عَنْ وَرَّادٍ، كَاتِبِ المُغِيرَةِ، قَالَ: كَتَبَ مُعَاوِيَةُ إِلَى المُغِيرَةِ رضي الله عنهما: اكْتُبْ إِلَيَّ مَا سَمِعْتَ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ ﷺ، فَكَتَبَ إِلَيْهِ: إِنَّ نَبِيَّ اللَّهِ ﷺ كَانَ يَقُولُ فِي دُبُرِ كُلِّ صَلاةٍ: «لا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ المُلْكُ، وَلَهُ الحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، اللَّهُمَّ لا مَانِعَ لِمَا أَعْطَيْتَ، وَلا مُعْطِيَ لِمَا مَنَعْتَ، وَلا يَنْفَعُ ذَا الجَدِّ مِنْكَ الجَدُّ» وَكَتَبَ إِلَيْهِ: إِنَّه: «كَانَ يَنْهَى عَنْ قِيلَ وَقَالَ، وَكَثْرَةِ السُّؤَالِ، وَإِضَاعَةِ المَالِ، وَكَانَ يَنْهَى عَنْ عُقُوقِ الأُمَّهَاتِ، وَوَأْدِ البَنَاتِ، وَمَنْعٍ وَهَاتِ».

Kutoka kwa Warad, Mwandishi wa Al-Mughirah, amesema:Muawiya alimwandikia Al-Mughirah, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili:

1- Niandikie uliyoyasikia kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na Amani zimshukie na akamwandikia: 2- Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu alayhi wa sallam alikuwa akisema kila baada ya kila swala: “Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu mmoja, Peke Yake, hana mshirika, ufalme ni wake, sifa njema ni zake, na Yeye ni Muweza wa yote. 3- Ewe Mwenyezi Mungu hakuna kizuizi kwa ulichotoa wala mtoaji kwa ulicho kizuia. 4- Na hanufaishi mwenye utukufu, bali utukufu ni wako” 5- Na akamuandikia: “Alikuwa akiharamisha yaliyosemwa na kusengenya. 6- Kuuliza sana 7- Kupoteza pesa 8- Amekataza kuwaasi akina mama. 9- Mauaji ya watoto wachanga wa kike 10- Na kuzuia (kuwa na choyo) na kuchukua (kupenda kupewa)” .

Ni: Al-Mughirah bin Shu’bah bin Abi Aamer

Ni: Al-Mughirah bin Shu’bah bin Abi Aamer bin Ma-soud Al-Thaqafi, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, Abu Issa, sahaba mkubwa, aliyesilimu mwaka wa vita ya handaki, na akashuhudia Al-Hudaybiyah, na alisifika kwa werevu. Umar ibn al-Khattab, Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani, akamteua kuwa kamanda mkuu wa Basra, kisha Kufa, na alishuhudia al-Yamama na kufunguliwa kwa mji wa al-Sham, na jicho lake likaondoka huko Yarmouk.Alishuhudia Al-Qadisiyah na wengineo. Alifariki mwaka wa 50 Hijiria, na alikuwa Amir wa Kufa kwa Muawiyah bin Abi Sufyan, Mwenyezi Mungu awe radhi nao

Miradi ya Hadithi