عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه: أَنَّ رَسُولَ اللهِ ﷺ مَرَّ عَلَى صُبْرَةِ طَعَامٍ، فَأَدْخَلَ يَدَهُ فِيهَا، فَنَالَتْ أَصَابِعُهُ بَلَلًا،  فَقَالَ: «مَا هَذَا يَا صَاحِبَ الطَّعَامِ؟» قَالَ: أَصَابَتْهُ السَّمَاءُ يَا رَسُولَ اللهِ،  قَالَ: «أَفَلَا جَعَلْتَهُ فَوْقَ الطَّعَامِ كَيْ يَرَاهُ النَّاسُ؟!  مَنْ غَشَّ فَلَيْسَ مِنِّي»



Kutoka kwa Abu Hurairah Mwenyezi Mungu awe radhi naye,

1- Mtume rehma na amani zimshukie alipita karibu na chombo cha chakula, akaweka mkono wake ndani yake, na vidole vyake vikalowa. 2- Akasema Mtume: “Ni nini hiki ewe mwenye chakula? Akasema: kimenyeshewa na Mvua ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. 3- Akasema Mtume: Kwa nini hukukiweka juu ya chakula ili watu wapate kukiona? 4- Adanganyaye si katika mimi”. 


Muhtasari wa Maana

Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam alikagua bidhaa za mfanyabiashara na akakuta unyevunyevu ndani ya chakula, hivyo akamwambia kuwa jambo hilo halijuzu, na kwamba udanganyifu ni haramu na haijuzu

Miradi ya Hadithi