عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، عَنِ النَّبِيِّ ﷺ، قَالَ: «اجْتَنِبُوا السَّبْعَ المُوبِقَاتِ» قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، وَمَا هُنَّ؟ قَالَ: وَالسِّحْرُ، وَقَتْلُ النَّفْسِ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلَّا بِالحَقِّ، وَأَكْلُ الرِّبَا، وَأَكْلُ مَالِ اليَتِيمِ، وَالتَّوَلِّي يَوْمَ الزَّحْفِ، وَقَذْفُ المُحْصَنَاتِ المُؤْمِنَاتِ الغَافِلاَتِ». 

Kutoka kwa Abu Huraira, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kutoka kwa Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, ambaye amesema: 1- “Jiepusheni na madhambi saba yenye kuangamiza.” Wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, na ni yapi? Akasema Mtume: 2- “Kumshirikisha Mwenyezi Mungu, 3- Na uchawi, 4- Kuiua nafsi aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu, isipokuwa kwa uadilifu. 5- Kula riba 6- Kula pesa za yatima 7- Kuikimbia vita 8- Na kuwatuhumu na machafu wanawake walio safi, Waumini walioghafilika”


1. Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam anauhadharishia ummah wake juu ya madhambi saba ya kuangamiza, ambayo yatamuangamiza mwenye kuitenda na kumuingiza kwenye moto wa Jahannam.

2. Moja ya hayo madhambi hatarishi: ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, nayo ndio dhambi kubwa kabisa, amesema ibni masoud Mwenyezi Mungu awe radhi naye: nilimuuliza Mtume Amani iwe juu yake:ni Dhambi ipi ambayo ni kubwa zaidi kwa Mwenyezi Mungu? Akasema Mtume: “ni kumjaalia Mwenyezi Mungu Mshirika na hali yeye ndiye kakuumba”. [1]  Na shirki ndio dhambi kubwa ambayo Mwenyezi Mungu haisamehe, ila mja akirudi na kutubia kwake Mwenyezi Mungu, na aboreshe itikadi yake na ibada yake, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi kushirikishwa na kitu. Lakini Yeye husamehe yasiyo kuwa hayo kwa amtakaye. Na anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu basi huyo amepotea upotovu wa mbali”

[An-Nisaai: 116]

3 . Dhambi ya pili ni uchawi: asili ya uchawi ni kukitoa kitu katika uhalisia, iwe kwa kuwatumia mashetani au kuwatumikisha, au kwa madawa, moto na mengineyo, ni dhambi kubwa kabisa yenye malipo mabaya zaidi, kwakuwa na mchanganyo wa mambo, mazingaombwe na kuficha

Na haya madhambi Saba ni miongoni mwa madhambi makubwa ambayo yameelezwa katika Qur’an na Sunnah kwa adhabu ya moto, laana, au chuki ya Mwenyezi Mungu au adhabu. Haikuishia kwa hizo saba Mtume Rehema na Amani zimshukie amezitaja katika Hadithi hii, bali ni nyingi, zikiwemo uzinifu, wizi, uasi kwa wazazi na mengineyo. hizo saba kwa sababu ndizo chafu na uhalifu mkubwa zaidi, pamoja na wingi wa kutokea kwake katika zama zake rehma na Amani zimshukie.

. uhalisia, na kuweka kizibo machoni, na kuwapotosha watu, kuharibu itikadi katika kuweka visababishi katika sababu zake ikiwa ni pamoja na kumsababishia madhara aliyefanyiwa uchawi, kama marahi, kutokwa akili, na inaweza kupelekea kuua. Ndio maana uchawi ukawa ni katika madhambi makubwa kutenda, kujifunza na kusomesha.

Mara nyingi uchawi hutokana na kuwatumia na kuwatumikisha mashetani, na hili hukamilika kwa kumkufuru Mwenyezi Mungu mtukufu. Mashetani hayakubali kufanya uchawi ila mpaka mchawi akubali kumkufuru Mwenyezi Mungu [2],. Amesema Mwenyezi Mtukufu: “Bali mashet'ani ndio walio kufuru, wakiwafundisha watu uchawi, na yaliyo teremshwa kwa Malaika wawili, Haaruta na Maaruta katika Baabil. Wala hao hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni mtihani; basi usikufuru. [Al-Baqara: 102]. Ndio maana Wanachuoni wengi wanasema Mchawi auawe kwa hadi kutokana na ukafiri wake na kuritadi, iwe uchawi wake umesababisha kifo au laa.

4. Dhambi ya tatu ni kuua Nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharamisha kuuawa pasina haki,damu za waislamu ni haramu kumwagika kwa kauli ya Mtume rehma na amani zimshukie: “Kwa hakika damu yenu, mali yenu, na hishma zenu, ni haramu kwenu mwenu, kama ilivyoharamishwa siku yenu hii, katika mwezi huu” [3]

Mara nyingi uchawi hutokana na kuwatumia na kuwatumikisha mashetani, na hili hukamilika kwa kumkufuru Mwenyezi Mungu mtukufu. Mashetani hayakubali kufanya uchawi ila mpaka mchawi akubali kumkufuru Mwenyezi Mungu ,. Amesema Mwenyezi Mtukufu: “Bali mashet'ani ndio walio kufuru, wakiwafundisha watu uchawi, na yaliyo teremshwa kwa Malaika wawili, Haaruta na Maaruta katika Baabil. Wala hao hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni mtihani; basi usikufuru. [Al-Baqara: 102]. Ndio maana Wanachuoni wengi wanasema Mchawi auawe kwa hadi kutokana na ukafiri wake na kuritadi, iwe uchawi wake umesababisha kifo au laa.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amemtishia muuwaji wa Muumini adhabu iumizayo. Akasema, Mwenyezi Mungu:

“Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa” .

[An-Nisaai: 93]

Vilevile Mwenyezi Mungu Mtukufu ameharamisha damu ya wasio Waislamu, watu wa dhimma, wasimamizi na walio katika ahadi ya kuufuata uislamu, Mwenyezi Mungu amesema:

“Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu”

[Al-Mumtahinat: 8]

Na akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Mwenye kumuuwa kafiri anayeishi chini ya dhimma ya mtawala wa kiislamu hatasikia harufu ya Pepo, na harufu yake itapatikana kwa umbali wa miaka arubaini"  [4]

5. Ya nne: Kula riba, ambayo ni ongezeko linalotokana na kubadilishana riba kwa aina yake au kwa kuchelewesha kupokea kile kinachopaswa kupokelewa kutokana na riba [5] .Ufafanuzi wa hili ni kwamba mtu anauza, kwa mfano, gramu ya dhahabu ya zamani kwa gramu mbili za dhahabu mpya, au anampa ndugu yake pishi ya tende nzuri kwa kubadilishana na pishi mbili za tende mbaya. Hii inaitwa Riba al-Fadl, ambayo ni pale mtu anapouza kitu cha riba - dhahabu, fedha, tende, ngano, shayiri na chumvi - kwa mfano wake, na kuongezeka thamani ya bei. Katika aina hii ni sharti kuuza kipimo kwa kipimo, gramu kwa gramu, na dirham kwa dirham bila kuzidiana. Aina ya pili ni riba An-Nasiat, nayo ni aina maarufu na iliyozoeleka zaidi, na ni pale mtu anapomkopesha ndugu yake mkopo kwa sharti la nyongeza wakati wa malipo, hivyo anampa dinari mia moja, kwa mfano, kwa sharti arudishe baada ya mwezi mia moja na kumi.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ameharamisha riba na anawaadhibu vikali wale wanaokula, Akasema Allah Mtukufu:

“Mwenyezi Mungu huiondolea baraka riba, na huzibariki sadaka. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila mwenye kufanya khiyaana na afanyae dhambi” [Al-Baqara: 276]. Na akasema utukufu ni wake: “Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba zilizo bakia, ikiwa nyinyi ni Waumini (278) Basi ikiwa hamkufanya hivyo jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake.”

[Al-Baqara: 278,279].

Na Jabir Mwenyezi Mungu awe radhi naye amesema: “Mtume rehma na amani zimshukie amemlaani mwenye kula riba, mwenye kuilipa, mwenye kuiandika, na mwenye kuishuhudia.” Na akasema. : “Wanafanana katika malipo.” [6] 

6. Ya tano: Kula pesa za yatima, Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam alimhusisha kwa kumtaja na kuwaacha watu wengine wote, ingawa kula fedha za watu kwa dhulma kwa ujumla ni dhambi kubwa, kwa sababu yatima ni mtoto mdogo na hawezi kujipatia riziki, na hana uwezo wa kumzuia dhalimu katoka fedha zake, tofauti na mtu mzima.Mwenyezi Mungu anasema:

“Hakika wanao kula mali ya mayatima kwa dhulma, hapana shaka yoyote wanakula matumboni mwao moto, na wataingia Motoni”

[An-Nisaai: 10]

 Na lililoharamishwa sio kula pesa yake tu, ila kwamba inajuzu kuchukua pesa zake na kuzitumia kwa vitu vingine tofauti na kula. Bali inakusudiwa kujimilikisha, na akataja kula kwa sababu ndiko kuliko zaidi.

7. Sita: Kukimbia vita, kwa sababu haijuzu kwa Muislamu kukimbia akiwa anakimbia vita akiwa anapigana na makafiri. Kwa sababu huo ni woga unaopelekea kushindwa kwa Waislamu na kudhoofika kwa azma yao, na Mwenyezi Mungu Mtukufu amewausia Waumini kuwa wasimame katika vita na wasitoroke, basi Mwenyezi Mungu utukufu ni Wake, amesema:

“Enyi mlio amini! Mkikutana na jeshi, basi kueni imara, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu sana ili mpate kufanikiwa”

[Al-Anfal: 45]

, Hili liliwekewa mipaka ikiwa washirikina watakuwa mara mbili ya idadi ya Waislamu au chini ya hapo, na ikiwa washirikina watakuwa wachache kuliko Waislamu au sawa nao au kuwazidi mara mbili au pungufu, Waislamu lazima wabaki imara, na kukimbia inakuwa ni dhambi kubwa, isipokuwa akikimbia kurudi katika kundi la Waislamu ambao wangewasaidia na kumsaidia, huko si kukimbia, au washirikina wakiwa wengi zaidi kuliko Waislamu, basi kwa hali hiyo inajuzu kukimbia. Mwenyezi Mungu anasema:

“Enyi Mlio amini! Mkikutana na walio kufuru vitani msiwageuzie mgongo” (15) Na atakaye wageuzia mgongo wake siku hiyo - isipo kuwa kwa mbinu za vita au kuungana na kikosi - basi atakuwa amestahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Na pahala pake ni Jahannamu, na huo ni mwisho muovu” .

[Al-Anfal: 15, 16]

Na akasema tena Mwenyezi Mungu:

“ Sasa Mwenyezi Mungu amekupunguzieni, na anajua kuwa upo udhaifu kwenu. Kwa hivyo wakiwa wapo watu mia moja kati yenu wenye kusubiri watawashinda mia mbili. Na wakiwapo elfu moja watawashinda elfu mbili, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri”

[Al-Anfal: 66]

8. Ya saba ni kuwasingizia wanawake walio safi na kuwasingizia uchafu na uwongo. Na wanawake wasafi; ni wanawake wasafi Waumini, basi hutoka katika hayo kumtukana mwanamke kafiri na mwanamke mzinifu aliyeteremshiwa uzinzi.

Amesema Mwenyezi Mtukufu: “

Hakika wanao wasingizia wanawake, wanao jihishimu, walio ghafilika, Waumini, wamelaaniwa duniani na Akhera, nao watapata adhabu kubwa” .

[An-Nur: 23]

Na hili halikomei katika kuwakashifu wanawake tu, bali ni pamoja na wanaume pia, kwa hivyo kumkashifu Muumini msafi ni kama kumkashifu mwanamke msafi katika kuwajibikiwa na adhabu ya hadd na kustahiki adhabu huko Akhera bila ya kutofautiana baina ya wanachuoni [7] Kuwataja wanawake wema haimaanishi kuwa mwanamke asiyekuwa mwema kwamba inafaa kumkashifu, au kumkashifu sio dhambi kubwa, bali anaiwekea mipaka katika hilo ili kuzidisha madhambi, kwani anamkashifu mwanamke Muumini. asiye na hatia ya kile kinachohusishwa naye, lakini badala yake hajui chochote kuhusu hilo [8]

Mafunzo

1- Mlinganiaji na muelimishaji anatakiwa kuwa makini kuwaonya watu juu ya dhambi kubwa na sababu za ghadhabu na adhabu ya Mwenyezi Mungu.

2- Madhambi ya watu hufutwa kwa kutenda matendo mema. Kama ilivyo katika siku ya Ijumaa, ufuatiliaji baina ya Hijja na Umra, na kadhalika, isipokuwa madhambi makubwa, na kwa ajili ya hayo akasema Mtume rehma na Amani zimshukie: “Swala tano, na sala ya ijumaa hadi ijumaa, Na Ramadhani hadi Ramadhani, ni kafara ya yaliyo baina yao ikiwa yataepukika madhambi makubwa” [9] Basi jihadharini na yale yanayobatilisha malipo na hayaondoki kwa amali njema.

3- Kamwe usidharau dhambi kwa sababu sio dhambi kubwa. Dhambi ndogo, ikiwa mja akiidharau na kuiona ndogo, inakuwa kubwa, na Muumini anaona madhambi yake ni milima. Al-Fudayl Ibn Iyadh, Mwenyezi Mungu amrehemu, amesema: “Kadiri dhambi inavyokuwa ndogo kwa maoni yenu, ndivyo inavyokuwa kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, na kadiri inavyokuwa kubwa zaidi kwenu, ndivyo inavyokuwa ndogo zaidi kwa Mwenyezi Mungu”.[10] Ibn Masoud, radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie, amesema: “Muumini anayaona madhambi yake kana kwamba amekaa chini ya mlima akiogopa usimshukie, na muovu anaona madhambi yake ni kama nzi wanaopita juu ya pua yake naye akasema hivi (akaashiria kumfukuza)” [11] 

4- Jihadharini na ushirikina na sababu zake na njia zake; Kwani ni chanzo cha ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na adhabu yake, inaporomosha matendo mema, na ushirikina umefichika zaidi kuliko kutambaa kwa mdudu chungu.

5-Ukitaka usalama Siku ya Qiyaama ni lazima uiunganishe, na jihadhari na matokeo ya ushirikina. Ibn Masoud amesema: Ilipo teremka (aya hii):

“Wale ambao wameamini, na hawakuchanganya imani yao na dhulma - hao ndio watakao pata amani na wao ndio walio ongoka”

[Al-An'am: 82]

Tukasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni nani miongoni mwetu asiyejidhulumu nafsi yake? Alisema:

"Si kama mnavyosema, Wale ambao wameamini, na hawakuchanganya imani yao na dhulma”

[Al-An'am: 82]

Kwa ushirikina, je hamkusikia Luqman alivyomwambia mwanawe:

“Na Luqman alipo mwambia mwanawe kwa kumpa mawaidha: Ewe mwanangu! Usimshirikishe Mwenyezi Mungu. Kwani hakika ushirikina bila ya shaka ni dhulma iliyo kubwa”  

[Luqman: 13] [12]

6-Tahadhari usiende kwa mchawi au mpiga ramli; Kwani huko ni kumkufuru Mwenyezi Mungu, Mtume amani iwe juu yake, amesema: “Mwenye kwenda kwa mtabiri au mchawi na akaamini anayoyasema, basi amekufuru yaliyoteremshwa kwa Muhammad, amani iwe juu yake.” [13]

7- Kujifunza uchawi na kuufundisha ni kumkufuru Mwenyezi Mungu, basi epukeni uchawi.

8- Ni wajibu kwa wenye mamlaka kuwawekea adhabu wachawi, wapiga ramli na makohani ili watu wengine wasiwaige na kuhuisha maovu yao.

9- Kuua nafsi kwa dhulma ni dhambi kubwa. Mwenyezi Mungu Alimuahidi adhabu iumizayo. Bali Mtume, Rehema na Amani zimshukie, ameeleza kuwa madhambi yote yamo katika matashi isipokuwa shirki na kuua. Ili kutishia na kuzuia, amesema Mtume amani iwe juu yake: “Mwenyezi Mungu husamehe kila dhambi; Isipokuwa mtu amuue Muumini kwa kukusudia, au mtu huyo afe akiwa kafiri” [14]

10- Ghadhabu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu huwa kali zaidi juu ya mtu, anaye muua Muumini kwa kukusudia bila ya haki, na ndio maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akamwandalia adhabu kali tofauti na wakosefu wengine, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:

“Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa” .

[An-Nisaai: 93]

11- Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake wamemwonya mla riba kwa kumtangazia vita ikiwa hataachana nayo, Je, unaweza kupigana nao?

12- Akasema Swalla Allaahu alayhi wa sallam: “Niliwaona usiku watu wawili walionijia, wakanipeleka kwenye nchi takatifu, Basi tukasafiri mpaka tukafika kwenye mto wa damu, ambamo mtu alikuwa amesimama, na katikati ya mto huo kulikuwa na mtu mwenye mawe mikononi mwake. Basi yule mtu akawa anamuelekea yule aliye katika mto, yule mtu alipotaka kutoka, yule mtu anamrushia jiwe mdomoni na kumrudisha pale alipokuwa. Ikawa Kila anapotaka kutoka nje, alimrushia jiwe, naye anarudi alivyokuwa. Kwa hivyo nikasema hii ni nini? Akasema: Uliyemuona mtoni ni Mla riba”.[15]

13- Jihadharini na kula pesa za watu kwa dhulma, kwani hiyo ni dhambi kubwa, haswa ikiwa mwenye pesa ni dhaifu au yatima ambaye hana uwezo wa kulinda pesa yake.

14- Tahadhari na madhara ya kula pesa za yatima; ni moja ya madhambi yanayoangamiza.

15- Ukiingia vitani na Waislamu kupigana na makafiri, basi mtegemee Mwenyezi Mungu na umwamini yeye, na fahamu kwamba uko katika mipaka ya Uislamu, na isemeshe nafsi yako: Uislamu hautapigwa mbele yangu, na simama imara kwa msaada wa Mwenyezi Mungu.

16- Usiwe sababu ya hasara ya Waislamu kwa kuonyesha udhaifu na kushindwa, kwani hilo litawaathiri askari wote.

      17- Linda ulimi wako na yale yanayowaudhi watu. Ulimi ndio unaowaingiza watu wengi Motoni.

      18-Mwenyezi Mungu Mtukufu alichukua hadhari ya kuhifadhi heshima kwa kumwajibisha yeyote ambaye anaona watu wanafanya uchafu alete mashahidi wanne, vinginevyo ni mwongo na mchonganishi ambaye lazima apigwe viboko themanini. Usiruhusu ulimi wako kukupa rasilimali mbaya.

19- Inaingia katika kawakashifu, kutukanana Waislamu leo wao kwa wao hata kwa mzaha. Basi jihadhari na aina hiyo ya ucheshi; Hakuna neno unalotamka isipokuwa utawajibishwa nalo.

20- Mshairi alisema:

Wacha madhambi madogo na makubwa, kwani huo ndio uchamungu

Uwe kama mtu anayetembea juu ya miiba, mwenye tahadhari kwa kile anachokiona

Usidharau dhambi ndogo = kwani hata milima inatokana na  kokoto

    21- Wengine walisema:

Na miongoni mwa watu, wapo waliozoea kudhulumu = na kujipatia udhuru wa kufanya hivyo

kathubutu kula haramu na kudai = kwamba ana sababu yake ya kufanya hivyo

Ewe unayekula mali ya haramu, tueleze = ni kitabu gani kichohalalisha mnachokula? Je, hujui kwamba Mwenyezi Mungu anajua yaliyotokea = na siku ya kiyama atahukumu kati ya waja.


Marejeo

1. Imepokewa na Al-Bukhari (4477) na Muslim (86).

2.Tazama: “Bada’a al-Fawa’id” cha Ibn al-Qayyim (2/ 760).

3. Imepokewa na Al-Bukhari (67) na Muslim (1679), kwa kutoka kwa Abu Bakra, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi.

4. Imepokewa na Al-Bukhari (3166).

5. Tazama: Muntaha al-Iradat cha Ibn al-Najjar (2/347).

6. Imepokewa na Muslim (1598).

7. Tazama: “At-Tawdhid li Sharh al-Jami’ al-Sahih” cha Ibn al-Mulqqin (31/284).

8. Tazama: “Fath Al-Mun’im Sharh Sahih Muslim” cha Musa Shaheen Lashin (1/ 291).

9. Imepokewa na Muslim (233).

10. “Siyar A’lam al-Nubala” cha al-Dhahabi (8/427).

11. Imepokewa na Al-Bukhari (6308).

12. Imepokewa na Al-Bukhari (3360) na Muslim (124).

13. Imepokewa na Abu Dawood (3904), Al-Tirmidhiy (135), Al-Nasa’i (9017), na Ibn Majah (639).

14. Imepokewa na Al-Nasa’i (3984).

15. Imepokewa na Al-Bukhari (2085).


Miradi ya Hadithi