عن أبي هريرة رضي الله عنه، قال: قال رسولُ الله ﷺ: «مَن لم يَدَعْ قولَ الزُّورِ والعَمَلَ به والجهلَ، فليس لله حاجةٌ في أن يَدَع طعامَه وشَرَابَه».
عن أبي هريرة رضي الله عنه، قال: قال رسولُ الله ﷺ: «مَن لم يَدَعْ قولَ الزُّورِ والعَمَلَ به والجهلَ، فليس لله حاجةٌ في أن يَدَع طعامَه وشَرَابَه».
Kutoka kwa Abu Huraira Mwenyezi Mungu awe radhi naye amesema:
Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimshukie: “Yeyote asiyeacha maneno ya uwongo na kuyafanyia kazi na ujinga, basi Mwenyezi Mungu hana haja naye kwa kuacha chakula na kinywaji chake.”
Amesema Mwenyezi mtakatifu: “Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kumcha Allah ”
[Al-Baqarah: 183].
Na akasema Allah ambaye jina lake ni tukufu: “Basi jiepusheni na uchafu wa masanamu, na jiepusheni na usemi wa uwongo” .
[Hajj: 30]
Mwenyezi Mungu amesema: “Na waja wa Arrahman Mwingi wa Rehema ni wale wanao tembea ulimwenguni kwa staha, na wajinga wakiwasemeza hujibu kwa kusema : Amani” .
[Al-Furqan: 63]
Amesema Allah Mtukufu : “Na wale ambao hawatoi ushahidi wa uwongo, na pindi wapitapo penye upuuzi, hupita kwa hishima yao”.
[Al-Furqan: 72]