عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه: أَنَّ رَسُولَ اللهِ ﷺ مَرَّ عَلَى صُبْرَةِ طَعَامٍ، فَأَدْخَلَ يَدَهُ فِيهَا، فَنَالَتْ أَصَابِعُهُ بَلَلًا،  فَقَالَ: «مَا هَذَا يَا صَاحِبَ الطَّعَامِ؟» قَالَ: أَصَابَتْهُ السَّمَاءُ يَا رَسُولَ اللهِ،  قَالَ: «أَفَلَا جَعَلْتَهُ فَوْقَ الطَّعَامِ كَيْ يَرَاهُ النَّاسُ؟!  مَنْ غَشَّ فَلَيْسَ مِنِّي»



Kutoka kwa Abu Hurairah Mwenyezi Mungu awe radhi naye,

1- Mtume rehma na amani zimshukie alipita karibu na chombo cha chakula, akaweka mkono wake ndani yake, na vidole vyake vikalowa. 2- Akasema Mtume: “Ni nini hiki ewe mwenye chakula? Akasema: kimenyeshewa na Mvua ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. 3- Akasema Mtume: Kwa nini hukukiweka juu ya chakula ili watu wapate kukiona? 4- Adanganyaye si katika mimi”. 


Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mwenyezi Mtukufu:

“Enyi mlio amini! Kuleni vizuri tulivyo kuruzukuni, na mumshukuru Mwenyezi Mungu, ikiwa kweli mnamuabudu Yeye tu”. 

[Al-Baqara: 172]

Na akasema pia:

“Wala msiliane mali zenu kwa baat'ili na kuzipeleka kwa mahakimu ili mpate kula sehemu ya mali ya watu kwa dhambi, na hali mnajua”.

[Al-Baqara: 188]

Miradi ya Hadithi