عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي اللَّه عنهمَا، عَنِ النَّبِيِّ قَالَ: «أَلْحِقُوا الفَرَائِضَ بِأَهْلِهَا، فَمَا بَقِيَ فَهُوَ لِأَوْلَى رَجُلٍ ذَكَرٍ» 

Kutoka kwa Ibn Abbas, Mwenyezi Mungu awawie radhi wote wawili, kutoka kwa  Mtume, rehema na amani zimshukie, amesema: “gaweni mitathi kwa kufuata wajibu kwa wale wanaostahiki, na chochote kinachobakia ni haki ya mwanamume

Abu Al-Abbas, Abdullah Bin Abbas Bin Abdul-Muttalib

Ni: Abu Al-Abbas, Abdullah Bin Abbas Bin Abdul-Muttalib, Al-Qurashi, Al-Hashimi Alizaliwa kwenye “Sha’ab Bani Hashim” miaka mitatu kabla ya kuhama, alikuwa ni marabi wa taifa na mfasiri wa Qur’an, binamu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu rehma na Amani zimshukie na alikuwa akiitwa: Bahari; kutokana na ujuzi wake; Mtume rehma na Amani zimshukie alimuombea dua kwa kusema: “Ewe Mola Mpe ufahamu wa Dini. [1] Na ni miongoni mwa maswahaba waliopokea hadithi nyingi sana, alisilimu akiwa mdogo sana, na alishikamana na Mtume Amani iwe juu yake baada ya kufunguliwa mji wa makka na akasimulia kutoka kwake. Alipoteza uwezo wa kuona mwishoni mwa maisha yake, na alifariki huko Taif katika mwaka wa 68 Hijiria. [2]

Marejeo

1.  Imepokewa na Al-Bukhari (6732) na Muslim (1615)

2. Imepokewa na Al-Bukhari (143) na lafudhi ni yake, na Muslim (2477).

Miradi ya Hadithi