عنْ أبي هُرَيْرَةَ - رضي الله عنه - قال: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ: «إِنَّ اللَّهَ لَا يَنْظُرُ إِلَى أَجْسَادِكُمْ وَلَاإِلَى صُوَرِكُمْ؛ لَكِنْ يَنْظُرُ إِلَى قُلُوبِكُمْ». وَأَشَارَ بِأَصَابِعِهِ إِلَى صَدْرِهِ»


Kutoka kwa Abu Hurayrah – Mwenyezi Mungu amuwiye radhi – ambaye amesema:

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu alayhi wa sallam: 1. “Mwenyezi Mungu haangalii miili yenu wala sura zenu; 2.Lakini Yeye anazitazama nyoyo zenu. Na akaelekeza vidole vyake kwenye kifua chake



  1. Amesema Mtume Rehema na Amani zimshukie kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu hamfanyii hesabu mja kwa kuzingatia muonekano wake, wala muundo wake wa mwili; Hakuna tofauti kati ya mtu mweusi na mweupe. wala kati ya tajiri na maskini, wala kati ya wenye nguvu na dhaifu. Mtu anaweza kuwa na uso mzuri, mwili wa wastani, hoja kali, mwenye lugha tamu, Hata hivyo, hatapewa uzito mbele ya Mwenyezi Mungu, kama Mwenyezi Mungu alivyoelezea juu ya wanafiki,

Amesema Mola Mlezi na mtukufu kuhusiana na hali za wanafiki:

“Na unapo waona, miili yao inakupendeza, na wakisema, unasikiliza usemi wao”

[Al-munafiqun: 4].

  1. Mwenyezi Mungu anazingatia nyoyo; kwani ndio hazina ya uchamungu na imani, na tofauti ya kweli kati ya watu ni kwa uchamungu na matendo mema tu.

    Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

    “Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamungu zaidi katika nyinyi”

    [Al-Hujurat: 13]

    . Na amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: “Hakuna upendeleo kwa Mwarabu kuliko asiyekuwa Mwarabu, wala asiyekuwa Mwarabu kuliko Mwarabu. wala mwekundu kwa mweusi, wala mweusi juu ya mwekundu; Isipokuwa kwa uchamungu” [1].

Mja anaweza kuwa na sura na mwonekano mbaya, lakini ana hadhi kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu.Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake. “ Huwenda mtu ambaye nywele zake zimetimka hazikuchanwa, anayeweza kufukuzwa milangoni kwa watu kwa muonekano wake mbaya, lau angeliapa kwa Mwenyezi Mungu, bila ya shaka angelimtekelezea kiapo chake .”[2]

Hata hivyo, baadhi ya watu wanaitumia Hadith hii kubatilisha amali na wajibu wa faradhi. Inadaiwa kuwa moyo ukishiba imani, basi hakuna haja ya kutenda ibada za kimatendo. Haya ni madai ya uwongo. Matendo ni sehemu ya imani, na imani haifai kwa mtu yeyote asiye tenda matendo.

MAFUNDISHO

1-  (1) Hadithi inabainisha kuwa Mwenyezi Mungu hazingatii matukio, muonekano na sura hazihesabiki, hivyo mja asimuhukumu yeyote kwa sababu ya sura yake tu. Mionekano ni ya kudanganya.

2- (1) Hadith imesema kwamba mtu hatakiwi kujishughulisha na sura na mandhari kwani kufanya hivyo ni kuupumbaza moyo. Bali, anapaswa kujali mwili wake na mwonekano wake kwa kiasi, na kuelekeza mazingatio yake mengi kwenye yale yaliyo juu yake ambayo yanahesabiwa katika mizani. , ambayo ni kuusafisha moyo na kuwa na msimamo mzuri ndani ya moyo. 

3- (2) Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, alielekeza ulazima wa kuusafisha moyo na kuutakasa na uchafu, shubuha, na viingilio vya ushirikina na mapenzi ya dunia; hakika hapo ndipo macho ya Mwenyezi Mungu yanapotazama.

4- (2) Muislamu lazima awe na nia njema; kwa kuwa thawabu na adhabu yatatokana na nia. Muislamu anapaswa kuwa na subira katika kusahihisha na kubeba mateso ya hilo, kwani jambo hilo ni gumu. Wema waliotangulia walikuwa wakijifunza nia ya kutenda kama ambavyo mnavyojifunza kutenda [3].

5- (2) Tahadhari ya kurekebisha na kuusafisha moyo ni jambo la kwanza ambalo wale wanaomfuata Mwenyezi Mungu wanalitegemea. Hivyo Kuangalia maradhi ya moyo na kuyatibu ni jambo muhimu zaidi ambalo walishikamana nalo wema walioshika njia sahihi. Kwa maana moyo ukijumuika na viungo vingine ni kama mfalme anayefanya kazi kati ya askari wake. Hivyo kila litakalo tendeka litakuwa ni kwa amri ya Mfalme, na kufanya chochote anachotaka, kwani mambo yote yanakuwa chini yake. Pale mtu anapojaribu kuusafisha moyo wake huvuna msimamo mzuri, uadilifu na upotofu, kama ambavyo askari jeshi wanavyofuata amri za mfalme kwa lolote analolitaka, kwa kuwa yeye ni mmiliki mwenye mamlaka. [4].

6-(2) Kwa kutokana na nia ndio mtu anafaa kupata stahiki yake ya malipo mema au hata adhabu; Mtu anaweza kufanya jambo jema, lakini alilikusudia mtu mwingine tofauti na Mwenyezi Mungu Ataadhibiwa kwa hilo na hatalipwa, na pengine mtu alikusudia jambo la haki kisha akashindwa kulifanya. Atalipwa kwa ajili ya nia yake tu. Mtu lazima afanye upya nia yake nzuri, na kujitahidi kurekebisha nia yake.

 7- (2) Walinganiaji na waelimishaji waelekeze mazingatio na mtazamo wa watu juu ya kuulinda moyo na kutibu maradhi yake.

8- (2) Muislamu lazima afanye kazi kwa mizani inayompendeza Mwenyezi Mungu, ambayo ni upendeleo kwa misingi ya dini, imani na uchamungu, si sura, kiasi, mazungumzo mazuri, mali, heshima ya kijamii na mengineyo.

9- (2) Kigezo cha dini na uchamungu ndicho muhimu zaidi kwa Muislamu; Mwanamume achunge kigezo hicho ikiwa anatafuta mke, na mwanamke anayetaka kumuoa anapaswa kumtunza, na pia ikiwa mtu anataka mfanyakazi, mshirika, au mkazi wa kupanga nyumba yake, au kadhalika. lazima achague wachamungu na watu wa dini.

10- (2) Moyo unakuwa mgonjwa kama vile mwili unavyokuwa mgonjwa, na tiba yake ni kwa kutubia, unapata kutu kama kioo kikiungua, usafi wake unafanywa kwa ukumbusho, na uko uchi kama mwili unavyodhihirika, na pambo lake ni uchamungu, na moyo huwa unapata njaa na kiu kama mwili unavyopata njaa na kiu, na chakula chake na kinywaji chake ni elimu, upendo, kumtegemea mola mlezi peke yake, kutoa huduma, na uaminifu. [5]

11- (2) Katika kuashiria kwake Mtume juu ya kifua chake kitukufu, ni matumizi ya lugha ya mwili, na hili ni miongoni mwa mambo yanayomuathiri msikilizaji, na kutia habari ndani yake, hivyo ni vyema kutumia lugha ya mwili katika elimu, mwongozo na ulinganiaji.

12- Julaybib Mwenyezi Mungu awe radhi naye alikuwa miongoni mwa maswahaba wa Mtume (Rehma na Amani zimshukie) na alikuwa si mwenye muonekano mzuri na alikuwa mfupi,wakati flani Mtume alimshauri kuoa, nae akamwambia Mtume Rehema na Amani zimshukie : Naonekana ni mtu nisie na thamani ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mtume  amesema: “Lakini kwa Mwenyezi Mungu wewe ni mwenye thamani sana .” Basi akampeleka moja ya nyumba za watu wa madina aende kuongea na binti yao, na yule mtu na mkewe wakamstaajabu, lakini binti yao akachukua hatua ya kukubaliana na amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kisha Julaybib akatoka kuelekea katika jihadi. Basi Mtume (Rehma na Amani zimshukie) alimtafuta baada ya kumalizika vita, akamkuta ameuawa (kapata shahada), amezungukwa na washirikina saba aliowauwa, kisha nae akauawa, basi Mtume akasema: "Huyu ni katika mimi nami ni katika yeye" kwamaana yeye ni miongoni mwa watu wangu .Na mkewe kwa sababu ya kuolewa na Julaybib akawa ni miongoni mwa wanawake matajiri [6].

13-Mshairi akasema:

Waweza kumuona mtu mwembamba ukamdharau = na kumbe katika nguo zake kuna simba angurumaye.

Na aweza kukupendeza alie mzuri ukampenda , = kisha akwa kinyume na dhana yako huyo mzuri Hauwi tukufu wa watu ndio pambo kwao = lakini mapambo yao ni ukarimu na wema


Marejeo

  1. Imepokewa na Ahmad (23489).
  2. Imepokewa na Muslim (2622)
  3. .Ihya Ulum al-Din cha Abu Hamid al-Ghazali (4/364).
  4.   “Ighaath al-Lahfan min maswaaid shaitwan” cha Ibn al-Qayyim (1/5)
  5. .Al-Fawad cha Ibn Al-Qayyim (uk. 98)
  6. .Tazama: “Al-Isti`ab fi Ma’rifat al-Sahabah” cha Ibn Abd al-Barr (1/272), “Al-Isbah fi Takmis al-Sahaba” cha Ibn Hajar (2/222).




Miradi ya Hadithi