عَنِ ابْنِ عُمَرَ - رضي اللَّه عنهمَا - قَالَ: «فَرَضَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ زَكَاةَ الفِطْرِ صَاعًا مِنْ تَمْرٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ شَعِيرٍ، عَلَى العَبْدِ وَالحُرِّ، وَالذَّكَرِ وَالأُنْثَى، وَالصَّغِيرِ وَالكَبِيرِ مِنَ الْمُسْلِمِينَ، وَأَمَرَ بِهَا أَنْ تُؤَدَّى قَبْلَ خُرُوجِ النَّاسِ إِلَى الصَّلاَةِ».

Kutoka kwa Ibn Umar – Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili – amesema:

1. “Mtume wa Mwenyezi Mungu amani iwe juu yake amefaradhisha zakatul-Fitri. 2. Pishi ya tende, au pishi ya Dengu, 3. Juu ya Muislamu mtumwa na aliyehuru, mwanamume na mwanamke, mdogo na mkubwa. 4. Na akaamrisha itolewe kabla ya watu kutoka kwenda kuswali.





Muhtasari wa Maana

Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, amesema kuwa Zakaatul-Fitri hutolewa kutoka kwa kila Mwislamu, mwanamume au mwanamke, huru au mtumwa, mdogo au mkubwa, kwa kila mtu pishi ya chakula, na hutolewa kabla ya kusali sala ya Iddi

Miradi ya Hadithi