عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه : أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ ﷺ قَالَ: «إِنَّ لِلَّهِ تِسْعَةً وَتِسْعِينَ اسْمًا؛ مِائَةً إِلَّا وَاحِدًا، مَنْ أَحْصَاهَا دَخَلَ الجَنَّةَ»، زَادَ في رواية: «إِنَّهُ وِتْرٌ يُحِبُّ الْوِتْرَ». متفق عليه
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه : أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ ﷺ قَالَ: «إِنَّ لِلَّهِ تِسْعَةً وَتِسْعِينَ اسْمًا؛ مِائَةً إِلَّا وَاحِدًا، مَنْ أَحْصَاهَا دَخَلَ الجَنَّةَ»، زَادَ في رواية: «إِنَّهُ وِتْرٌ يُحِبُّ الْوِتْرَ». متفق عليه
Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) Amesema:
Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake:Hakika Mwenyezi Mungu ana majina tisini na tisa.mia moja ispokuwa moja,Mwenye kuyadhibiti ataingia Peponi.”Akaongeza katika riwaya nyingine: “hakika yeye (Mwenyezi Mungu) ni witiri anapenda witiri.”
imepokelewa na Bukhari Na Muslim
Hadith hii ni katika Hadith za msingi katika Majina Mazuri ya Mwenyezi Mungu:
Ametaja Mtume (Rehema na Amani zimshukie) kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ana majina tisini na tisa.Na wanazuoni wamekubaliana kuwa sio kwamba Hadith hii inamaana kuwa majina ya Mwenyezi Mungu ni tisini na tisa tu,bali makusudio yake ni kuhabarisha kuwa hayo (majina) tini na tisa atakaye yadhibiti ataingia peponi, sio kwamba idadi yake ni tisini na tisa tu[1]. Kwani Mwenyezi Mungu anamajina yasiohesabika kwa idadi na majina hayo yote ni mazuri na yamebeba sifa, matukufu, kama ilivyo katika dua ya mtume (rehma na amani ziwe juu yake) (ewe Mwenyezi Mungu ninakuomba kwa kila jina lako (zuri), ulilojiita mwenyewe, au uliloliteremsha kwenye kitabu chako, au ulilomfundisha yeyote katika waja wako, au ulilobaki nalo katika elimu ya siri[2])
2. Haya majina yaliyoelezwa kwa kusema: “Mia moja isipokuwa moja,” hii inamaana ya uthibitisho kwamba idadi hiyo ndio imekusudiwa, asije msikilizaji au msomaji akachanganya hilo.
3. Mwenyezi Mungu Mtukufu amewafadhilisha viumbe vyake kwa kufanya malipo ya kuyadhibiti majina hayo kuwa ni kuingia peponi, na hilo linatosha kuwa ni fadhila na malipo makubwa.
Na kudhibiti ambako ni sababu ya kuingia peponi kuna maana nyingi, Qur`ani imeeleza hilo pia na maneno ya waarabu, katika maana zake ni: - kuhifadhi (kuyakariri kichwani), kuyahesabu ili kuweza kuyafanyia kazi vizuri, na kufahamu vizuri kuisoma Qur`ani yote, kwani Qur`ani imejaa majina matukufu ya Mwenyezi Mungu.[3]
Kwa hiyo, kinachokusudiwa hapa ni: Mwenye kuyaamini, na kuyadhibiti kwa idadi, na kuyahifadhi na kuyafanyia kazi, ataingia Peponi[4],
Na Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake), hakubainisha majina hayo mazuri, ili aache akili zikiitafakari Qur`an na Sunnah, na ziiishi maisha ya kuyatafuta, ili ziweze kufikia malengo, na ziongeze juhudi ya kufahamu Kitabu cha Mwenyezi Mungu na maana yake, kama mtume alivyoficha saa ya kujibiwa dua katika siku ya Ijumaa, na usiku wa cheo.
4. Kisha Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake) akamwambia, kuhusu mojawapo ya majina makubwa ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambalo ni jina la Witr, na maana yake ni: Mmoja,(asiyegawanyika) kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu hana mshirika wala anayelingana naye, ndio maana matendo mengi ameyafanya kuwa witri, kama swala tano, kupata udhu sunnah ni mara tatu katika viungo vingi, na kutufu( kuzunguka Al ka`aba) mara saba, na siku za Tashreeq (kuchinja, kula na kunywa katika mwezi wa dhul hajah) ni tatu, na mbingu na ardhi ni saba.[5]
Mwenyezi Mungu amewaneemesha waja wake na akaweka wazi majina anayopenda kuitwa nayo, akasema Mwenyezi Mungu:
“Na Mwenyezi Mungu ana majina mazuri kabisa, basi muombeni kwayo”
[Al-A’araf: 180]
, na ameweka wazi kuwa mwenye kumuomba Mwenyezi Mungu kwa majina hayo ataingia Peponi. Haifai kwa Muislamu mwenye akili timamu anayejua kuwa Mwenyezi Mungu anapenda kuitwa kwa majina hayo, na kwamba amewaandalia Pepo wale wanaomwita kwayo kisha akazembea na kupuuza!
Mwenye furaha ni yule anayetumia akili yake vizuri na kukitafakari Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume wake, (rehma na amani ziwe juu yake), na akang`amua katika kitabu hicho majina yake mazuri, na akafahamu maana yake, na kuyafanyia kazi, kwa kuomba kupitia majina hayo matukufu, ili aweze kufaulu kuingia peponi.
Katika kuyadhibiti majina ya Mwenyezi Mungu ni kuyatumia katika kuomba dua, azidishe kunyenyekea na kuelekea kwa Mwenyezi Mungu kwa kutumia jina la Allah na kuomba kwa majina yake Matukufu kulingana na hali yake, kisha anasema: Ewe Mwingi wa Rehema., nihurumie, Ewe Mwenye kusamehe, nisamehe, Ewe mwenye kuruzuku, niruzuku, na kadhalika.
Katika kuyadhibiti majina ya Mwenyezi Mungu ni mja kuweza kutimiza haki za majina haya, na kuyafanyia kazi maana yake; mja atakapojua kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, atakuwa na uhakika na Yakini kwamba Mwenyezi Mungu atamruzuku,
Na kudhibiti jina la Mwenyezi Mungu, ambalo ni Mwingi wa Rehema, kunampelekea mtu kuwa ni mwenye kutarajia rehema zake na kumsukuma kuwa ni mwenye kuwarehemu viumbe Wake ili Muumba wao apate kuwarehemu.
Na kudhibiti jina la Mwenyezi Mungu, ambalo ni mwenye kuruzuku, kunampelekea mtu kumpenda Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa fadhila zake nyingi, na kutotafuta riziki katika njia alizoziharamisha Mwenyezi Mungu, kwasababu riziki zinatoka kwake, naye ni Mkarimu mwingi wa kutoa.
5. Ukipatwa na jambo; iwe neema au msiba, au jambo linalohitaji kufikiria, basi hudhurisha majina ya Mwenyezi Mungu kichwani kwako, ukiwa unazingatia kila jina na maana yake, iwe inaendana na hali yako, kisha muombe Mwenyezi Mungu kwa majina hayo, hakika utapata utulivu wa yakini na faraja ya moyo.
6. Tafakari majina ya Mwenyezi Mungu, kisha lolote utakaloweza kulifanyia kazi vizuri, - kama vile jina la Mwingi wa Rehema, Mkarimu, Mwenye kusamehe, Mwenye kusamehe na kustiri, na Mwenye kushukuru - basi lifanyie kazi. Na yale ambayo hayafai kuyafanyia kazi (ispokuwa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu) – kama jina la Mwenye Kujikweza. - Basi mwachie anayestahiki na kuwa mnyenyekevu, na mpole.
7. Kuwa na utaratibu wa kudumu wewe mwenyewe Pamoja na familia yako na marafiki zako, wa kuwa mnamtaja na kukumbushana jina miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu, kisha mkawamnaishi nalo katika matendo yenu ya kila siku, na mkajua maana yake, na athari za imani zilizofungamana na katika kujua maana yake, halikadhali tumieni vitabu vinavyoaminika katika kutambua maana ya majina ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, yanategemea yale aliyoyabainisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma naAmani iwe juu yake) na maimamu wa mwanzo, sio kutumia vitabu vinavyoashiria kwa dhana tu.
8- Mshairi anasema:
Ewe Mwenyezi Mungu nakuomba kwa majina mazuri, basi niitikie = nimeyadhibiti ili nipate baraka zake.
Tisini na tisa yote yamechorwa moyoni mwangu, na lile la (Allah) roho yangu iko tayari kutoka kwa ajili yake.
Na kwa majina hayo siachi kuwa mwenye kufuatilia na kujifunza = Kama ndege anayetarajia mwenye kiu alie kutana na umande,
Je, kwa ukarimu wako unaweza kumkatalia mwenye kuomba, kwa majina yako? = aliekesha usiku mzima gizani, akiomba nakukutarajia kwa kusema Ee Mwenyezi Mungu?!.