عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، عَنِ النَّبِيِّ ﷺ قَالَ: «إِنَّ اللَّهَ تَجَاوَزَ عَنْ أُمَّتِي مَا حَدَّثَتْ بِهِ أَنْفُسَهَا، مَا لَمْ تَعْمَلْ أَوْ تَتَكَلَّمْ»
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، عَنِ النَّبِيِّ ﷺ قَالَ: «إِنَّ اللَّهَ تَجَاوَزَ عَنْ أُمَّتِي مَا حَدَّثَتْ بِهِ أَنْفُسَهَا، مَا لَمْ تَعْمَلْ أَوْ تَتَكَلَّمْ»
Kutoka kwa Abu Huraira, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kutoka kwa Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam ambaye amesema: “Mwenyezi Mungu ameusamehe umma wangu kwa yale waliyojisemea ndani ya Nafsi maadamu haukufanya wala kusema.”
Amesema Mwenyezi Mungu:
“Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito”
[Al-Baqara: 185].
Na akasema Mola aliyetukuka:
“Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo. Faida ya iliyo yachuma ni yake, na khasara ya iliyo yachuma ni juu yake pia”
[Al-Baqara: 185].
Pia amesema Mwenyezi Mungu mtukufu:
“Mwenyezi Mungu anataka kukupunguzieni taabu, na mwanaadamu ameumbwa dhaifu” .
[An-Nisa: 28]
Mwenyezi Mungu anasema:
“Wala Mwenyezi Mungu hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini”
[Al-Hajj: 78].