عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ - رضي اللَّه عنهمَا - أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ قَالَ: «مَا حَقُّ امْرِئٍ مُسْلِمٍ لَهُ شَيْءٌ يُوصِي فِيهِ، يَبِيتُ لَيْلَتَيْنِ إِلَّا وَوَصِيَّتُهُ مَكْتُوبَةٌ عِنْدَهُ»



Kutoka kwa Abdullah bin Omar – Mwenyezi Mungu awawie radhi wote wawili – kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake amesema: “Si haki ya Muislamu mwenye kitu cha kuweza kuusia. Anakaa siku mbili bila wasia wake kuandikwa pamoja naye.”

Inajuzu kwa mtu kutumia sehemu ya mali yake na wasia ni sehemu yake, kwa sharti isizidi thuluthi, na wasia huo usimlenge mwenye kurithi; kwa kauli ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Mwenyezi Mungu alikupeni theluthi ya mali yenu iwe ni sadaka siku ya kufa kwenu, ili kuongeza matendo yenu mazuri” [1] Na Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akasema: “Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na Aliye Juu, amempa kila mtu haki yake, kwa hivyo hakuna wosia kwa mwenye kurithi” [2] Pengine mwanamume huyo anataka kuusia baadhi ya pesa zake kwa jamaa ambao hawarithi, au anataka kutoa sadaka kutoka katika fedha zake.

Ndio maana Mtume Rehema na Amani zimshukie, alimwamrisha kila anayetaka kuusia kitu katika fedha zake achukue hatua ya kuandika wosia wake, ili siku moja au mbili zisipite pasina kuwepo wasia wake wa maandishi; Hajui kwamba mauti yaweza kumjia ghafla na kumzuwia na alichokuwa akitaka. Wema waliuotangulia walilifanya jambo hili kuwa ni maalumu kwa wagonjwa na wale walio karibu na kifo, lakini kwenye hadith ni ishara inayoonyesha kuwa jambo hili ni maalumu kwa watu hao tu, ili kuendelea kufuata tabia ya kufanya hivyo [3] 

Hata hivyo, taratibu za kisheria juu ya wosia katika asili zinatofautiana kulingana na anayeusiwa; Huenda ikawa ni wajibu, kama mtoa wosia atakuwa anadaiwa deni ambalo warithi hawalijui, hasa ikiwa mdai hana ushahidi unaojulikana juu ya hilo; Kama mdaiwa asipoelekeza usia kwake, basi haki ya mdai ingepotea. Na Huenda wosia ukawa ni haramu, kama kuusia kitu kilichoharamishwa. Kama kuusia katika maasi, ama kama wosia kwa mrithi. Pia wosia unaweza kuwa ni sadaka au Sunnah, kama kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu au kuwausia jamaa ambao si warithi.


1. Muislamu lazima kila wakati akumbuke kifo, na kukipa kipaumbele, hivyo anafanya kazi kwa wakati huu na wala hakimshughulishi na starehe na matamanio ya dunia. Al-Hasan, Mwenyezi Mungu amrehemu, alisema: Mauti yamefungwa kwenye nyusi zenu, na dunia imekunjwa nyuma yanu. [4]

2. Mwenyezi Mungu alietakasika amehusika kugawanya mirathi yeye mwenyewe, basi haijuzu kwa Muislamu kubishana na Mola wake Mlezi juu yao, au kudhani kuwa mgawanyo wake ni bora kuliko mgawanyo wa Mwenyezi Mungu hakimu wa mahakimu.

3. Mwenyezi Mungu Mtukufu amewafadhilisha waja wake thuluthi ya fedha zao, na wanazitumia wapendavyo kwa kutoa wosia, basi mwenye hekima ni yule anayeitumia neema hiyo katika radhi na utiifu wa Mwenyezi Mungu.  na anatoa kiwango hicho katika njia Yake.

4. Muislamu afanye hima kuandika wosia wake - ikiwa ana jambo analotaka kulifanya - kabla ya ulimwengu kumsahaulisha, au maradhi yakamfanya kuwa kilema, au kifo cha ghafla. Maswahaba, Mwenyezi Mungu awawie radhi, wakachukua hatua, kwani Ibn Umar, Mwenyezi Mungu awawie radhi, msimuliaji wa hadithi hii anasema: “Hakuna usiku uliopita tangu nilipomsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehma na Amani ziwe juu yake, akiyasema hayo isipokuwa nimeuandika wosia wangu [5].

5. Kuruhusiwa kutoa sadaka na kuusia theluthi haimaanishi kuwa hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kutoa kiwango kigine tofauti na hicho, au kwamba wasia ulio bora zaidi ni wasia wa theluthi, yaani moja ya tatu. Jambo bora kabisa ni kuwaacha warithi wakijitosheleza na hawahitaji msaada kwa watu, na ndio maana Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, alimwambia Saad bin Abi Waqqas, alipotaka kutoa wosia wa nusu ya mali yake: “Toa wosia wa moja ya tatu, na hiyo ni nyingi; Ni afadhali warithi wako wawe matajiri kuliko kuwaacha wakiwa ombaomba (masikini)” [6] Ndio maana Ibn Abbas, Mungu awe radhi nao wote wawili, alikuwa akisema: Ni bora watu wakatoa wosia wa robo (moja ya nne) kuliko theluthi, na Abu Bakr as-Siddiq Mwenyezi Mungu amuwie radhi akausia khumsi (moja ya tano)  ya mali zake. Na akasema: Ninayaridhia aliyoridhia Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema:

“Na jueni ya kwamba ngawira mnayo ipata, basi khums (sehemu moja katika tano) ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume, na jamaa, na mayatima, na masikini, na wasafiri”.

[Al-Anfal: 41]

6. Wanachuoni wa elimu na wale wanaowaandikia watu wosia wao wawabainishie kuwa jambo hilo liko tofauti. Ikiwa warithi ni masikini na wanahitaji mali, ni bora kutotoa wasia, na ikiwa ni matajiri, inastahiki kwake kuusia theluthi moja au chini ya hapo, kulingana na hadhi ya warithi.

7. Mshairi amesema:

Kila wakati tunakisogelea kifo = na siku zetu zinakunjwa nazo ni vituo tu.

Na sijaona jambo la kweli mfano wa kifo= kanakwamba ni uongo, linapo gubikwa na matamanio.

Ni ubaya ulioje kwa kijana kuwa mzembe = na atakuwa na hali gani atapozeeka?!

Basi ondoka duniani ukiwa na uchamungu = hakika umri wako ni siku, nazo ni chache.

8. Mshairi Mwingine akasema:

Mali tunazozikusanya ni kwa ajili ya warithi = Na haya majumba yetu ni kwa ajili ya bundi tu.

Hakuna nyumba atayoishi mtu baada ya kufa = isipokuwa ile aliyoijenga kabla ya kufa Yeyote aliyeijenga vizuri, ataishi kwa starehe= na ataejenga kwa shari atahasirika sana.

Marejeo 

1. Imepokewa na Ibn Majah Na.: (2709).

2. Imepokewa na Abu Dawood (2870), Al-Tirmidhiy (2120), na Ibn Majah (2713).

3. Fath al-Bari cha Ibn Hajar (5/360).

4. “Jami’ al-Ulum wa al-Hakam” cha Ibn Rajab (2/382).

5. Imesimuliwa na Muslim (1627).

6. Imepokewa na Al-Bukhari (2742) na Muslim (1628).


Miradi ya Hadithi