1- Mwenyezi Mungu Mtukufu anaamrisha kufanya ihsani katika kila jambo. Akasema, Mwenyezi Mungu:
“Na fanyeni wema, hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema”
Na wema maana yake ni: kutenda kitu kwa ufanisi zaidi, na hayo ni pamoja na mambo yote ya kimaisha; Katika ibada: kuMuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu, kana kwamba unamuona, na kujifanyia wema usijitafutie moto, na usijitwike usichoweza kubeba, na kuwatendea watu ni kuishi nao katika misingi ya maadili ya Uislamu; Basi usimdhulumu yeyote, wala usichukue haki za watu, na ishi nao kwa wema, basi vizuri na wale wanaokufanyia wema nawe uwalipe wema, na kuwasamehe waliokudhulumu, wala usiwalipe ubaya kwa ubaya.
Na wema ulioamrishwa upo katika aina mbili: wajibu, ambao ni uadilifu na kukiweka kitu mahala pake, na kumpa kila mwenye haki haki yake, na kutekeleza wajibu wako. Na aina ya pili ni sunnah, ambayo ni kuwapa watu manufaa ya kimwili, kifedha au kielimu, na kuwaelekeza kwenye yale yatakayowanufaisha duniani na Akhera, na kila wema ni sadaka.
2- Basi kufanya jambo kwa uzuri ni wajibu hata katika kuua nafsi, hivyo haijuzu kumwaga damu ya mwanaadamu, Mwislamu au kafiri, bila ya uhalali. Bali ikilazimika kuuawa lazima itumike njia nzuri ya kumuua, hateswi hadi kufa, wala hauwawi kwa sumu au kupigwa kwa kitu kisichoua na kuachwa mpaka afe, bali humchagulia njia nyepesi na isiyo chungu zaidi.
Na Sharia imemtenga mwenye kueneza ufisadi katika ardhi inapowekwa juu yake adhabu ya utekaji na ujambazi. Ni kwa lengo la kumkemea na kuwatisha wengine wasifanye alichofanya.
Pia kulipiza kisasi kwa mauaji ni jambo ambalo liko tofauti. Ambapo muuaji anauawa kama alivyoua; Iwapo aliuwa kwa sumu, au kwa kupiga risasi, au kwa kutupwa kutoka mahali pa juu, au vinginevyo, ndivyo atavyofanyiwa muuaji. Mwenyezi Mungu Mwenye kutakasika amesema:
“Na mkilipiza basi lipizeni sawa na vile mlivyo adhibiwa. Na ikiwa mtasubiri, basi hakika hivyo ni bora zaidi kwa wanao subiri” ,
na Myahudi alimuuwa kijakazi huko Madina kwa jiwe, basi Mtume, rehema na amani zimshukie, akamleta na akampiga kichwa chake kati ya vijiwe viwili [1]
Pia na katika kufanya vizuri katika kuua kwamba maiti isikatwekatwe viungo vyake, wala hadhulumiwi au ikakusudiwa kuifurahisha nafsi katika kitendo hicho ; Haya ni kutokana na kupetuka mipaka katika kuua, ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu ameyakataza pale aliposema:
“Na aliye uliwa kwa kudhulumiwa basi tumempa madaraka mrithi wake. Lakini asipite mpaka katika kuuwa. Kwani yeye anasaidiwa”.
3- Pia ni lazima kufanya wema katika kuchinja mnyama, haijuzu kamwe kuchinja mnyama kwa makusudio mengine tofauti na kumla, na wala haijuzu kumchukua mnyama kuwa shabaha wanayoitupa watu kwa ajili ya burudani au mashindano.Abdullah bin Omar, Allah awe radhi nao wote wawili, amesema:
“Hakika Mtume rehma na amani zimshukie amemlaani mwenye kuchukua kitu ambacho kina nafsi kisha kukichezea”[2]
Basi akitaka kuchinja mnyama amchinje vizuri, asimburute mpaka sehemu ya kuchinja, wala asichinje mbele ya wanyama, na wala haanzi kwa kumchuna ngozi na kumkata kabla yake, haanzi kwa kuchuna ngozi na kuikata kabla haijapoa na roho yake kutoka. Bali, anafanya kile kinachosaidia kumliwaza mnyama na kutoa roho yake kwa urahisi bila kusababisha maumivu, kwa hiyo ananoa ubao au kisu anachochinjia, na kuchagua hali nzuri itayompa faraja. Na akate mishipa ya shingo, koo, ili kurahisisha kutoka kwa roho, kisha anaiacha mpaka ipoe na roho itoke kabisa.
(1) Kwa aina za sadaka: Kuwafanyia wema waliokudhulumu, Mwenyezi Mungu Mtukufu kataja kuwa hiyo ni daraja kubwa watakayoifikia wale walio na bahati kubwa ya imani na subira. Mwenyezi Mungu anasema:
“Ondosha uovu kwa lililo jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu (34) Lakini hawapewi wema huu ila wanao subiri, wala hawapewi ila wenye bahati kubwa”
2- Malipo ni kutegemeana na kitendo, basi fanyeni wema na Mwenyezi Mungu Mtukufu atakutendeeni wema
”Malipo ya matendo mema ni wema” .
3- Katika aina za ulazima wa kufanya wema: ni kutenda wema kwa jamaa; Kwa kuwasahihisha, kuwafanyia wema, kuwachunga mambo yao, na kuwatimizia mahitaji yao.
4- Miongoni mwa mambo ya lazima kwa muislamu kuyafanya kwa uzuri zaidi: Ni kutekeleza wajibu na kuacha makatazo; Anatekeleza majukumu kwa ukamilifu, bila upungufu katika nguzo na yaliyo wajibu, na anaacha makatazo na njia zinazo mpelekea huko.
5- Iwapo mtu ataamrishwa kufanya wema katika kumuua ambaye ni lazima auwawe, basi hapana shaka kwamba kuhifadhi damu ya watu na kuiharamisha, na kujitahidi kuilinda ni miongoni mwa aina za lazima kuzitenda kwa uzuri.
6- Miongoni mwa kufanya vizuri katika kuua, tusiwatusi waliouawa kwa kutekelezewa adhabu kisharia au kulipiziwa kisasi, na amesema Mtume rehma na amani zimshukie kuhusu mwanamke aliyepigwa mawe katika uzinifu wakati Khalid bin Al-Walid Mwenyezi Mungu awe radhi naye alipomtusi
“Subiri, ewe Khalid, ninaapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu imo mkononi Mwake, hakika (mama huyu) ametubu toba ambayo, lau mkusanya kodi za dhulma angetubia, angesamehewa” [3]
7- katika kuchinja vizuri ni kusimamiwa na mwenye kufanya vizuri, na si kila mtu anafanya hivyo.
8- Iwapo mnataka kuchinja, basi mshukuruni Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa neema alizokuruzukuni, kama alivyo kufanyieni katika wanyama wa mifugo ambayo angelitaka asingeli watiisha wanyama hao.
9-Hakikisha unatumia kisu kikali, na kumtenga mnyama anayechinjwa na wanyama wengine, na kuweza kumdhibiti asikukimbie wakati wa kuchinja na kupata maumivu, na fanya hima kumchinja na kutomuonyesha kisu kabla ya kuchinja, na kukata shingo, koo na umio, kwani kufanya hivyo kunaondowa roho haraka.
10- Amesema Mshairi:
Watendee wema watu utaitumikisha mioyo yao = kwani wema unamfanya mtu kuwa mtumwa
Afanyaye wema kwa watu katika mali yake watu wote = humfuata, na pesa ni fitna kwa watu.
Watendee watu mazuri ikiwa uwezo unao = kwani uwezo huwa haudumu kwa watu.
Marejeo
- Imepokewa na Al-Bukhari (5295) na Muslim (1672).
- Imesimuliwa na Muslim (1958).
- Imesimuliwa na Muslim (1695).