti na kusema kwake: “Usikasirike”.
Na makatazo ya Mtume rehma na Amani zimshukie, juu ya ghadhabu yamekusudiwa kuziacha sababu zinazopelekea mizozo na kugombana kwa dhulma, na kufanya yale yanayozuia hasira ikiwemo kuvumilia, ukarimu, kukandamiza hasira, kuwavumilia watu, uchangamfu na bashasha. Iwapo sifa hizi zitapatikana katika nafsi, ni wajibu kuizuia hasira inapotokea sababu zake.
Inakusudiwa pia kutotenda lolote inapotokea hasira; Mwislamu akikasirika na akahisi dhiki ya hali ya juu, ni lazima aizuie hasira yake, na asiseme lolote au asitende kwa sababu ya hasira yake, kwani hilo litamwingiza katika dhambi.
Mwenyezi Mungu Mtukufu amewasifu waja wake ambao hudhibiti hisia zao, katika ghadhabu zao, hukandamiza hasira zao na huwasamehe waliowakosea.
Amesema Mwenyezi Mungu:
“Na yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi, iliyo wekwa tayari kwa wachamungu (133) Ambao hutoa wanapo kuwa na wasaa na wanapo kuwa na dhiki, na wanajizuia ghadhabu, na wasamehevu kwa watu; na Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema”
[Al Imran: 133, 134]
Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, ameeleza juu ya malipo makubwa ya wale wasiokasirika kwa kusema:
“Mwenye kuzuia ghadhabu yake na hali ana uwezo wa kuitoa, basi Mwenyezi Mungu atamwita mbele ya viumbe wote Siku ya Qiyama na kumhiyarisha kilicho bora kwake” [1]
1- Kila Muislamu atafute ushauri kwa wenye elimu na wenye uzoefu. Ushauri wao utampa mtu muhtasari wa uzoefu na ujuzi wao.
2- Maswahabah, Mwenyezi Mungu awawie radhi, walijali sana kumwomba ushauri Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, juu ya kila linalowatatiza, na walifanya hivyo mara nyingi. Huu ni ushahidi wa uaminifu wa ufuasi wao na shauku yao ya kujifunza na kujua sheria ya Mwenyezi Mungu. Na tunapaswa kuwaiga.
3- Mlinganiaji na muelimishaji wanatakiwa kumnasihi kila mmoja kwa mujibu wa hali yake, kwani mtu huyu aliyemuomba Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam alionekana kuwa na hasira, na kwa ajili hiyo akamusia asikasirike, na hakumnasihi kufanya kitu kingine.
4- Jihadhari na hasira; kwani humnyima mja kutambua sheria ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, hivyo humlazimisha Muislamu kusema uwongo, kuwatuhumu wengine, kuwatukana, na kuwatuhumu watu kwa waliyoyatenda.
Ndio maana moja ya dua zake Mtume, amani iwe juu yake, ilikuwa:
“Ninakuomba neno la kweli katika hali ya hasira na kuridhika” [2]
5- Fahamu kwamba kupigana dhidi ya nafsi yako ni nguvu zaidi kuliko kupigana na maadui. Kwani nafsi huamrisha uovu, inayomchochea mtu kuwapiga waliomdhulumu, sawa awe adui au kipenzi.Ndio maana Mtume
swallallahu alayhi wa sallam, akasema:
“Mwenye nguvu si yule mwenye kuangushana mieleka; Mwenye nguvu ni yule anayejizuia anapokasirika” [3]
Sio mwenye nguvu anayewapiga watu na kuwashinda, lakini mwenye nguvu kisawasawa, ni mwenye hujidhibiti akiwa na hasira.Ndio maana Al-Hassan Al-Basri, Mwenyezi Mungu amrehemu, alisema alipoulizwa: Jihad ipi iliyo bora zaidi? Akasema: “Jihad yako dhidi ya nafsi yako na matamanio yako” [4]
6- Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam ni kiigizo chetu sote, pia Mtume, rehma na amani zimshukie, hakukasirikia kwa ajili ya nafsi yake, wala hakujinusuru. bali alikuwa anakasirika kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
Mama wa Waumini, Aisha, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema:
“Mtume rehma na Amani zimshukie, hakujilipiza kisasi kwa ajili ya nafsi yake isipokuwa tu unapovunjwa Utakatifu wa Mwenyezi Mungu, basi analipiza kisasi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu” [5]
Hasira ni jambo baya isipokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, hivyo ni wajibu kwa kila Muislamu.
7- Mtume rehma na amani zimshukie alielekeza njia za kuzuia ghadhabu na kuitibu. Ni kule kutafuta kimbilio kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani aliyelaaniwa. Siku moja watu wawili walitusiana mbele ya Mtume rehma na amani zimshukie tukiwa tumekaa naye. Na mmoja wao anamtukana rafiki yake, uso wake ukawa mwekundu kwa hasira
na akasema Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam
“Hakika mimi ninalijua neno amabalo, kama atalitamka mtu huyo, itaondoka hasiraa yake, lau akisema: Najikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani aliyelaaniwa”[6]
Muislamu akiona dalili za hasira ndani yake, basi atafute hifadhi kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani aliyelaaniwa.
8-Moja ya njia za kutibu na kudhibiti hasira ni kukaa ikiwa mtu amesimama, na kulala chini akiwa amekaa; Kwani aliyesimama yuko tayari kulipiza kisasi, na aliyekaa ndiye anayefuatia, na mwenye kulalia ubavu yuko mbali zaidi na hao.
Mtume amani iwe juu yake amesema:
“hakika hasira ni kaa la moto lililomo ndani ya moyo wa mwana Adam, ndio maana mnaona wekundu wa macho yake, na kuvimba misuli yake, Kwa hiyo yeyote atakayehisi chochote kutokana na hilo, basi na ajilaze chini” [7]
Pia akasema:
“Ikiwa mmoja wenu amekasirika akiwa amesimama, basi na aketi chini, na ikiwa hasira itamtoka, hilo ni bora, vinginevyo na alale chini” [8]
9-Njia mojawapo ya kudhibiti hasira ni mtu kukaa kimya. Na lau akisema, hasira zilimtawala, basi yeye ndiye atakuwa akizungumza tofauti na wengine
na ndio maana Akasema Mwenyezi Mungu:
“Na ukikasirika basi nyamaza. “Na Musa ilipo mtulia ghadhabu” .
[Al-Araf: 154]
Na akasema Mtume Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
“Na ukikasirika basi nyamaza” [9]
10- Jihadhari na kutamka mambo kwa hasira ambayo yatakupotezea uhai na kukupelekea kujuta maisha yako yote. Ni kiasi gani hasira ilimsababishia mmiliki wake fedheha na majuto. Hata Ataa bin Abi Rabah, Mwenyezi Mungu amrehemu, amesema: “Hakuna kitu kibaya zaidi kilichowaliza Wanachuoni mpaka mwisho wa maisha yao kuliko hasira ambayo mmoja wao aliikasirisha, na akaharibu maisha ya miaka hamsini, au miaka sitini, au sabini. Na pengine hasira imemlazimu mwenye nayo kulazimisha alichojiuzulu”[10] Mawreq Al-Ijli, Mwenyezi Mungu amrehemu, amesema: “Sikusema chochote kwa hasira ila nilijuta wakati ilipoondoka kuridhika” [11]
11- Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam hakuongeza katika wosia wake kuacha hasira; kwa sababu ni kichwa cha kila jambo baya; aliambiwa Ibn Al-Mubarak, Mwenyezi Mungu amrehemu: “Tukusanyie tabia njema kwenye neno moja.” Akasema: “Kuacha hasira” [12]
12- Amesema Mshairi:
Kuzuia hasira yangu ni bora kuliko jaribio langu = dhidi ya adui kwa kuharibu imani yangu
Hakuna kheri katika jambo ambalo matokeo yake yatanitia simanzi = Siku ya Kiyama akiba yangu itapopungua
13- Mshairi mwingine akasema:
Na sijaona wema uliokamilishwa ila kwa kitu = na sijaona mwenye akili timamu ila kwa misingi ya tabia njema.
Na sijaona kwa maadui nilipowajaribu = adui mkubwa wa akili ya mtu kuliko hasira.