عَنْ طَارِقِ بْنِ شِهَابٍ قَالَ: أَوَّلُ مَنْ بَدَأَ بِالخُطْبَةِ يَوْمَ العِيدِ قَبْلَ الصَّلاةِ مَرْوَانُ، فَقَامَ إِلَيْهِ رَجُلٌ، فَقَالَ: الصَّلاةُ قَبْلَ الخُطْبَةِ، فَقَالَ: قَدْ تُرِكَ مَا هُنَالِكَ فَقَالَ أَبُو سَعِيدٍ رضي الله عنه: أَمَّا هذَا فَقَدْ قَضَى مَا عَلَيْهِ؛ سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ ﷺ يَقُولُ: «مَنْ رَأَى مِنْكُمْ مُنْكَرًا فَلْيُغَيِّرْهُ بِيَدِهِ، فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبِلِسَانِهِ، فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبِقَلْبِهِ، وَذَلِكَ أَضْعَفُ الإِيمَانِ»

Kutoka kwa Tariq bin Shihaab amesema:

Mtu wa kwanza aliyeanza khutba ya siku ya Idi kabla ya swala ni Marwan, na mtu mmoja akasimama karibu naye na kumwambia: “Swala ni kabla ya khutba.” Akasema, “Kilichopo kimeachwa. Amesema Abu Said Radhiya Allaahu anhu: Ama mtu huyu ametimiza wajibu wake. Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na Amani zimshukie akisema: “Yeyote miongoni mwenu anayeona kitendo kiovu, basi na akibadilishe kwa mkono wake. Ikiwa hawezi, basi kwa ulimi wake. Ikiwa hawezi, basi kwa moyo wake, na hiyo ndiyo imani dhaifu zaidi”

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana


Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu:

 “Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa  kwa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu”

[Al Imran: 110].

Amesema utukufu ni wake:

“Walilaaniwa walio kufuru miongoni mwa Wana wa Israili kwa ulimi wa Daud na wa Isa mwana wa Maryamu. Hayo ni kwa sababu waliasi na wakawa wanapindukia mipaka (78) Walikuwa hawakatazani maovu waliyo kuwa wakiyafanya. Hakika ni maovu yalioje mambo waliyo kuwa wakiyafanya”

[Al-Maida: 78, 79].

Mwenyezi Mungu aliyetukuka akasema:

 “Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi. Huamrisha mema na hukataza maovu, na hushika Sala, na hutoa Zaka, na humt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao Mwenyezi Mungu atawarehemu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mtukufu Mwenye nguvu, Mwenye hikima”

[Al-Tawba: 71].

Miradi ya Hadithi