عن أبي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ يَقُولُ: «جَعَلَ اللهُ الرَّحمةَ في مِائَةِ جُزْءٍ، فَأَمْسَكَ عِنْدَهُ تِسْعَةً وَتِسْعِينَ جُزْءًا، وَأَنْزَلَ فِي الأرْضِ جُزْءًا وَاحِدًا، فَمِنْ ذَلِكَ الجُزْءِ يَتَرَاحَمُ الخَلْقُ، حَتَّى تَرْفَعَ الفَرَسُ حَافِرَهَا عَنْ وَلَدِهَا؛ خَشْيَةَ أَنْ تُصِيبَهُ» متفق عليه

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhi za Mwenyezi Mungu Ziwe Juu Yake) amesema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma Na Amani Zimshukie) akisema:

1. “Mungu amejalia huruma katika mafungu mia moja, 

2. kisha akabakiza kwake sehemu tisini na tisa (za huruma) na akateremsha ardhini sehemu moja tu. 

3. Kutokana na sehemu hiyo viumbe uhurumiana, (kiasi kwamba) farasi hunyanyua kwato yake kwa mtoto wake kwa kuogopea asimkanyage) .” imepokelewa na Bukhari Na Muslim .


1- Ameeleza Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake) kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amegawanya huruma katika sehemu mia moja.

Na sentensi hii inamaana ya kusogeza karibu ufahamu kutoka kwa Mtume (Rehema Na Amani Za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake), na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi jinsi ilivyo, lakini kinachokusudiwa ni kwamba kuna huruma nyingi ambazo Mwenyezi Mungu Mtukufu amezitayarisha kwa ajili ya waja wake, na kilichokusudiwa hapa ni kutufanya tutambue kuwa huruma yetu vyovyote itakavyokuwa itabaki kuwa ndogo na ya chini, na huruma ya Mwenyezi Mungu .ndio iliyojuu kuliko huruma ya yeyote [1]

2- Kisha Mtume (Rehema Na Amani Za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) akabainisha hayo kwa kusema kwamba asilimia tisini na tisa ya rehema hizo zitakuwa huko Akhera kwa waja wake, na kwamba yote tunayoyaona hapa duniani yanatokana na athari za rehema; Kama huruma ya mama kwa mtoto wake, na watu kuhurumiana na kusameheana baina yao, na hata wanyama kwani ni mengi tunayojua kutoka kwao (katika matukio ya kuhurumiana) na tusiyojua, yote hayo yanatoka katika sehemu hiyo ya huruma ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu ameiteremsha kwetu.

Ikiwa tunayoyaona hapa duniani katika huruma yamepatikana kutoka katika sehemu moja kati ya sehemu mia moja za huruma, basi itakuwa vipi sehemu nyingine ambazo Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaandalia waja wake huko Akhara...? huruma hizo zimehifadhiwa na kutunzwa Kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu hadi Siku ya Kiyama,  Siku hiyo watu watapata rehema nyingi zaidi kuliko matendo waliyoyafanya duniani, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu atawasitiri na kuwasemehe, kuwafanyia wepesi ili wasameheana.

3- Kisha akatoa mfano wa huruma aliyoiteremsha Mwenyezi Mungu kwa waja wake, nayo ni kwamba wanyama na Wanyama mwituu wanahurumiana wao kwa wao, kiasi kwamba mnyama mwitu hawezi kumla mwanawe, halikadhalika farasi jike licha ya kasi yake na uwepesi wa harakati zake: huinua miguu yake kwa mtoto wake ili asimdhuru.
Na huu ni mfano mdogo katika mifano ya sehemu hii moja ya (huruma), na kwayo unadhihirika upana wa rehema ya Mwenyezi Mungu.

Mafunzo

Tunajifunza katika hadith hii yafuatayo: -

1- Rehema ya Mwenyezi Mungu ni pana, kiasi kwamba ana rehema iliyoenea kwa viumbe wote, na rehema kubwa na kamili ambayo ni maalum kwa wachamungu wenyeimani,

Mwenyezi Mungu amesema:

“Na rehema yangu imekizunguka kila kitu, kwa hivyo nitawaandikia wale wachamungu na wenyekutoa zakah, na wale ambao wanaamini alama(aya) zetu.” 

[Al-A`ARAAF: 156]

Yeyote anayetaka kupata ujira huo mwingi kutoka katika rehema za Mwenyezi Mungu, basi na afanye haraka kufuata njia ya waja wa Mwenyezi Mungu wema, na achunge mipaka yake, na kufuata amri zake, na ajiepushe na yale aliyoharamisha Mwenyezi Mungu.

2- Ikiwa wanyama na wanyama mwitu ambao Mwenyezi Mungu hakuwapa akili na hekima wanahurumiana wao kwa wao, basi vipi kuhusu yule ambaye moyo wake umeondolewa rehema?! Hakika asiehurumia hatohurumiwa.

3- Kila unapoona Mwenyezi Mungu Mtukufu anakupa mitahani au kumpa mtihani mja kwa balaa au matatizo, basi ujue kwamba hii inatokana na hekima yake kubwa, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu hapungukiwi na rehema, 
Na unapoona Mwenyezi Mungu Mtukufu amemlaani mtu au kumuhukumu kuingia motoni milele, basi jua kwamba mtu huyo anastahili.

4- Usihuzunike kwa madhara yaliyokusibu, kwani rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni pana sana, na iko karibu kwa waja wake wanyonge wanaoitafuta kwake, na wakawa na dhana nzuri kwake.

5- Mola Mlezi Mwenye huruma huteremsha huruma hizo kiasi kinachoweza kunyoosha Maisha yetu, na hubakiza na kututunzia katika huruma hizo, tutakazohurumiana kwazo siku ambayo haitofaa mali wala pesa, bali tutalipizana kwa mema na mabaya,
Na aliefilisika ni yule ambaye kulipizana (kisasi) kutamaliza matendo yake mema, matendo mabaya yakawa mengi,

Kisha zitachukuliwa zile dua ambazo Malaika wanatuombea kwa Mwenyezi Mungu ikiwemo: Kutuombea rehma na msamaha na kunyanyuliwa daraja. Na kubwa zaidi ni kwamba baada ya hayo atatusamehe madhambi yetu na kutusamehe mapungufu yetu katika kuMuabudu  Yeye na kutekeleza amri zake. 
Hakika Mtu anayepuuza kumshukuru Mwenyezi Mungu na kurejea kwake baada ya kujua haya basi atakuwa ni mzembe aliepata hasara.

6- Mshairi anasema:
Kwako, Mungu wa Uumbaji, ninainua maombi yangu,,,,, hata kama nikiwa muovu, Ewe Mwenye neema na Ukarimu.

Moyo wangu ulipokuwa mgumu, na nikakosa pa Kwenda, nkafanya matarajio yangu kuwa ni ngazi ya kufufikia msamaha wako.
Dhambi yangu iliongezeka, nilipo zilinganisha na msamaha wako, msamaha wako ulikuwa mkubwa Zaidi kuliko chochote.
Na bado unasamehe dhambi = na Wewe ni mkarimu unaesamehe.

Marejeo

  1. Tazama: “Sharh Sahih Al-Bukhari” Cha Ibn Battal (9/213-214), “Irshad Al-Sari” Cha Al-Qastalani (9/19).


Miradi ya Hadithi