20 - NAFASI YA MASWAHABA RADHI ZA MWENYEZI MUNGU ZIWAFIKIE

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ: «لَا تَسُبُّوا أَصْحَابِي، لَا تَسُبُّوا أَصْحَابِي، فَوَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، لَوْ أَنَّ أَحَدَكُمْ أَنْفَقَ مِثْلَ أُحُدٍ ذَهَبًا، مَا أَدْرَكَ مُدَّ أَحَدِهِمْ، وَلَا نَصِيفَهُ».

Kutoka kwa Abu Huraira, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesema:

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Swalla Allaahu alayhi wa sallam."Msiwatukane Maswahaba zangu, Msiwatukane Maswahaba zangu,Naapa kwa yule Ambaye nafsi yangu imo mikononi Mwake, kama mmoja wenu akitoa dhahabu kama sawa na Mlima wa uhudi, basi hatafikia gao la mmoja wao, wala nusu yake.

Abd al-Rahman ibn Sakhr al-Dawsi

MSIMULIZI: Ni: Abd al-Rahman ibn Sakhr al-Dawsi, al-Azdi, al-Yamani, anayejulikana sana kwa lakabu yake, “lakabu ni jina la kupewa tu kwa utani” na hili ndio jina mashuhuri zaidi ya majina yote yaliyosemwa juu yake na jina la baba yake. Ni sahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amanizimshukie. Alikuwa akienda naye popote aendapo, na alikuwa miongoni mwa masahaba walio hifadhi na kusimulia hadithi nyingi sana kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehma na Amani ziwe juu yake, “kama alivyosema Al-Bukhari, Zaidi ya hadithi mia nane zilipokewa kutoka kwake –kati ya masahaba na matabiiy. Umar bin Al-Khattab aliMtumia kama gavana wa Bahrain, kisha akarudi na kuishi Madina na alikuwa ameshughulika na kusimulia hadithi na kuwafundisha watu kuhusu dini yao, na alikufa Madina mwaka wa (58 AH) [1]

Marejeo

  1. Rejea historia yake katika vitabu vifuatavyo: “Maarifaat al-Sahaba” na Abu Nu’aym (4/1846), “Alastieab Fi Maerifat Al'ashabi” na Ibn Abd al-Bar (4/1770), “Asad al-Ghaba” na Ibn al-Atheer (3/357), “Al-Isbah fi Tamazu al-Sahaba” cha Ibn Hajar al-Asqalani (4/267).


Miradi ya Hadithi