عَنْ طَلْحَةَ بْنِ عُبَيْدِ اللهِ رضي الله عنه قَالَ:جَاءَ رَجُلٌ إِلَى رَسُولِ اللهِ مِنْ أَهْلِ نَجْدٍ، ثَائِرُ الرَّأْسِ، يُسْمَعُ دَوِيُّ صَوْتِهِ، وَلَا يُفْقَهُ مَا يَقُولُ، حتَّى دَنَا، فَإِذَا هُوَ يَسْأَلُ عَنِ الإِسْلامِ،فَقَالَ رَسُولُ اللهِ : «خَمْسُ صَلَوَاتٍ فِي اليوْمِ وَاللَّيْلَةِ»، فَقَالَ: هَلْ عَليَّ غَيْرُهَا؟ قَالَ: «لَا، إِلَّا أَنْ تَطَّوَّعَ».قَالَ رَسُولُ اللهِ : «وَصِيَامُ رَمَضَانَ»، قَالَ: هَلْ عَليَّ غَيْرُهُ؟ قَالَ: «لَا، إِلَّا أَنْ تَطَّوَّعَ».قَالَ: وَذَكَرَ لَهُ رَسُولُ اللهِ الزَّكَاةَ، قَالَ: هَلْ عَليَّ غَيْرُهَا؟ قَالَ: «لَا، إِلَّا أَنْ تَطَّوَّعَ».قَالَ: فَأَدْبَرَ الرَّجُلُ وَهُوَ يَقُولُ: وَاللهِ، لَا أَزِيدُ عَلَى هَذَا وَلا أَنْقُصُ. قَالَ رَسُولُ اللهِ : «أَفْلَحَ إِنْ صَدَقَ». وفي رِوايةٍ: «دَخَلَ الجَنَّةَ إِنْ صَدَقَ»

Kutoka kwa Talha bin Ubaydillah Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yakeamesema:

  1- Alikuja mtu mmoja katika watu wa Najd kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani ziwe juu yake), Sauti yake inasikika, lakini haeleweki anachosema, mpaka akakaribia, kumbe anauliza kuhusu Uislamu  2- Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani ziwe juu yake): "Swala tano kwa mchana na usiku", akasema: Je, ni lazima nifanye jambo lingine? Akasema: “Hapana, isipokuwa ukijitolea”.  

3- Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani ziwe juu yake): "Na Saumu ya Ramadhani", akasema: Je, ni lazima nifanye jambo lingine? akasema: “Hapana, isipokuwa ukijitolea”.  

4- (Talha bin Ubaydillah ) Akasema: Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani ziwe juu yake), akamtajia Zaka, akasema: Je, ni lazima nifanye jambo lingine? akasema: Hapana, isipokuwa ukijitolea.  

5- (Talha bin Ubaydillah ) Akasema: Basi yule mtu akageuka na kusema: Wallahi siwezi kuongeza wala kupunguza katika haya.  

6- Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani ziwe juu yake): "Atafaulu ikiwa ni mkweli." Na katika riwaya nyingine: “Ataingia Peponi ikiwa anasema kweli. 

Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Mwenyezi Mungu anasema: 

“Na shikeni Swalah na toeni Zaka; na kheri mtakazo jitangulizia nafsi zenu mtazikuta kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yafanya” . 

[Al-Baqarah: 110]

Mwenyezi Mungu alisema: 

“Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi atakaye udiriki mwezi huu naafunge”  

[Al-Baqarah: 185]

Mwenyezi Mungu amesema: 

“Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe na uwatakase kwazo”

[At-Tawbah: 103]. 

Mwenyezi Mungu alisema: 

“Shika Swalah jua linapo pinduka mpaka giza la usiku, na Qur'ani ya al fajiri. Hakika Qur'ani ya alfajiri inashuhudiwa daima (78) Na amka usiku kwa ibada; ni ziada ya sunna khasa kwako wewe. Huenda Mola wako Mlezi akakunyanyua cheo kinacho sifika”  

[Al-Isra: 78, 79]

Mwenyezi Mungu alisema:

  “Na atakaye fanya wema kwa kujitolea, basi ni bora kwake” . 

[Al-Baqarah: 184]

Miradi ya Hadithi