عَنْ طَارِقِ بْنِ شِهَابٍ قَالَ: أَوَّلُ مَنْ بَدَأَ بِالخُطْبَةِ يَوْمَ العِيدِ قَبْلَ الصَّلاةِ مَرْوَانُ، فَقَامَ إِلَيْهِ رَجُلٌ، فَقَالَ: الصَّلاةُ قَبْلَ الخُطْبَةِ، فَقَالَ: قَدْ تُرِكَ مَا هُنَالِكَ فَقَالَ أَبُو سَعِيدٍ رضي الله عنه: أَمَّا هذَا فَقَدْ قَضَى مَا عَلَيْهِ؛ سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ ﷺ يَقُولُ: «مَنْ رَأَى مِنْكُمْ مُنْكَرًا فَلْيُغَيِّرْهُ بِيَدِهِ، فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبِلِسَانِهِ، فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبِقَلْبِهِ، وَذَلِكَ أَضْعَفُ الإِيمَانِ»

Kutoka kwa Tariq bin Shihaab amesema:

Mtu wa kwanza aliyeanza khutba ya siku ya Idi kabla ya swala ni Marwan, na mtu mmoja akasimama karibu naye na kumwambia: “Swala ni kabla ya khutba.” Akasema, “Kilichopo kimeachwa. Amesema Abu Said Radhiya Allaahu anhu: Ama mtu huyu ametimiza wajibu wake. Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na Amani zimshukie akisema: “Yeyote miongoni mwenu anayeona kitendo kiovu, basi na akibadilishe kwa mkono wake. Ikiwa hawezi, basi kwa ulimi wake. Ikiwa hawezi, basi kwa moyo wake, na hiyo ndiyo imani dhaifu zaidi”

Muhtasari wa Maana

Haifai kwa Muumini kuona uovu bila kuukemea. Akiweza kuubadilisha kwa mkono bila ya kupatikana majaribu wala madhara, atafanya, la sivyo atamkemea kwa ulimi wake na kumuusia mwenzake, la sivyo atakemea kwa moyo wake na kukasirika kwa ghadhabu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Miradi ya Hadithi