عن النَّوَّاس بن سَمْعانَ رضي الله عنه قال: سألتُ رسولَ الله ﷺ عن البِرِّ والإثمِ، فَقالَ: «البِرُّ حُسْنُ الخُلُقِ، والإِثْمُ ما حاكَ في صَدْرِكَ، وَكَرِهْتَ أَنْ يَطَّلِعَ عليه النَّاسُ».

Kutoka kwa Al-Nawwas bin Samaan, Allah amuwiye radhi, amesema: 1- Nilimuuliza Mtume rehma na amani zimshukie kuhusu wema na dhambi. 2- Akasema: “Wema ni kuwa na tabia njema. 3- Na dhambi ni ile inayokutia wasiwasi kifuani mwako, na unachukia watu kuijua”

Al-Nawwas bin Samaan bin Khalid Al-Kalabiy

Al-Nawwas bin Samaan bin Khalid Al-Kalabiy, aliyekuwa akiishi Sham, na baba yake, Samaan bin Khalid, walikuja kwa Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam na akasilimu Na akampa zawadi ya viatu vyake, basi Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam akavipokea na kumwombea dua, na Samaan alimuozesha Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam dada yake. Alipoingia kwa Mtume rehma na Amani zimshukie aliomba hifadhi kutoka kwake, na akaiacha, na akafa katika mwaka wa (50 Hijiriya). (50 AH) [1] 


Marejeo

1. Tazama ufafanuzi wake katika: “Ma’rifat al-Sahaba” cha Abu Naim (5/ 2701), “Al-Istifa’ fi Ma’rifat al-Ashab” cha Ibn Abd al-Barr (4/ 1534), na “Asad al-Ghaba” cha Ibn al-Athiir (4/ 591).


Miradi ya Hadithi