عَنْ جَابِرِ بنِ عبدالله - رضي الله عنهما - قَالَ: «لَعَنَ رَسُولُ اللهِ ﷺ: آكِلَ الرِّبَا، وَمُؤْكِلَهُ، وَكَاتِبَهُ، وَشَاهِدَيْهِ»، وَقَالَ: «هُمْ سَوَاءٌ»

Kutoka kwa Jabir bin Abdullah – Mwenyezi Mungu awawie radhi wote wawili – amesema:

1-    “Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam, amemlaani 2. mwenye kula riba, mwenye kuilipa, 3. Na Wakala wa riba. 4. Na mwenye kuiandika 5. Na mashahidi wenye kushuhudia riba.” 6. Na akasema Mtume: “Wote wako sawasawa” .

Imepokewa na Muslim (1598).


Muhtasari wa Maana

Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam amelaani riba, mwenye kuichukua, mwenye kuitoa, na mwenye kuandika mikataba yenye riba, na mwenye kushuhudia hilo, na akaeleza kuwa wote hao katika madhambi wanalipwa sawasawa.

Miradi ya Hadithi