عن العِرباضِ بنِ ساريةَ قال: قام فينا رسولُ الله ﷺ ذاتَ يوم، فوعَظَنا موعظةً بليغةً، وَجِلَتْ منها القلوبُ، وذَرَفَت منها العيونُ، فقيل: يا رسول الله، وعظْتَنا موعظةَ مُوَدِّع، فاعهَدْ إلينا بعهدٍ، فقال: «عليكم بتقوى الله، والسمعِ والطاعة، وإنْ عبدًا حبشيًّا، وسترَوْنَ من بعدي اختلافًا شديدًا، فعليكم بسُنَّتي، وسُنَّة الخلفاء الراشدين المهديِّين، عَضُّوا عليها بالنَّوَاجِذ، وإيَّاكم والأمورَ المُحدَثاتِ؛ فإن كلَّ بِدعة ضلالة».

00:00
00:00
تحميل الملف الصوتي
00:00
00:00
تحميل الملف الصوتي

Kutoka kwa Al-Irbaadh bin Sariya, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema:

1- Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimshukie alisimama kati yetu siku moja na kutuhutubia hotuba fasaha iliyozifanya nyoyo zitetemeke na macho kutoa machozi. 

2- Ikasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu mawaidha yako ni mawaidha ya kuaga, basi tuusie . 

3- Akasema: “Juu yenu kumcha Allah. 

4- Kusikia na kutii, hata kama mtumwa wa Kihabeshi. 

5- Na mtaona ikhitilafu kali baada yangu. Ni lazima kushikamana na Sunnah zangu, na Sunnah za Makhalifa walioongoka, mzing’ang’anie kwa magego . 

6- Jihadharini na mambo mapya yaliyozushwa. Kwani kila uzushi ni upotofu.” 

Abu Najih, Al-Irbad bin Sariya, Al-Sulami

Yeye ni: Abu Najih, Al-Irbad bin Sariya, Al-Sulami, kutoka kwa watu wa Al-Suffa, aliyeshuka kutoka kwa Mtukufu. Na alikaa Homs, na alikuwa mion-goni mwa maswahaba ambao aya hii iliteremka kwa ajili yao. “Wala wale waliokujia ili uwachukue ukasema: Sina kipando cha kukuchukueni. Tena wakarudi na macho yao yanamiminika machozi kwa huzuni ya kukosa cha kutoa” [Al-Tauba: 92], Alifariki katika mwaka wa (75 AH), na ikasemwa: Katika fitna ya Ibn al-Zubayr (1).

Marejeo

  1. 1 tazama: “Ma’rifat al-Sahaba” na Abu Nu’aym (4/ 2234), “Al-Isti’ab fi Ma’rifat al-Ashab” na Ibn Abd al-Barr (3/ 1238)., “Siyar A'lam al-Nubala'” cha al-Dhahabi (4/ 431).


Miradi ya Hadithi