عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ ﷺ: «انْظُرُوا إِلَى مَنْ أَسْفَلَ مِنْكُمْ، وَلَا تَنْظُرُوا إِلَى مَنْ هُوَ فَوْقَكُمْ؛فَهُوَ أَجْدَرُ أَنْ لَا تَزْدَرُوا نِعْمَةَ اللهِ عَلَيْكُمْ»
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ ﷺ: «انْظُرُوا إِلَى مَنْ أَسْفَلَ مِنْكُمْ، وَلَا تَنْظُرُوا إِلَى مَنْ هُوَ فَوْقَكُمْ؛فَهُوَ أَجْدَرُ أَنْ لَا تَزْدَرُوا نِعْمَةَ اللهِ عَلَيْكُمْ»
Kutoka kwa Abu Hurairah, amesema: amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani ziwe juu yake) Tizameni walio chini yenu, 1- Na wala msitizame walio juu yenu 2- Kufanya hivyo ni sababu bora ya kuwafanya msizidharau neema za Mwenyezi Mungu kwenu ”
1. Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) anahimiza maswahaba zake na umma wote watizame walio chini yao katika mambo ya kiDunia, kama mali, sura na mfano wa hayo, kama mafakiri, wahitaji, madhaifu, wagonjwa, wenye mahitaji maalumu na wengine wengi, wataona jinsi Mwenyezi Mungu alivyo wafadhilisha.
2. Na Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) amezuia kutizama walio juu kiDunia na wenye nguvu na afya njema,
kama anavyo sema Mwenyezi Mungu:
“131. Wala usivikodolee macho tulivyo wastareheshea baadhi ya watu miongoni mwao, kwa ajili ya mapambo ya duniani, ili tuwajaribu. Na riziki ya Mola wako Mlezi ni bora na inadumu zaidi. .
[Twaha: 131]
3. Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) amebainisha sabau ya kufanya hivyo ni kupelekea wasidharau neema ambazo Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaneemesha. Mwanadamu akimtizama aliye chini yake kiDunia, anatambua kwamba, Mwenyezi Mungu amemfadhilisha zaidi kuliko watu wengi, atalipokea hilo kwa shukurani, kutenda wema na kuilipa neema hiyo kwa kufanya ibada. Ama akitizam wenye neema na akijikita kutizama maisha yao ya kidunia na jinsi Mwenyezi Mungu alivyo waneemesha, na hilo likampelekea kujilinganisha nao, itampelekea kukufuru neema za Mwenyezi Mungu na huenda likampelekea katika husda na kinyongo. Hadithi haimaanishi kwamba, mja aache Dunia, na wala asifaidike kwa alicho jaaliwa na Mwenyezi Mungu, bali makusudio asiruhusu Dunia kujikita katika moyo wake, kiasi kwamba haridhiki na alicho jaaliwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu.
1.Mwanadamu anaweza kuona au kusikia mtu ambae yuko vizuri kidunia, inatakiwa ajitibu mwenyewe kwa kutizama aliye chini yake, kama alivyo sema Mtume Mtukufu.A: “anapo ona mmoja wenu aliye bora kimali na umbile, basi amtizame aliye chini yake”[1].
2.Inatakiwa muumini aweke akhera mbele ya macho yake, asitizame neema za Dunia, na wala asikithirishe kuwatiza waovu, kwa hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaandalia waja wake wema katika Pepo: “mambo ambayo jicho alijawahi kuyaona, wala sikio kuyasikia, wala mwanadamu yeyote kuyawaza”[2], ikitoke jicho lake kutizama kitu chochote katika mapambo ya Dunia, basi asiipeleke nafsi yake huko, inatakiwa akumbuke neema za Mwenyezi Mungu Mtukufu ambazo amewaandalia waja wake wanao muogopa.
3.Badili kipimo chako cha kutathmini mambo, na ukumbuke kwamba neema za uhakika, hadhi na za milele, ziko Peponi. Kwa kufanya hivyo, utabadili tabia ya ushindani katika mambo ya kidunia na kuwatamani walio pewa neema hizo. Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) amesema: “hakuna husda ila katika mambo mawili; mtu ambae Mwenyezi Mungu amemjalia mali, akalazimika kuitumia katika mambo ya kheri, na mtu ambaye Mwenyezi Mungu amemjaalia hekima anaitumai kutatua migogoro na kusomesha”[3].
4.Kaaroon alipo vuka mipaka ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na akawa jeuri mwenye kiburi, kwa sababu ya neema alizo jaaliwa na
Mwenyezi Mungu Mtukufu, watu wanye nafsi dhaifu walimtizama kisha wakasema:
(: Laiti tungeli kuwa tunayo kama aliyo pewa Qaruni! Hakika yeye ni mwenye bahati kubwa.”
[qaswas: 79]
hawakuhifadhi macho na nafsi zao zisifitinishwe kwa neema za kidunia alizo jaaliwa, na wala hawakupata chochote katika neema hizo. Walikuwa kama alivyo sema mshairi:
Umeona ambalo haulimudu***wala hauwezi kulivumilia walau kidogo.
5.Amesema Ibn a’wn -Mwenyezi Mungu amrehemu-: nimeishi na matajiri, nikaona matatizo yangu yana naafu kuliko yao, na nimeishi na mafukara nikajihisi nina raha[4].
6.Muumini anapo tambua kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu amegawa riziki kwa hekima zake, nafsi yake inatulia, na wala hawazi vile alivyo wajalia wengine zaidi yake katika neema za kidunia.
7.Katika mambo makubwa yenye kuleta furaha katika moyo wa muumini, ni kutambua neema nyingi za Mwenyezi Mungu Mtukufu alizo mneemesha, na azitizame kwa jicho la mazingatio, na kutizama walio chini yake, kama alivyo sema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: “mwenye kuamka asubuhi kati yenu akiwa na amani, na akiwa na afya katika mwili wake, na akiwa na chakula cha siku hiyo, basi huyo ni kama amepewa kheri za dunia nzima[5] ”
8.Mtu anapo pata mtihani au msiba, kutizama walio chini yake kunapelekea kuona kwamba yeye ana nafuu,. Hilo litamfanya awe mvumilivu na kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa afya aliyo mjaalia.
9.Amesema mshairi:
Shikamana na uchamungu na rizika kwa alicho kujalia Mwenyezi Mungu***mja bora wa Mwenyezi Mungu ni yule mwenye kurizika.
Usihangaike na Dunia wala usiwe na taama***tamaa zinaweza kumuangamiza anaye jidanganya kuzifikia.
10.Na amesema mshairi mwingie:
Niliona kurizika ni vazi la utajiri***nikawa nashikamana nalo.
Heshima yake ikanivisha vazi ***masiku yanaenda bila kudhalilishwa. Nikawa tajiri bila hela***natembea nikiwa na heshimiwa kama mfalm