عن أبي هريرة رضي الله عنه، قال: قال رسولُ الله ﷺ: «مَن لم يَدَعْ قولَ الزُّورِ والعَمَلَ به والجهلَ، فليس لله حاجةٌ في أن يَدَع طعامَه وشَرَابَه».

Kutoka kwa Abu Huraira Mwenyezi Mungu awe radhi naye amesema:

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimshukie: “Yeyote asiyeacha maneno ya uwongo na kuyafanyia kazi na ujinga, basi Mwenyezi Mungu hana haja naye kwa kuacha chakula na kinywaji chake.”


Muhtasari wa Maana

Makusudio ya saumu ni uchamungu na kulinda ulimi na viungo na haramu. Ikiwa hili halitafikiwa na mtu akajishughulisha na mambo ya haramu akiwa amefunga, basi hakuna thamani ya kufunga huko mbele ya Mwenyezi Mungu.

Miradi ya Hadithi