عنْ أبي هُرَيْرَةَ - رضي الله عنه - قال: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ: «إِنَّ اللَّهَ لَا يَنْظُرُ إِلَى أَجْسَادِكُمْ وَلَاإِلَى صُوَرِكُمْ؛ لَكِنْ يَنْظُرُ إِلَى قُلُوبِكُمْ». وَأَشَارَ بِأَصَابِعِهِ إِلَى صَدْرِهِ»


Kutoka kwa Abu Hurayrah – Mwenyezi Mungu amuwiye radhi – ambaye amesema:

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu alayhi wa sallam: 1. “Mwenyezi Mungu haangalii miili yenu wala sura zenu; 2.Lakini Yeye anazitazama nyoyo zenu. Na akaelekeza vidole vyake kwenye kifua chake



Vitendawili vya Qur'ani Vinavyohusiana

Amesema Mola Mlezi na mtukufu:

“Wala usinifedheheshe Siku watapo fufuliwa (87) Siku ambayo kwamba mali hayato faa kitu wala watoto (88) Isipokuwa mwenye kumjia Mwenyezi Mungu na moyo safi” .

[Ash- Shuaraa: 87 - 89]

Pia amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu :

“Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamungu zaidi katika nyinyi”

[Al-Hujurat: 13]

Amesema Mola Mlezi na mtukufu kuhusiana na hali za wanafiki:

“Na unapo waona, miili yao inakupendeza, na wakisema, unasikiliza usemi wao”

[Al-munafiqun: 4]

Miradi ya Hadithi